Kuingiza siasa kwenye taaluma, msigano kati ya Muhimbili Upanga na Chuo cha MUHAS enzi hizo ndio kulifanya Hospitali ya Mloganzila mwanzo kufanya vibaya,
Kipindi Hospitali inafunguliwa kuna maagizo yalitoka juu ya kuwa hamisha wagonjwa kutoka MNH UPANGA kwenda MLOGANZILA, ili kupunguza msongamano wa wagonjwa MNH-UPANGA,
MNH-Upanga nao wakatumia mwanya ule waliopewa wakawa wanachagua wale terminal ill patients wa internal medicine(wagonjwa wa magonjwa ya ndani) ndio wakawa wanawapeleka Mloganzila, wakifika kule wakawa hawachukui muda wana fariki, ndio jina baya la Mloganzila lilianzia pale.
ila kwa sasa kwa Afrika Mashariki na kati hakuna Hospitali yenye mazingira na miundombinu bora kuizidi mloganzila, na kwa sasa inafanya vizuri nadhani ni hospitali chache sana hapa nchini zinazidi Mloganzila kwenye kutoa huduma.
Nendeni mkatibiwe Mloganzila mtakuja na majibu tofauti na mnayo yasikia na kuyasoma Mitandaoni, wana jitahidi sana kwenye kutoa huduma, watoa huduma wao wana kauli nzurI, na wanawajali wagonjwa, mimi binafsi ni shahidi, ndio imekuwa kimbilio langu napopata changamoto za kiafya.
Kipindi cha COVID-19 wagonjwa wa COVID walikuwa wakiponea pale, wengi ni mashahidi.
Kwa sasa chini ya Prof Janabi imekuwa na muelekeo mzuri zaidi, na staff wa pale wengi ukiohojiana nao wanamkubali sana huyu mwamba Prof Janabi, anajali maslahi wa wafanyakazi wake, na hii imeongeza morari ya watoa huduma pale Mloganzila na Upanga kwa ujumla,
Naskia kuna msigano unaendelea kati ya Chuo cha Muhimbili na Muhimbili Upanga nani anapaswa kuiendesha Hospitali,
Kama mdau wa Afya nawashauri mwacheni kwa sasa Prof Janabi aendeshe ile Hospitali ana maono na muelekeo mzuri zaidi, na amefanikiwa kuleta mabadiliko chanya toka akabidhiwe Hospitali ya Upanga na Mloganzila, ataleta mapinduzi makubwa sana kwenye hizi Hospitali mbili za Taifa, kama alivyo fanya pale Taasisi ya Moyo ya JKCI.