Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Kafara

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2007
Posts
1,396
Reaction score
425
Mengi yamesemwa kuhusu Mzee wetu huyu na sisi tuliokuwa shuleni wakati ule tulilishwa kile ambacho naamini ni sumu. Wakubwa tuelimisheni ukweli kuhusu Mzee huyu.


Oscar Kambona


Hii ameandika Simon Martha Mkina

Natumaini waandishi wa historia ya tanzania watampa nafasi yake kwa mchango mkubwa aliyoutoa.
RIP Mzee Kambona

Oscar Salathiel Kambona, alitaka kumpindua Nyerere kwa kushirikiana na wapiganaji wa Umkhonto.

=======

kichakaa man, ameandika;

Marehemu Oscar Kambona alizaliwa mwaka 1925 katika kijiji cha Kwambe kilichopo mwambao mwa ziwa Nyasa, karibu na Mbamba-bay, wilaya ya Mbinga, Mkoa wa Ruvuma. Alikuwa mtoto wa marehemu Rev. David Kambona na Bibi Miriam Kambona.

Rev. Kambona alikuwa ni miongoni mwa waafrika wa kwanza kupata upadre katika kanisa la Anglikana la Tanganyika. Wakati Oscar Kambona akiwa mdogo, baba yake alikuwa akimweleza kuhusu ndoto zake juu ya uhuru wa nchi yake, hivyo Oscar alikuwa akiwa na hamu sana ya kuitumikia nchi yake.

Oscar alipata elimu ya msingi nyumbani kwao, chini ya mwembe (ambao bado upo), katika kijiji chao kwa kuwatumia wazazi wake wote wawili na mjomba wake, ambao wote walikuwa walimu. Baada ya hapo alipelekwa shule ya kati ya Mt. Barnabas, Liuli, na baadaye shule ya Sekondari ya Alliance, ambako alilipiwa ada na Askofu mzungu wa Anglikana kwa vile baba yake hakuweza kumudu kulipa ada ya paundi 30 kwa mwaka.

Oscar alikuwa akisimulia jinsi alivyoweza kumshawishi Askofu huyo amlipie ada kwa kusema sala ya Baba yetu kwa kizungu. Oscar alichaguliwa kwenda ‘Tabora Boy’s Senior Government School’, ambako alionana na Julius Nyerere kwa mara ya kwanza; wakati huo Nyerere alikuwa anafundisha katika shule ya kikatoliki.

Baada ya kumaliza masomo ya sekondari alienda katika shule yake iliyopita ya Alliance kama mwalimu na baadae alichaguliwa kuwa ‘Schoolmaster’. Ilikuwa katika mkutano wa kitaifa wa walimu, mnamo mwaka 1954, ambapo Kambona na Nyerere walikutana tena.

Kambona alikuwa tayari kukitumikia chama cha TANU ambacho kilikuwa kimeanzishwa muda si mrefu, lakini Nyerere akasema wasingeweza kumwajiri kwa vile chama kilikuwa hakina fedha.

Kambona akasema chama hakikuwa na fedha kwa vile hakikuwa na ‘organising secretary, na ndipo alipoamua kufanya kazi hiyo ili kujenga chama, bila ya malipo’. Aliishi kwa kutegemea akiba aliyojitunzia kwa kufanya kazi miezi 6.

Katika kipindi hiki Kambona alisafiri sehemu mbalimbali za nchi na kuonana na machifu na wazee wa vijiji ili kusajili wanachama. Katika miezi 6 alifanikiwa kusajili wanachama 10,000, na hadi kufikia mwaka mmoja alikuwa amepata wanachama hai 100,000. Kambona alitumia michango aliyopata kufungua akaunti ya kwanza ya TANU.

alienda Butiama kumshawishi Nyerere achukuwe uongozi wa chama moja kwa moja. Baada ya miaka mitatu Kambona aliamua kwenda kusomea sheria katika Chuo cha Middle Temple, nchini Uingereza mwaka 1957 kwa ufadhili wa Gavana.

Akiwa London Kambona alikuwa kiongozi wa chama cha wanafunzi wa Tanganyika na Mwenyekiti wa tawi la TANU la London. Ni wakati huo ambapo Kambona alipata fursa ya kukutana kwa mara ya kwanza na watu mashuhuri kama George Padmore, mwanaharakati wa umoja wa Afrika, ambaye alimshawishi ahudhurie mkutano wa mwaka 1958 wa waafrika wote(All Africa’s Peoples Conference), uliofanyika nchini Ghana muda mfupi baada ya kupata Uhuru.

Akiwa Ghana Kambona alipata nafasi ya kukutana na mwanaharakati mwingine maarufu wa siasa za Afrikla, Kwame Nkurumah. Akiwa uingereza Kambona alikuwa mwaafrika wa kwanza kutangaza taarifa ya habari kwa Kiswahili katika idhaa ya kiswahili ya BBC.

Aliporudi nchini Tanganyika, mwaka 1959, TANU ilikuwa imeshaweka bayana madai yake ya kupewa serikali ya madaraka, vinginevyo TANU ilikuwa tayari kuanzisha mapambano kama ilivyokuwa kwa Mau Mau ya Kenya. Wakiwa London wakisubiri kupewa madaraka ya ndani, Nyerere na Kambona walijadili hatua mbalimbali ambazo zingechukuliwa ili kuepuka kutoweka kwa amani.

Wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Londoni 1991, Kambona alikumbuka matukio kama hivi, ‘’Bwana Nyerere alikuwa akiishi nami katika chumba kidogo nilichopewa chuoni.

Tulijadiliana ni namna gani angeweza kurudi nyumani na kuonana na wafuasi wake bila kupewa serikali ya madaraka. Baadae nilifanikiwa kumshauri kuwa wakati atapozungumza na vyombo vya habari katika the East African Arch aseme kuwa walowezi wa kizungu ambao wapo Tanganyika wana hekima zaidi katika kanda ya Afrika Mashariki.

Alikubali kusema hivyo endapo na yeye Kambona angekubali kukatisha masomo yake ya sheria huko London na kurudi Tanganyika ili ampe nguvu na kumuunga mkono katika kikao cha kamati kuu ya TANU wakati akitetea tamko lake la wenye hekima zaidi.

Katika uchaguzi wa kwanza TANU ilishinda viti vyote isipokuwa kimoja. TANU iliunda serikali ya mambo ya ndani chini ya Nyerere ambaye alikuwa Waziri kiongozi wa kwanza.

Na katika harakati hizo za matayarisho ya serikali ya ndani, Kambona alimwoa Flora Moriyo wakati wakiwa kwenye msafara wa harakati za kukamilisha matayarisho ya uhuru na serikali ya Uingereza. Harusi ilifungwa katika kanisa la Mt. Paul, London, na Nyerere ndiye alikuwa msimamizi. Kambona aliteuliwa kuwa waziri wa Elimu.

Baadaye alishika nyadhifa za waziri wa Mambo ya Ndani, Mambo ya nchi za nje na Ulinzi na Tawala za Mikoa. Pia alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa Kamati ya Ukombozi ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika na mwenyekiti wa utayarishaji wa AOU charter.

Mwaka 1964, Kambona alifanya kazi kubwa katika kuunganisha Zanzibar na Tanganyika, akiwa pamoja na Raisi Nyerere, Raisi Karume na Waziri Kiongizi Hanga. Hii ilikuwa ni baada ya mapinduzi ya Zanzibar.

Wakati wa wanajeshi wa kikosi cha Calito walipoasi mwaka 1964 Kambona alikuwa msuluhishi mkuu kati ya serikali na wanajeshi hao. Nyerere na Kawawa walienda mafichoni Kigamboni. Baada ya siku tatu za majadiliano Kambona aliafiki kuongeza kasi ya kuwawezesha waafrika kushika hatamu jeshini.

Katika mahojiano na gazeti la Daily Telegraph la London Kambona alisema, ‘baada ya kuwatuliza wanajeshi nilikwenda kuwatafuta viongozi wengine na kuwarudisha mjini kwa kutumia Land Rover yangu’. Hatimaye maasi hayo yalidhibitiwa kabisa na majeshi ya Uingereza na Nyerere alimsifu Kambona bushara na uaminifu wake.

Tofauti kati ya Nyerere na Kambona zilianza kujitokeza baada ya maasi ya wanajeshi. Nyerere alitaka kuanzisha mfumo wa chama kimoja nchini ili kuimarisha usalama. Kambona alipinga hoja hiyo kwa maelezo kwamba mfumo huo ungezorotesha uhuru wa watu na maendeleo ya demokrasia.

Hata hivyo, Kambona alishindwa bungeni; alikataa kusaini muswada (bill). Mwaka 1967, baada ya safari ya China ya mwaka 1965, Nyerere akiwa amependezwa na mfumo wa kikomonist wa Mao, alitaka kuanzisha mfumo kama huo kwa jina la ujamaa.

Dhana ya msingi ya mfumo wa ujamaa ilikuwa ni kuwahamishia watu katika vijiji vya ujamaa na kutaifisha viwanda ana mali. Kambona hakukubaliana na utaratibu huo kwa maelezo kwamba ungeongeza umaskini na udhibiti wa serikali kwa watu.

Alijiuzulu kutoka katika serikali na Chama na hatimaye yeye na familia yake walikimbilia Kenya na kisha Uingereza ambako walipatiwa uhifadhi wa kisiasa. Mara baada ya kuondoka mali za Kambona zilichukuliwa.

Ndugu zake wawili, waliwekwa kizuizini bila ya kufikishwa mahakamani na kufungwa kwa zaidi ya miaka kumi. Wanafamilia wengine walinyanyaswa na kuwekwa kizuizini. Wengine kati yao walibambikiziwa kesi za uhaini, wakafikishwa mahakamani na kisha kufungwa na serikali.

Kati yao walikuwa Bibi Titi ambaye alipigania uhuru pamoja ana Nyerere na alikuwa kiongozi wa jumuia ya kina mama. Alikuwepo pia Michael Kamaliza ambaye alikuwa mwanaharakati wa chama cha wafanyakazi, mwanachama wa TANU na waziri.

Wengine ni pamoja na Gray Mattaka, John ana Eliya Chipaka na Prisca Chiombola. Kambona alituhumiwa kuwa kiongozi wa wahaini wakati akiwa London na alihukumiwa bila kuwapo. Watuhumiwa hatimaye walikata rufaa katika mahakama kuu ya Afrika Mashariki na wakaachiwa huru.

Hata hivyo, baadae walikamatwa na serikali na kufungwa tena. Kambona alituhumiwa kuwa aliiba pesa nyingi sana zikiwa ni mali ya umma, kitu ambacho Kambona alikataa katika taarifa yake na waandishi wa habari Septemba 6 huko London 1967.

Tuhuma hizo zilisema kuwa ‘’ Kambona amekutwa na pesa nyingi sana kama karanga alipopekuliwa katika Uwanja wa ndege Embakasi Nairobi’’ Hata hivyo Kambona katika taarifa yake kwa waandishi wa habari alikanusha kuhusika na tuhuma hizi na badala yake akaipa serikali ya Tanzania kuiomba serikali ya Kenya kutoa ukweli juu ya jambo hilo- jambo halikufanyika.

Akiwa Londoni Kambona aliishi maisha ya shida na dhiki. Katika mwaka 1982 ndugu zake Kambona na Otini Kambona walifunguliwa kutoka kizuizini baada ya juhudi za waziri mkuu wa New Zealand Robert Muldoon. Katika mwaka 1990 Kambona akiwa na matumaini makubwa ya mabadiliko ya kisiasa katika Tanzania hususani mabadiliko ya demokrasia, aliunda chama kiitwacho Tanzania Democratic Alliance.

Wakati vyama vingi vilipoanzishwa Tanzania 1992 Kambona aliomba kurudi Tanzania. Serikali ya Tanzania ilimkatalia katakata na kudai kuwa Kambona hakuwa Mtanzania. Kambona badala yake aliomba Serikali ya Uingereza kumpa pasi ya kusafiria kurudi Tanzania. Hata hivyo Serikali ya Tanzania ilitamka kwamba pamoja na kupata pasi hiyo itamweka ndani pindi atakapoingia Tanzania.

Pamoja na msimamo huo wa Serikali, Kambona alitua kwenye ardhi ya Tanzania tarehe 5 september 1992. Hakuna mamlaka iliyomkamata bwana Kambona bali alipewa miezi mitatu awe amekamilisha utata wa uraia wake. Baada ya kurudi, Tanzania aliona kuwa harakati za kuelekea kwenye demokrasia ya kweli zilikuwa zikienda kwa mwendo wa kinyonga.

Hata hivyo Kambona hakuweza kujihusisha kwa kiasi kikubwa na siasa kutokana na matatizo ya kiafya hususani shinikizo la damu. Hatimaye Oscar Kambona alifariki akiwa katika matibabu mjini London mwezi Juni 1997.

Mdogo wake Otini Kambona naye alifariki katika kipindi hichohicho kutokana na magonjwa ya moyo. Wote wawili walizikwa Tanzania, na serikali ya Tanzania iligharimia gharama zote za usafirishaji miili ya marehemu ndugu hawa.

Oscar Kambona ameacha mke na watoto wawili. Mtoto wao wa kwanza Mosi Kambona aliuawa mjini London katika mazingira ya kutatanisha. Roho ya Oscar Kambona na ndugu na jamaa wote waliotangulia MWENYEZI MUNGU aziweke pema peponi, Amin.

Kumsoma bonyeza hapa
 
Ngoja nitoe kumbukumbu yangu, it may have holes.

Inasemekana kuwa Kambona alikuwa rafiki mkubwa sana wa Nyerere aliyekuwa bestman kwenye harusi yake iliyofanyika London. Katika serikali za kwanza kwanza za Nyerere, Kambona alikuwa ni Waziri mwandamizi aliyekuwa an sauti kuliko mawaziri wengin wote, isipokuwa labda Kawawa. Wakati wa maasi ya 1964, inasemekana pia kuwa ni Kambona na Okello ndio walioongea na kuwatuliza askari waasi. Vile vile katika zile siku 100 za kuelekea Muungano, Nyerere alisikiliza sana ushauri wa Kambona kuliko mtu yeyote kuhuhusu umuhimu wa muungano na structure yake.

Hata hivyo baadaye uhusiano kati ya Kambona na Nyerere ulianza kuwa mbaya hasa pale Kambona alipoanza kujenga majumba mengi ya kupangisha Dar kwa haraka haraka huku akiwa waziri, jambo ambalo halikuwa tamu kwa Nyerere. Halafu wakati Nyerere anaandika Azimio la Arusha, Kambona alijitokeza kumpinga Nyerere directly kutokana na ile miiko ya uongozi ambayo ilikuwa inaingiliana na zile nyumba alizokuwa amejenga hapo Dar.

Kwa vile mwishoni lile Azimio la Arusha lilipita na kuanza kutaifisha majumba ya kupangisha yakiwemo na yale ya kambona, basi Kambona akasuka mpango wa kumpindua Nyerere kusudi kusimamisha hiyo operation ya Azimio la Arusha. Waliohusika katika mpango walikuwa wengi sana ikiwa ni pamoja na Titi Mohammed, Lifa Chipaka, Kamaliza, na wengineo. Sielewi mpango wenyewe ulivujaje, lakini wahusika wote walishikwa na kuswekwa kwenye gereza la Keko. Kutokana na umaarufu wake, Kambona alisaidiwa na walinzi wa gereza hilo kutotoroka. Nadhani kwanza alikimbilia Malawi ambako ndiko alikoondokea kwenda kuishi uhamishoni London.

Kitu kimoja binafsi huwa nadhani kuwa Mzee kambona was right kuhusu vipengele kadhaa vya Azimio la Arusha, hasa ule utaifishaji wa njia kuu zote za uchumi. Hata hivyo kwenye miiko ya uongozi nadhani vile vile alikuwa kakosea. Kilichotakiwa ni kuwa kuandika upya miiko hiyo huku ikiheshimu mali alizokuwa nazo mtu kabla ya kuwa kiongozi.
 
Katika mahojiano na gazeti la new africa huko nyuma Nyerere aliulizwa ikiwa kuvunjika kwa urafiki wake na Kambona ni moja ya mambo yanayomkosesha raha ktk utawala wake,Nyerere alisema hapana na alimshangaa Kambona kama katibu wa TANU alihusika katika maandalizi yote ya azimio la arusha hata kabla halijatangazwa na mwishoni akabadilika kulikana. Kilichomsikitisha Nyerere ni kuwapigia magoti waingereza waliokuwa wakoloni wetu waje wamwokoe wakati wa maasi ya jeshi,wakati tulijidai tunaweza kujitawala.

Toafauti kati ya hawa ni attitude towards money/richness and how to get it.

Nyerere alifuata msimamo wa biblia na wa kikomunisti,kuwa ni ngumu kwa tajiri kuingia ktk ufalme wa Mungu,huwezi kuwa tajiri pasipo kutumia nguvu ya watu wengine hivyo kwa kuwa tajiri umenyonya wengine(marxism),pia maneno ya mtakatifu mmoja kuwa unapompa maskini shati humsaidii bali unampa haki yake! Kambona nafikiri hakuona vibaya mtu kutumia akili na nguvu zake kuchuma mali.

Je historia ya sasa tz tunaweza kuwahukumu vipi hawa waasisi wa taifa letu?mawazo ya yupi yameonyesha ku hold?

Baada ya kuvunjwa azimio la arusha tumejionea na tunaendelea kuona na kujadili viongozi wetu wanavyofuja mali na kuliibia taifa, rushwa, nepotism, etc.

Nakubaliana na mawazo hapo juu kuwa implementation ya azimio ilienda haraka sana kabla hatujawa na skilled personnel ya ku takeover na kuendesha taasisi mbali mbali.

For me Nyerere was right and had the right intention to selfishlessly serve the poor people of tz and lived to his words until his death.
 
Mzee Kichuguu asante for brief,

Unajua huwa sometimes na regret kumezeshwa zile nyimbo za nursery ...Kambona ha ha! wivu ulimshinda shauri ya mapesaaa! But kambona in some extent naona alikua sahihi kupinga mpango wa azimio la Arusha.Hata Nyerere mwenyewe nadhani alikuja kugundua kosa.

ONA LEO MAMBO YA UJAMAA YALIVYO KIMYA KIMYA
 
Kwenye uendeshaji wa uchumi nadhani he was right; tatizo lake moja tu ni kuwa alikuwa anataka utajiri na akashindwa kujenga hoja ya namna ya kutunza mali za viongozi waliopo madarakani wanazopata kihalali bila kutumia madaraka yao.

Kwa mfano nyumba ya kupandisha ambamo wamepanga raia wa kawaida haina uhusiano wowote na madaraka ya kiongozi, kulikuwa hakuna haja ya kuitaifisha.
 
Kuna kitu kingine pia. Kabla hajahamia London, na labda baada ya uhusiano na mwalimu kuanza kuyumba, Kambona alimwambia mwalimu kuwa hali yake ya afya haikuwa nzuri.

Mwalimu alimwelekeza Kambona kwenda kutibiwa uholanzi ambako kulikuwa na daktari aliyekuwa rafiki yake mwalimu. Kambona alikaa uholanzi kwa matibabu kwa zaidi ya mwezi. Aliporudi nyumbani, kwa mashangao wa mwalimu, Kambona alijiuzulu uwaziri na ukatibu mkuu wa TANU.

Ingawa alitaja sababu za kiafya kama sababu za kujiuzulu kwake, bado hazikumconvice mwalimu hivyo ukapangwa mpango wa kumkamata. Sijui ni vipi aligundua mapema na hivyo kuponyoka mapema hadi Nairobi alikopandia ndege kwenda London. Inawezekana pia kuwa hakuridhika na nafasi aliyokuwa nayo. Wakati anaondoka kwenda kwenye matibabu alikuwa waziri wa maendeleo vijijini baada ya azimio la Arusha.

Inawezekana pia kuwa uhamisho wa kumpeleka kwenye wizara hiyo ilikuwa kumkomoa.
 
Mzee G,

Kambona alipokuwa anatoroka kuelekea London, alikamatwa pale Nairobi Airport na askari wa Kenya, akiwa na masanduku mengi ya dola cash, Kenyatta allipompigia Mwalimu simu on whta to do na Kambona, bado akiwa chini ya ulinzi pale Airport, Mwalimu alimjibu kuwa wamuchie aendelee na safari yake,

ukweli ni kwamba Mwalimu alikuwa happy kuondoka kwa Kambona, ili ampromote Kawawa, ambaye alikuwa yes man!, as opposed na Kambona aliyekuwa objective!
 
Nilisoma article moja ya Letters to the Editor iliyondikwa na Oscar Kambona kwenye gazeti la Africa Now kufuatia yale mahojiano kati ya Peter Enahoro na Nyerere aliyoongelea Majige hapo juu; Kambona alisema aliswekwa ndani pale Keko Maximum Security Prison, ila alisaidiwa na walinzi wa pale kutoroka. Na kuwa alitoroka kwa roli la mizigo hadi nchi ya jirani ambayo sina uhakika kati ya Kenya na Malawi lakini nadhani alikuwa amesema alitorokea Malawi. Gazeti hilo lilikuwa Africa Now toleo la 32, December 1983.

Naona account hiyo siyo kama ilivyorekodiwa na wengi, kwa mfano kitabu hiki. Maelezo ya Gagnija na Mzee ES hapo juu naona ndiyo sahihi zaidi. Nimesoma article nyingine Journal of African Studies inaonyesha likiwa linapinga madai fulani ya Oscar Kambona katika hiyo barua aliyoandika Africa Now. Mwandishi (sikumbuki jina lake ila nitalitafuta tena kurekebisa post hii) ansema kuwa Kambona alikuwa akidai kuwa alisweka ndani na Nyerere ili kupata symphasizers lakini siyo kweli kuwa aliswekwa ndani.
 
Kambona alikuwa mwongo. Tena alikuwa mtu wa wivu sana. Hakuwapenda Kawawa na Jamal, na mpaka sasa sababu zake sijui. Lakini sababu kubwa ya Mwalimu kumwambia Kenyatta amwachie ni kwamba hakutaka kumfanya Kambona "a hero" kwa kumweka ndani.

Baada ya kuondoka Mwalimu aliwang'oa polepole watu wake aliokuwa amewapachika katika idara ya usalama wa taifa na jeshini. Kwa hiyo historically it was a good move.
 
Mzee Jasusi,

Ninakuaminia kwenye hizi kind of ishus, ninaamini kabisa kuwa unayosema ndio ukweli wenyewe kuhsu Kambona, ingawa mpaka leo sielewi kwa nini Mwalimu, alimruhusu huyu Mnyasa kubanda chati, over wabongo, bado sijaelewa!

Maana ukilifuatialia kwa makini ishu lake, utaona jamaa hakuwa na uchungu kabisaa na bongo, halafu vipi kuhusu mtoto wake mmoja anayesadikiwa kuwa ni shoga, aliyepigwa risasi huko majuu, kuna ka-"tetesi" kuwa someone kutoka kunyumba alihusika ili kumkomoa Kambona ni kweli?
 
Jasusi,

Nakubaliana nawe kuwa Kambona alikuwa mtu mwenye wivu sana. Kama nilivyoeleza mapema, kitendo cha kumhamishia wizara ya maendeleo vijijini ndicho kilichomletea ugonjwa uliompeleka kutibiwa uholanzi kwa zaidi ya mwezi. Mwalimu aliwahi kulalamikia tabia hiyo ya wivu. Lakini ni kweli pia kuwa baada ya Kambona kuachia uwaziri na ukatibu wa chama, mwalimu alipata mshituko na akawa amemwandalia nafasi pale Keko.

Kwamba alitoroka baada ya kuona watu wake wanakamatwa mmoja baada ya mwingine inanipa tatizo kidogo. Nijuavyo, watu wake walikuja kukamatwa Kambona akiwa amehamia Uingereza alipojaribu kupanga kuiangusha serikali. Nafikiri kwa jinsi alivyokuwa maarufu, alikuwa na watu waliomtaarifu mapem juu ya mpango wa kumweka keko hivyo akawahi kuponyoka.

Ni kweli pia kuwa kumkamata pale Nairobi kungemfanya hero, lakini ni kwa nini mwalimu alimruhusu aende na hayo masanduku yaliyosheheni dola?
 
Gagnija,

Kweli kuna maswali mengi ambayo hatuna majibu yake ya uhakika. Kambona aliwahi kuwa waziri wa ulinzi.

Alichofanya wakati huo aliweka watu wake katika nafasi muhimu jeshini na vile vile katika Usalama wa Taifa. Mzee ES, wakati wa harakati za kupigania uhuru, Mwalimu alikuwa anahitaji msaada wa kila mtu. Kambona, Kawawa, Shaba, Bomani, Eliufoo, you name them. Kuunda huu utanzania usio na misingi ya kikabila ilikuwa kazi kweli kweli.

Na hapo ndio tunapaswa kuwashukuru wazee wetu wa TANU.

Kambona alikuwa na personal ambitions, na nina hakika kama Mwalimu angemwachia madaraka aliyomwachia Kawawa ya uwaziri mkuu kwa mwaka mzima, Mwalimu asingerudi kama rais mwaka 1962. Hiyo ya kumwachia aende London nadhani Mwalimu alimwona less a threat outside the country than inside.

Kumbuka this was only 3 years after the 1964 mutiny. With him outside it would be easy to root out his supporters within the army and the intelligence. Na kweli time came to prove Mwalimu right.
 
Self imposed exile. What alternative do you have when you are being harrased, charges are being concocted against you, and much more. Were his concerns about Ujamaa and one party state right on? Let the debate begin...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…