Ukweli ni upi : Alexander the Great akiwa INDIA

Ukweli ni upi : Alexander the Great akiwa INDIA

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Posts
20,537
Reaction score
31,729
picalexander12.jpg

Habari za jioni wakuu bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye mada

Natumaini wote tumeshasikia mengi sana kuhusu alexander the great ila kuna mambo machache yananitatiza na tusaidiane kujuzana kuhusu mtawala huyu.

ALEXANDER NI NANI
images (36).jpg

Alexander III wa Macedonia alizaliwa 20/21 July 356 BC na kufariki 10/11 June 323 BC (Miaka 33) maarufu kama Alexander the Great aliyekuwa mfalme wa nchi ya makedonia iliyokuwa ndani ya ufalme wa kigiriki na alitumia muda wake mwingi wa maisha kupigana vita za kuteka miji mbalimbali ili kuongeza ufalme wake

UMAARUFU WAKE
images (33).jpg

Umaarufu wake ulikuja baada ya kuwa mwanajeshi asiyewahi kushindwa vitani na kufikia umri wa miaka 30 alikwisha angusha falme zote kubwa zilizokuwa tishio kati ulimwengu wa kale akitandika mataifa makubwa kuanzia ulaya,Afrika hadi Asia hivyo anatazamiwa kuwa commander bora zaidi wa kijeshi katika historia.

ALEXANDER AKIWA INDIA
baada ya kupata picha kidogo ya nani anazungumziwa twende moja kwa moja kwenye swali langu JE NINI KILITOKEA KWA ALEXANDER INDIA
images (37).jpg


Alexander baada ya kuvamia ufalme wa uajemi na kuutandika alielekea India akiwa na ndoto za kuifikia china hivo kutawala Asia nzima. Lakini kuna vita ilipiganwa kati yake na mfalme Puru/porus iliyozaa utata mkubwa.

1. Kwa upande wa wazungu wanadai Alexander alimpiga mfalme Porus na kwamba aliposhinda alimuona Porus ni mzuri vitani sababu alimpa ushindani hivyo akaamua kumrudishia ufalme wake wa hilo eneo aliloteka na alexander akaamua tu kugeuza kurudi uajemi baada ya wanajeshi wake kuweka mgomo kuwa wamechoka!!

2. Kwa upande wa wahindi wanadai alexander alipigwa sana na Puru hivyo akaamua kuomba poo na kusaini naye mkataba wa amani maana alisikia kwamba huko mbele kuna falme zina jeshi la tembo elfu 5000 wakati Puru alitoa upinzani kwa tembo 100 tu hivyo akaogopa sana na kuamua yaishe na arudi alipotoka maana wanadai kama alexander alishinda kwanni ageuze?? Kwanni ampige Puru alafu asimuue wala kumpora utawala wake??
images (35).jpg


Maswali ya kujiuliza GT
1. Alexander the Great anafahamika kwa ukatili wake awamo kwenye uwanja wa vita ssa iwaje hapa aliguswa na huruma ilihali alichomwa mkuki ambao ungeweza muua ila bado akamsamehe Porus na kumuachia eneo hilo alitawale????!!!

2. Kingine kabla ya vita hyo alexander alikwisha ingia ubia na mfalme Ambhi wa taxila ambaye aliahidiwa kama atamsaidia kumpiga mfalme porus watagawana utawala na mfalme Ambhi sasa najiuliza kama walishinda vita kivipi huyu Ambhi hakupewa huo ufalme alioahidiwa ila huyo huyo aliyepigwa yaani Porus ndio aliambiwa aendelee kutawala?? Na wala hakuna ushahidi wa kishitoria unaoonyesha mfalme ambhi akilalamika kunyimwa ahadi na alexander je kama kweli alexander alishinda kivp nchi hakupewa Ambhi.

3. Hoja nyingine ni kwamba wanadai jeshi la alexander liliamua tu baada ya kushinda kugeuza nyumbani eti kisa wamechoka?? Swali langu ni hili maeneo yote ambayo wanajeshi wake waligoma walinyongwa na pia jeshi lilikuwa na utaratibu wa kubadilisha wanajeshi ambapo waliokaa muda mrefu walirudishwa na vijana fresh wabichi kabisa walichukuliwa kuongeza nguvu sasa waliochoka ni wakina nani?? Pia kabla ya hapo ukimgomea alexander unachinjwa sasa ni muujiza gani walitumia hao askari kumpinga alexander na hakuwachinja??

HITIMISHO
Baada ya vita hii alexander alijeruhiwa vibaya sana na alifia akiwa huko babeli alipokuwa anarudi kutoka India na hata farasi wake alifia kwenye vita hiyo ya India!! Na baada ya hapo utawala wake ulimeguka baada ya wanajeshi wake kugombea madaraka hivyo jeshi kugawanyika na utawala kuporomoka na mpaka anakufa wazungu wanadai alexander hakuwahi kupigwa na hata kuna muda ulifika akaanza kulia sababu amekosa wapinzani wa kupigana nao hapa dunia!!! Je Great thinker unafkiri kuna historia inapotoshwa kuhusu mtawala huyu wa kipekee au historia yake ina usahihi 100% bila chumvi yeyote

Naomba kuwasilisha
images (34).jpg
 
Mungu Ni Mwema Wakati Wote
Hongera Sana Mkuu
Kuleta Bandiko Zuri Nadhani Ni Kwa Moyo Uliojaa Shukrani Sana Kutaka Tujue Haya Japo Hata Kama Baadhi Yetu Tunayajua.

Hongera Sana! Muda Siyo Mrefu Members Watakuja Kutupa Zaidi Kila Mtu Kwa Mtazamo
 
kumuita "the great" huwa inanikera sana
huyu anafaa kuitwa alexander the barbarian/the greek
mtu anavamia nchi za watu,anaua,anakalia kimabavu halafu anaitwa the great
alichofanya kemet/ancient egypt mshenzi huyu ndio sababu waafrika tumekuwa dhaifu sana
 
kumuita "the great" huwa inanikera sana
huyu anafaa kuitwa alexander the barbarian/the greek
mtu anavamia nchi za watu,anaua,anakalia kimabavu halafu anaitwa the great
alichofanya kemet/ancient egypt mshenzi huyu ndio sababu waafrika tumekuwa dhaifu sana
True
 
Muuaji Wa Kizungu Anaitwa ' The Great '.

Wanasema Alikufa Kwa Malaria Na Wengine Wanasema Typhod Fever 😀

Lakini Katika Mapigano Yake Akaja Kukutana Na Wapinzani Wanaotumia Tembo( Itakuwa Ndo Hao Kina Porus), Hakuzoea Vita Ya Namna Hii, Alipigwa Vibaya Na Kiongozi Wake Wa Jeshi Akaona Amkimbize Alex' Nyumbani Kukwepa Kipigo, Lakini Tayari Alikuwa Amejeruhiwa Vibaya,kufika 'babeli' Mhuni Akadanja.

Na Huo Ndio Ukweli Ninao Uamini...
 
Ni kweli alikua shujaa alipiga nchi nyingi tu kwenye utawara wake, lakini kipindi hicho anawapiga nchi nyingi na kujibebea rundo la sifa kuna wanaume walimsoma na kujaribu kufatilia kwa Karibu mbinu na utendaji wake akiwa kwenye uwanja wa vita.

Wakagundua wakienda kupigana kwa miguu/ana kwa ana au farasi kwenye uwanya wa Vita hawatamshinda kwani alikua mzoefu sana huyu bwana kwenye maswala hayo, wakaamua kutumia tembo ambapo waliona kweke lazima ingekua ngumu kuwashinda kwani Katika kuchunguza kwao waligundua bwana Alex hakuwahi kupigana vita ya namna hiyo kama yao waliyopanga kuingia nayo kwenye uwanja wa vita kwaiyo wakawa na imani kiasi frani kuna watashinda
Lisha ya Alex kutisha katika nyanja ya vita kipindi hicho.

Ukweli ni kwamba jamaa alipewa kipigo hakuwahi kudhania katika maisha yekee kwamba kuna siku itatokea Kama hiyo .

Na wakati analia siyo kwamba alilia kwasababu hakuona wakushindana nnae hapa duniani,,. ...la ,.. Alilia kwasababu alipigwa na jeshi ambambalo hakulidhania na hakutarajia,
Sema wazungu huongeza sana chumvi kwenye baadhi ya historia.
 
Back
Top Bottom