Ukweli ni kwamba watu wengi wa Dar es Salaam wamezidiwa kipato na watu wa mikoani

Baba nchi ishavurugwa, achana na hizo stori. Ongelea ya kwako🤣.
Watu tumekaa kote.

Mkoani utapaona patamu ukiwa na kazi au biashara inayoeleweka, gharama za maisha ziko chini. Dar napo hivyo hivyo utapaona New York kama kipato chako ni cha kati kwenda juu.

Huna hela, una kipato cha chini mziki wa mkong'onto wa maisha ni ule ule tofauti ni tempo tu na dj anavyo scratch🤣.

Kwa experience, nimewahi kubeba box za weight ya kawaida Dar kwa masaa kadhaa nikalipwa 50k, lakini Mwanza kazi ya 50k mpaka utawaza kwanini umezaliwa,ungekuwa hata wingu tu unyeshe uishe.

Mada za hivi huwa hazijengi, ungeiandika kwa namna nyingine utoe ushauri hata wa vijana ku invest katika kununua ardhi na kuziendeleza hata kwa manufaa ya vizazi vya baadae sababu mwaka 2100 Tz itakuwa inamiliki 1.02% ya global GDP ikiwa nafasi ya 19 kwa uchumi duniani.

Hivyo grand,grand children wata enjoy😊.

Maana mkitoka hapo huwa mnaanza makabila,Wachaga wengi wana maisha mazuri kuliko Wahaya, badala ya kuwaza mchaga mimi na Mhaya mtoto wa Ali Mufuruki(R.I.P) tunafanana au naishi kwa tabu.
 
Umeona mfano wako ulinganishe kati ya Mwanza na Dar hukuona mkoa mwingine acheni hizo.
 
Kuishi DSM peke Yake ni Mafanikio sio kila Mtu anaweza kuishi dsm na akaweza hata kupata milo mitatu.

So Mkuu hili jiji sio kila mtu anaweza kulimudu akaingia na akatoka salama hapa DSM ni world cup.
Kwa hiyo maisha ni kumudu milo mitatu tu!....!?bwege sana wewe!

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Nonsense

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…