Ukweli ni kwamba watu wengi wa Dar es Salaam wamezidiwa kipato na watu wa mikoani

Moja ya seemu ambayo siwezi kuishi ni DSM, kutoboa ni pagumu sana,kuish dar panagarama sana,

Kodi ya nyumba,nauli Kila siku,usipopiga hesabu vizuri utaish maisha ya kupanga ad kufa,

Dar utavaa vizur,Bata nying,totoz,ila kutoboa hiiii bagosha
 
Andiko hili linatokana na taarifa kuwa kipato cha kila Mwanadalisalama kimepanda kwa sh. Laki tano. Haya mambo ya takwimu si ya kuyategemea sana. Kwa kifupi takwimu hizi zinaficha ukweli kwamba wakati matajiri wanaogelea katika bahari ya mabilioni, akinayakhe wamezama katika lindi la tope la ufukara.
 
Huko mikoani ni wapi? Na Dar sio mkoa wa Tanzania? Mbona mnanichanganya au Dar ni nchi inayojitegemea.
 
"Tanzania ilivyokuwa na ardhi kubwa mpaka nyingine imekuwa kama haina mwenyewe lakini kuna kijana hana hata umiliki wa square meter nne za mraba katika nchi hii, kazi kutunza ndevu na nywele tu".
 
Wapi huko ndizi moja 300 hujui kuna masoko hapo kuna bidhaa ni bei rahisi kuliko mikoani
 
Kiufupi uchumi wa dar umeshikiliwa na watu wachache huku wengine wakibaki kuwa machinga na wachuuzi

Watu watatu kama mo,bakhresa na gsm wameshikilia uchumi wa maelfu ya watu
 
Ni Dar tu niliona kwa mara ya kwanza watu wanakula mpaka utumbo wa kuku ambao kijijini hata mbwa tukiona anakula tunampiga. Ila ndiyo hivyo umasikini wa kujitakia uliochangiwa na rushwa na ulafi wa CCM umetuleta hapa.
 
Unafananisha world cup na ndondo dsm ni world cup kitendo Cha kucheza world cup tayari unakuwa umeweka heshima ya pekee Sana .
Endelea kujidanganya na world cup yako! watu wanapiga pesa masasi na kahama huko utakuja kushtuka upo nafasi ya mwisho kwenye kundi lako la world cup.
 
Upo sahihi.
 
Mimi hapa asubuhi breakfast nimetumia 1200 mtu mmoja, ningekua bush hii hela ningekula breakfast nzito, mchana ugali na sato mkubwa usiku wali maharage ya kumwaga. Wqtu wa dar tuna mioyo Migumu.
Sato yupi huyo wa 1200 we bwege! unaijua sato unaisikia?
 
Kopesha watu wote watakulipa ila sio watu wa dar hawalipi madeni hata elfu 20 mtu anaingia mitini na anafanya kazi ya mwisho wa mwezi ila wa mikoani zege hailali dar ukimpa mtu elfu 10 akikuona anabadilisha njia jiji limezidiwa na population.
 
Mbona ni standard kbs ukienda vibaya unauziwa 350
Ndizi mitaa mingi dar hakuna tofauti na mikoani sh 100 ndizi nyingi zinatoka hapo moro njoo nikuoneshe labda huko supermarket ndio mnauziwa ndizi 300
 
Magorofa mengi yapo wapi?

Magari mengi yako wap?

Maduka mengi yako wapi?

Kama hivyo vitu vipo kwa wingi Dar basi mmezidiwa kipato watu wa mikoani poleni sana
Hao hao wa mikoani wakija dar hawataki kurudi kwao,kijijini kugumu sana wasitudanganye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…