Satoh Hirosh
JF-Expert Member
- Mar 30, 2021
- 6,432
- 25,646
Salaam,
Kumekuwa na tetesi huwa naisikia miaka kadhaa sasa kuhusu hii hospitali ya Mloganzila. Hadi naandika huu uzi ni kwa sababu kuna ndugu wa rafiki yangu wa karibu ambae ni mgonjwa na ameambiwa aende Mloganzila kupata matibabu.
Iko hivi; Nilikuwa Nimekaa nae tunapiga stori za kupoteza siku mara simu yake ikaita Kisha akapokea. Maongezi yalikuwa kuhusu mtu ambae ilionekana anaumwa(ndugu wa huyu jamaangu ambae tunapiga stori) na wamepewa rufaa wampeleke huyo mgonjwa Mloganzila. Sasa huyu bwana ambae nilikuwa nae tukipiga stori akawa mkali Sana kwenye Yale maongezi anasema "Hapana,Mloganzila hapana kwa kweli,tuongee na docta ili mgonjwa wetu aende Muhimbili ila siyo Mloganzila. Mnataka afe?"
Baada ya maongezi ya simu kuisha nikamuuliza jamaa; Hivi kwa nini mnakataa kumpeleka huyo mgonjwa Mloganzila,mnakomaa aende Muhimbili badala yake? Akajibu ndugu Mloganzila pale ni njiapanda ya kuzimu,Ukimpeleka hospitali nyingine alafu Doctor akakuandikia rufaa au akakushauri umpeleke mgonjwa wako pale ni Kama hamtakii heri mgonjwa maana uhakika wa kurudi home mzima ni mdogo Sana.
Sasa hii ni stori ya juzi,tena nimesikia kwa mtu anayenihusu,ila maneno Kama haya kuhusu Mloganzila binafsi sijaanza kuyasikia leo wala Jana. Nimewahi kusikia maneno Kama haya mwaka Jana msibani maeneo ya kwa azizi nilipoenda kumzika mzee wa rafiki yangu "mzee aliumwa kidogo tu badala ya kumpeleka temeke wao wakampeleka Mloganzila,ona Sasa kilichotokea" .Haya Ni baadhi ya maneno niliyosikia pale msibani. Pia hata kwenye maongezi ya kawaida vijiweni kuhusu maswala ya afya na magonjwa likitajwa jina la hii hospitali lazima Kuna watakaoguna tu. "Mmh mgonjwa wenu yupo wapi? Mloganzila? Mmh" maneno Kama haya nimeyasikia Mara kadhaa mtu akiongelea habari ya mgonjwa aliyeko Hapo hospitali.
Sasa wakuu,
Hii ina ukweli kiasi gani? Au ni uzushi Kama ule uzushi kuwahusu bodaboda kwamba wakipelekwa Muhimbili kwenye ile ward yao maarufu lazima wakatwe mguu kitu ambacho siyo kweli? Na Kama siyo kweli wahusika walitoa ufafaunuzi au kukanusha?
Niliwahi kumsikia kiongozi mmoja wa Muhimbili kwenye redio fulani akikanusha uvumi/uzushi ulioenea kuhusu majeruhi wa ajali za bodaboda kwamba wakipelekwa Muhimbili madaktari hawajisumbui kuanza kuhangaika kuwatibia,badala yake wanawakata miguu,mchezo Kwisha. Jamaa alitoa ufafanuzi mzuri na ukaeleweka. Ila hili la Mloganzila sijawahi kusikia mahali popote likiongelewa/kujadiliwa na wahusika.
Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app