Ukweli ni kwamba wapalestina hata wakiuwawa na waisrael pale sio kwao warudi walikotoka

Ukweli ni kwamba wapalestina hata wakiuwawa na waisrael pale sio kwao warudi walikotoka

Kazi kwelikweli nani aliyekwambia wafilisti ndio wapalestina?? Wafilisti wametokea ukoo wa caphtor mwana wa mizraim sasa wapi na wapi na wapalestina?? Hivi hii story mnaitoaga wapi kuwa wapalestina ni wafilisti??? Kwanni mnapotosha hata makanisani nasikiaga sana hadi nashangaa mnatoa wapi hizo taarifa....

Alafu kingine nchi ya ahadi kibiblia inafika hadi Euphrates na inaanzia mto nile mbona sijawahi sikia wakienda kuishi misri au iraq ambapo ndipo mto frati upo?? Why palepale mashariki ya kati?? Kana kwamba ardhi wanayodai kupewa ndio palepale tu kwanini hili kiasi wawatese wapalestina wasio na hatia

Mwisho kusema wapalestina warudi walipotoka ni kauli ya ajabu sababu hta wayahudi walihamia tu pale na walikuta wazawa......hivyo basi hakuna sababu yeyote ya kuwatesa wapalestina kama waliishi wa wagibeoni vizuri ingawa waliwakalia kimabavu basi waishi hivyo hivyo na palestina yaani nchi moja yenye haki sawa wakumbuke hata wao walipokuwa utumwani walipokelewa na nchi nyingi tu kwanni leo hii wawaone wapalestina kama hawana haki eti sababu walipewa hiyo nchi..... Mbona wao walipewa hifadhi nchi nyingi tu sembuse leo hii waone wengine ndio hawafai kuishi hapo!! Sio undumilakuwili huu

Mimi ni mkristo ila kiukweli hawa wayahudi wenye nywele nyeupe na macho ya blue!! Wanakosea sana
Hivi asili ya wapelestina ni wapi,mana Mimi nasikia tu story inayohusu hao Waisrael lakini story inayohusu wapelestina siikii, naomba mnisaidie hapo
 
Hivi hizi hoja mnatoa wapi.... Unasema canaan alilaaniwa kuwa atakuwa mtumwa hivyo unabii ukatimizwa?? Vipi kuhusu waisrael kuwa utumwani misri je nayo walilaaniwa?? Au waafrika kwenda utumwani nao tulilaaniwa.... Hivi kuna ufalme enzi hizo haukuburuzwa utumwani sasa why utumie hoja ya canaan kulaaniwa kuhalalisha issue ya israel kuikalia palestina?? Zina uhusiano gani??
Sasa jibu kwa kutumia historia ya mashariki ya kati. Kila sehemu ina historia yake, mfano wanyakyusa wana historia yao.
 
Haahaaaa acha utani bhana vizazi 10 vilipita baada ya Nuhu ndio abraham anazaliwa alafu unasema alizaliwa miaka 2 baada kifo cha nuhu?? Hivi unaweza kunipa huo mstari wa biblia

kasome mwanzo 11 sura nzima utagundua abraham kazaliwa miaka 400 toka kifo cha Nuhu hivyo unachosema hapa ni upotoshaji mkubwa sana ili tu kuitetea israel so sad!!!
Hahahhhaaaaa
 
Katika mizunguko yangu nilipita Aman Jordan, katika kutafuta sehemu ya kula nilielekezwa juu (gorofani) nikapanda na kula msosi wangu.
Baada ya hapo nikawa nazunguka zunguka mjini na kuona biashara zingine zikiwa juu

Ikabidi nimuulize mzawa, kulikoni biashara zingine zipo juu?

Akaniambia hivi, baada ya Palestine kuuza ardhi yao kwa waisrael sisi serikali yetu ikaleta mkakati kuwa ni marufuku kumuuzia au kumkodishia ardhi wa kuja.

Kwa hiyo ukiona biashara zote za chini n
(Ardhini) ni wazawa na juu tunawapangishia foreigners ili wasije wakadai kama jews

Sasa jiulize haya maswali

Kutembea raha sana
 
Hivi asili ya wapelestina ni wapi,mana Mimi nasikia tu story inayohusu hao Waisrael lakini story inayohusu wapelestina siikii, naomba mnisaidie hapo
Wafilisti ndio walianzisha eneo wakaliita palestina
Wa sasa hivi ni waarabu tu wasiostahili kuitwa wapalestina
Na wafilisti hawakuwa na eneo linaitwa Jerusalem sasa hawa waarabu wa kiislamu wanaodai Jerusalem ni yao wanajitafutia ubaya tu
 
Katika mizunguko yangu nilipita Aman Jordan, katika kutafuta sehemu ya kula nilielekezwa juu (gorofani) nikapanda na kula msosi wangu.
Baada ya hapo nikawa nazunguka zunguka mjini na kuona biashara zingine zikiwa juu

Ikabidi nimuulize mzawa, kulikoni biashara zingine zipo juu?

Akaniambia hivi, baada ya Palestine kuuza ardhi yao kwa waisrael sisi serikali yetu ikaleta mkakati kuwa ni marufuku kumuuzia au kumkodishia ardhi wa kuja.

Kwa hiyo ukiona biashara zote za chini n
(Ardhini) ni wazawa na juu tunawapangishia foreigners ili wasije wakadai kama jews

Sasa jiulize haya maswali

Kutembea raha sana
We kichaa kweli ulishasikia Israel ana shida na Jordan [emoji1137]
Shida ni hivi viarabu vya kiislamu vinadai Jerusalem ni yao
Kwa hapa watapata tabu sana
 
Wewe unaeandika utumbo na kuwapenda utafikiri unawajua kiundani
Tembea dogo uione dunia sio kunukuu
Unajua falasha yaliyowapata
Mimi nimefika huko kote na kuona mengi wewe endelea kusoma tu
Maneno yako hayo yamekufanya uonekane kichaa
 
Miongoni mwa Wapalestina wapo wana wa ukweli wa Israel isipokuwa tu walikuwa arabised na christinized na falme zilizofuata!. Viongozi wa Israel wanalijua hili toka kale, na Ben-Gurion kabla hajawa Kiongozi wa Taifa la Israel aliliandika sana hili.
Mathalani baada ya Ben Gurion kuwa kiongozi mkuu wa Taifa la israel aliendesha Operesheni ya Kuwafundisha Uyahudi Mabedouin wa kiarabu huko Katika Majangwa Ya Israel "akitaka warudi katika asili yao", Lakini Mabdouin walimkatalia na hivyo operesheni kusitishwa.
 
Unaweza kumthibitisha walau huyo Mungu unaesema ardhi ile ni ya kwake?
Kama utaweza kuthibitisha uwepo wake pia fafanua mbona historia ya kitabu chako unachosimamia kinasema kuwa kabla ya hawa watoto wa Ibrahim kuiteka nchi ile walipambana kwanza na wenyeji wa pale? Kwahiyo tukubali watoto hawa wa Ibrahim waliingia vitani na Mungu unaemmaanisha?
Nakuuliza hivi sababu umesema nchi ile ilikuwa ya Mungu wako.
Una maswali kuntu sana.Yaani ngumi jiwe.Ili wajinga wajinga wasizoee kuvamia jukwaa hili la watu wenye IQ ya juu
 
Kwa utafiti wangu tu nimegundua wakanaan hawapo tena
Wafilisti hawapo tena
Waliopo pale ni waarabu wa kiislamu waliovamia tu
Warudi kwao wawaachie wayahudi eneo lao
Mkuu hivi waarabu na wapalestina Ni watu tofauti?
 
Wafilisti walikuwa kabila la watu wa Ulaya ambao walivuka Bahari ya Kati na kisha kushindwa kuvamia Misri waliteka pwani ya Kanaani (1175 KK hivi) wakifaidika na silaha za chuma walizozitumia dhidi ya watu waliokuwa na zile za shaba tu, wakiwa wenyeji au Waisraeli.

Ingawa hawakuwa wengi, waliathiri sana nchi yao mpya, kiasi cha kuiachia jina la Palestina.

Habari nyingi juu yao zinapatikana katika Biblia.
jiulize na asili yako wewe wapi
 
hakuna mtu ambae asili yake ni pale alipo otherwise ww uwe mlima au jabali
 
Unazungumzia biblia hii yenye vitabu kama series ya jumong na kufanyiwa marekebosho kutokana na dunia inavyokwenda au? tuanzie hapo.
hivi biblia imekosa heshima kwa watu kwa kiwango hiki...!? isee
 
Wafilisti ndio walianzisha eneo wakaliita palestina
Wa sasa hivi ni waarabu tu wasiostahili kuitwa wapalestina
Na wafilisti hawakuwa na eneo linaitwa Jerusalem sasa hawa waarabu wa kiislamu wanaodai Jerusalem ni yao wanajitafutia ubaya tu
umeongea kishabiki sana,maneno matupu huna hata reference ya hayo uliyoropoka umeamua tu kusema"wafilisti" mara "wapalestina" mara "waarabu" umependa tu kusema hivyo ila huna reference umetoa wapi huo ujinga wako umerefer nini?!
 
Kingine labda usichokifahamu ugomvi wa Wayahudi na Wapalestina wewe kama mtu mweusi haukuhusu kwa maana hauelewi na kwanza wote wawili Wayahudi na Wapalestina hawakupendi na wanakuona nyani tu!
Duu hii kali!
 
Back
Top Bottom