Hii hospitali irudishwe MUHAS....kwani wao ndio wamiliki kuanzia wazo la ujenzi na pia isitoshe imejengwa kwenye plot yao.
MUHAS pia wanaweza kuifanya ile taasisi ikaleta mapinduzi makubwa sana kwenye sekta ya Afya wasipoleta maslahi yao binafsi kama walivyofanya walipokabidhiwa ule mradi
Nimependekeza iendelee kuwa Chini ya Prof Janabi kwa sababu muelekeo chanya umeanza kuonekana,
anafanya vizuri kwa sababu anajali utu na maslahi ya wafanya kazi wake, JKCI ipo pale sababu ya maslahi bora, wala si vinginevyo, na pale MNH UPANGA na MLOGANZILA pameanza kuonesha mwanga sababu ameanza kuwalipa vizuri wafanya kazi wake, wala hakuna muujiza mwingine,
Hospitali ya Taifa Muhimbili Upanga na Mloganzila ndio icon la Taifa letu kwenye kutoa huduma, haziitaji majaribio kwenye utendaji, zinahitaji mtu smart kuziongoza, Hospitali zilizo chini zinatakiwa zijifunze kutoka kwao, mambo mazuri yanatakiwa yaanzie kwao yashuke hadi ngazi ya zahanati na vituo vya Afya.
Hospitali nyingi Duniani zinazo milikiwa na vyuo ndio zinaongoza kwa kutoa matibabu ya hari ya juu, sipingi MUHAS kurudishiwa hospitali yao, ila wanatakiwa wajipange haswa.
Ile hospitali kuiendesha si mchezo, imewekewa mazingira kama ya First World, AC kila mahali, escalator, ventilation, system za moto, nk, hivyo vyote vinakula umeme wakutosha,
Kuendesha Hospitali ile kunahitaji ubunifu wa hari ya juu, na si kwa kutegemea ruzuku ,
Inahitaji kuwa na huduma za ziada amabazo hazipatikani nchini, pamoja na nchi zinazo tuzunguka,
Watengeneze mazingira yatayowavutia wateja kwenda pale, badala ya watu kukimbilia kwenda kutibiwa nje ya nchi,
kwa hadhi ya hospitali yenu Agakhan inatakiwa iwe inakuja kujifunza kwenu mkitumia fursa mliyo nayo.
Mfano kuhusu malazi, eneo la kibamba hakuna hotel na lodge za maana, hospitali inaweza kuingia ubia na sekta binafsi wajenge lodge na hotel za kueleweka, ndugu wa wagonjwa wasisumbuke sehemu za kufikia,
Ile stand ya pale, nayo inawachafulia mandhari ya pale, ombeni mjengewe stand inayo endana na hadhi ya hospitali yenu.
Sehemu za kupata chakula nazo zipo chache, ikifika saa 12 wameshafunga, hadi uamue kwenda kibamba chama ndio unaweza ukapata chakula cha kueleweka,
Wafundisheni staff wenu customer care nzuri, hii dunia ya ubepari, mgonjwa akija leo mkamzingua kupata majibu na matibabu kwa haraka kesho harudi kwenu, ataenda aghkhan, rabininsia, n.k
Waondoleeni staff wenu njaa njaa zisizo za maana, walipeni stahiki zao kwa wakati, hili nchi za wenzetu ndio walipotuzidia, nurse, daktari, mtoa huduma wa afya kama kipato hakieleweki msitegemee miujiza kwenye kutoa huduma bora, wataishia kupiga part-time (vijiwe) na kuacha taasisi za umma zikiendelea kujikongoja kutoa huduma,
majibu mabovu kwa wagonjwa na customer care mbovu asilimia 90% inachangiwa na vipato duni vya watoa huduma, asilimia 10% ni tabia ya mtu mmoja mmoja.
tukumbuke wanatumia muda wao mwingi hospitali, wengi wao hawana sehem nyingine za kuwaongezea vipato, wanatoka kazini muda umeenda, ukiongeza changamoto za usafiri wanafika majumbani usiku,
kesho yake saa moja anatakiwa kuwahi kazini, bado hajaingia night shift, hakuna kulala usiku mzima, na bado wapo wachache, ikifika jioni mtoa huduma hoi, kila kiungo kinamuuma,
maslahi kiduchu, anawaza atarudi vipi nyumbani, na kesho ataacha nini nyumbani watoto wapate chakula.
Tembeleeni hospitali mkajionee wanayo yapitia watoa huduma wa afya, muda ambao sisi tumelala wao wanapigania uhai wa ndugu zetu, bado hatujawananga mitandaoni,
inahitaji miujiza kupata customer care nzuri kwa mtoa huduma wa afya anayepitia mazingira hayo.
Niwape kongole watoa huduma wote wa Afya nchini, kwa kuendelea kuokoa uhai wa ndugu nzetu, japo mnapitia changamoto nyingi na mazingira magumu ya utendaji kazi,
Msichoke mna Hazina yenu mbinguni, mnafanya kazi ya Mungu ya uponyaji, japo mnapitia changamoto nyingi za maisha.
Nchi za wenzetu katika kada zinazolipwa vizuri kada ya Afya inaongoza,
"A healthy nation is a wealthy nation, and every life matters. If you’re healthy, you can wish anything. If you’re not healthy, you wish only to have your health back. That’s why health is the foundation."