Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Mwkjj,
Yes, fair assessment, nipo emotional esp pale watu wanapojaribu kuwa "cute" wakti watu wanaongelea vitu serious!!!!.

Inaonekana kwa wewe hapa kila kitu ni routine, kwahiyo mwendo mdundo.......kwa upande wangu its NOT. Hatuoni vitu kwa mtazamo mmoja, lakini mie nime-avoid sana ku-demize ur point of view......lakini wewe na jamaa zako hiyo ndio game yenu na mnazania ni sifa. Sasa sishangai kwani watu kama Mchambuzi waliamua ku-quit au kadampinzani kusimamia anachosimamia.

Kama ni kweli tupo serious na suala la Tanzania basi hii ndio opportunity na watu waache ku-bs!!!!. Hii mada kuwekwa kwenye vibweka tu na wewe kushabikia uamuzi huo tayari inatoa picha kubwa ktk 3-D................well mie naangalia zangu football saa hii, mambo ya Ngoswe haya, LOL.

Nyani Ngabu,
Najikongoja Foxboro, kuona Big Ben anavyokuwa sacked, intercepted na kadhalika. I hope Pats wanakwemda 13-0 jioni hii, itakuwa safi sana!!.
 
Mwanakijiji,
Nakubaliana na wewe. Lakini usije ukadanganywa na tofauti kati ya Dems na Rep; ukianagalia picha kubwa, tofauti zao ni ndogo. Kuna baadhi ya vitu wanatofautiana, lakini hawa wote wawili wamepanda meli moja. Wote ndumilakuwili.

Nimeona ripoti moja inasema kwamba majimbo ya Democratic senators ni tajiri kuliko Rep.
 
fv
Mwanakijiji:



Fani yangu ni uhandisi na formula moja katika uhandisi don't reinvent the wheel. Hivyo sioni sababu ya wasomi wa kiafrika kupoteza muda kufikiri vitu vipya wakati vitu vilishafanyiwa kazi.

Hapo ulipo una vitu bwelele kama TV, telephone, gari, kitanda, chupi mpaka mswaki vinavyotokana na mawazo ya ki-magharibi. Kwanini hutoi subira mpaka pale tutakapotengeza vitu kwa kutumia mawazo yetu.

Wanasema using'ate mkono unaokulisha. Nina uhakika wasomi wetu wangekuja na mambo mazuri tu. Kitu kilichoboronga ni Ujamaa wa Tanzania ulijengwa kwa misingi ya mikopo na misaada. Nyerere aliacha nchi inategemea wafadhiri. Wasomi wetu hawawezi kufanya vitu vyao wakati kuna mtu anayetulisha anataka tu-copy vitu vyake.

Siku zote unawasifu wachina lakini wachina hawakuta upuuzi wa kukopa kutoka benki ya dunia. Mao alipokufa aliacha nchi masikini fulani lakini hakuacha deni. Hivyo waliomfuatia waliweza kuleta mabadiliko yao bila ku-copy sana.

Nyerere pia aliweza kufanya mambo yake kwa sababu wakolomi walimuachia pesa. Lakini wangemuachia deni la kama yeye aliloacha na nchi yenye kutegemea misaada basi ujamaa wake ungeishia vitabuni.
 

Kitu muhimu cha kuelewa ni kuwa kuna njia za uzalishaji za kijamaa na njia za matumizi ya huduma za kijamii za kijamaa.
Vilevile kuna njia za uzalishaji za kibepari na njia za matumizi ya huduma za jamii za kibepari.

Nchi za Scandinavia hazitumii njia za kijamaa kuzalisha. Ujamaa wao huko katika matumizi muhimu ya kijamii.

Ujamaa wa Nyerere, wa kirusi ulitaka uzalishaji uwe wa kijamaa na matumizi ya huduma muhimu yawe pia ya kijamaa. Hapo ndipo mzee mzima aliboronga.
 

Tofauti kubwa kati ya democrats na republicans sio ubepari na ujamaa mamboleo.

Core values ya republicans ni social conservertism and fiscal Conservativism.

Democrats ni social progressive ambayo haina uhusiano wowote na ujamaa. Tajiri kama Bill Gates anaweza kuamini democrats.
 
Bin,
Nice and godbless you!!! I hope majority of us would have the same kind of understanding of the issues as you are!!!! brilliant........ keep it up hommy!!!!
 
Nyerere pia aliweza kufanya mambo yake kwa sababu wakolomi walimuachia pesa. Lakini wangemuachia deni la kama yeye aliloacha na nchi yenye kutegemea misaada basi ujamaa wake ungeishia vitabuni.

Mwalimu, aliacha deni la Dola Billioni saba, Mwinyi akali-double by the time anaondoka likawa Dola Billioni 14, sikui sasa hivi limefikia wapi?
 

Bin Maryam,

Asante kwa maelezo mazuri katika hili. kuna swali moja niliuliza hapo juu kuhusu ubepari ambalo ukilijibu utaona makosa katika maelezo yako hapa.

Swali ni kuwa je kuna nchi yoyote duniani ambayo ubepari ulifanikiwa? Jibu ni kuwa hapana. Ubepari bila ujamaa iliishia kuwa kasheshe, na the same way naona imekuwa katika ujamaa.

hizi sera peke yake hazisimami na Nyerere angechanganya kidogo ubepari basi angekuwa salama.

Issue yako ya ujamaa katika kuzalisha mali umekosea kwa sababu hata nchi kama marekani zimetumia ujamaa katika uzalishaji. kama unaijua marekani vizuri na sera zake kiuchumi je unaweza kuita vifuatavyo uzalishaji wa kibepari?

- Army Corps of engineering
- NASA
- Social Security Adminstration
- Medicare
- Department za ujenzi za States
- Na ile kitu alianzisha Jimmy Carter ya kutafuta mafuta
- Public Transportation za marekani

Ukiangalia wamarekani pamoja na kujiita machampion wa ubepari lakini wametumia ujamaa kuzalisha mali hasa katika vitu muhimu vya nchi kama miundo mbinu (infrastructure).

Ukweli hakuna nchi duniani ambako ubepari peke yake umefanikiwa kama vile ambavyo hakuna nchi yoyote duniani ambako ujamaa peke yake umefanikiwa.
 

NO tofauti ni zaidi ya hii hapa ndugu yangu.

Democrats wa leo wanahitaji zaidi ya social progression. Kumbuka alichoanzisha Jimmy Carter kuhusu alternative energy production? Hii ilikuwa pure socialism ingawa ilipata support ya karibu 80% ya wamarekani.

Kumbuka alichotaka kuanzisha Bill Clinton kwenye health care na Energy policy iliyosimamiwa na Bill Richardson?

Mabepari wengi wametamani na wengine wameingiza sera fulani za kijamaa kama vile wajamaa walivyoingiza ubepari na wakafanikiwa.
 

Wakuu,

Hivi kweli tukiamua kuhusu mafanikio ya nchi kwa kuangalia madeni ya nje mbona marekani itakuwa ndio imekufa kabisa.

Maraisi na Magavana wa Marekani wa miaka 40 iliyopita wamekuwa wanafuata trend ifuatayo. Demokrats wamekuwa wanapunguza deni la nchi huku republican wakiliongeza.

Reagan na Bush Senior waliongeza deni la marekani kwa mkupuo mkubwa sana? Clinton akalipunguza, na sasa Bush junior ndio ameliongeza hadi kwenye paa. Sababu kubwa watakayokuambia wamarekani ni kuwa republicans wanapigana vita na democrats hawapigani. Sijui kama hii pia inaweza kutumiwa kwa Nyerere.

Kama tu kuwa Rais akirithi nchi lazima isiwe na deni ndio afanikiwe? Nchi nyingi duniani zingekuwa na matatizo leo hii.
 
Mwafrika,
Safi na ndio maana hilo deni la Marekani hasa kwa China linawafanyia kitu mbaya!!!. Bottomline ni kuwa madeni ni mabaya na hakuna kinacho justify kuwepo na deni.

Greenspan, kwenye kitabu chake kipya kazungumzia lakini bado ni vague kuelewa kwa kina.............sisi ni masikini, Nyerere alitumia $$$ 500 Mil kupigna Uganda na deni mpaka leo linatutoa kamasi. Hivi China wanadaiwa na nani??.
 

Ni kweli kabisa YNIM,

Sina record nzuri ya china lakini ninavyojua mimi hakuna nchi yoyote duniani (serikali) ambayo haidaiwi - na wadeni wa ndani au wa nje. Kutokana maelezo yako na ya kitabu cha Greenspan, sio kweli kuwa suala la madeni ni issue ya ubepari au ujamaa.

Kama ni hivyo China ingekuwa inadaiwa zaidi ya Marekani au rais wa nchi anapokuwa Demokrat basi deni la marekani lingekuwa linaenda juu. Hii point ya madeni wakuu Bin Maryam na FMES watakuwa wanakosea wakiifanya kuwa ilisababishwa na ujamaa au sera za Nyerere pekee.
 

Mwanakijiji,

Ingawa nina tafsiri tofauti kidogo ya democrats na republicans kwenye light ya ubepari na ujamaa lakini hiyo paragraph ya mwisho inabidi iwe ndio msingi wa hoja zako.

Tatizo ni kuwa hii mada ilianza kwa kumtafutia Kambona nafasi yake katika historia ya Tanzania kabla haijabadilika haraka na kuwa ugomvi na ushindani kati ya Nyerere na Kambona. Kilichofuata ni utoto na mengine ya ajabu lakini sumu imebaki hapa kuwa ugomvi kati ya wanaomuunga mkono Nyerere na wanaompinga Nyerere. Chochote unachoandika kinahesabika tu kuwa utetezi wa Nyerere na chochote wanaopingana nawe wanachoandika kinaonekana tu kama kumpondea Nyerere.

Kama unaunga mkono sera nzuri za Nyerere (na sio tu kufuata ujamaa au alichosema mwalimu) ni vizuri kuangalia ni kitu gani kizuri kinaweza kuchukuliwa katika nia na mitizamo ya Nyerere. Hii pia iwe kwa wanaompinga Nyerere (au wale wafuasi wa sera za kibepari) ambao wanaweza kuacha mabaya yote ya Nyerere na kuunda sera nzuri yenye mafanikio kwa watanzani (kama ilivyoanza azimio la zanzibar mwanzoni mwa miaka ya tisini).

Mabepari walikuwa na akili kwa kufuata sera za kijamaa kwa usiri wakitumia cover ya dini na jeshi. Wajamaa pia waliofanikiwa walitumia sera za kibepari kwa siri na wazi na wakafaniwa. Tanzania pia ambayo ilianza kuachana na ujamaa mwaka 1984 leo hii inaweza kuwa mbali sana kiuchumi kama viongozi wa leo hii wakiacha ubinafsi na wakiamua kuwa responsible badala ya kutoa visingizio vingi kwa matatizo ya nchi na kushindwa kwao.
 
Mwafrika,
Hiyo ishu kwamba wakolonia walimuachia Nyerere pesa nyingi sio kweli. Angalia "Three Year Plan" na "Five Year Plan" mara baada ya uhuru. Nyerere alihaha kupata funding kwa ajili ya hiyo mipango. Mwingereza alikuwa anampa masharti, Wamerikani na Wajerumani pia walikuwa wanatoa masharti kabla ya kutoa pesa.

Hiyo miaka 40 ya Mwingereza walituacha na engineer 2 na madaktari 12, wakati asilimia 85 walikuwa hawawezi kusoma na kuandika.

How can you develop a country in 25 years if you start with 2 engineers, 12 doctors, and 15 percent of the population unable to read and write? Jamani watu wanafanya mchezo.
 

Mwafrika:

Unapolinganisha deni la nchi ni lazima vile vile uchukue per capital income. Hivyo marekani kwa kutumia asset zao, ongezeko la tax wanalipa deni kwa ulaini.

Reginal Mengi ana deni kubwa lakini asset zake na kipato chake zinaruhusu yeye kuwa na deni hilo.

Deni la Tanzania sio kubwa sana na sio la kutisha. Kinachosumbua ni mapato yasioweza kulipa deni lenyewe.

Vile vile nchi nyingi zinaweka akiba zake katika dollar ya kimarekani. Hivyo mmarekani anapolipa deni lake la nje analipa kwa pesa yake ya nyumbani.

Tanzania deni letu kubwa (80%) lilikuwa deni la nje. Hatuwezi kutumia pesa za kwetu kulipa deni hilo.
 

Unajua kwa sababu umesema kuwa wewe ni Mhandisi kwa hiyo nitajaribu kuwa makini nisijadili hili suala la numbes. Suala ulioanzisha wewe lilikuwa ni kuwa Mwalimu aliachiwa pesa na wakoloni na yeye akaacha deni kwa kiongozi anayefuata na hiyo ndiyo ikawa tatizo kwa viongozi waliofuata.

Hoja yako ilikuwa kwamba kama Nyerere asingeacha deni (bila kujali hayo ya per capital income na assets) basi nchi ingekuwa bora zaidi leo hii. Hili sio kweli, at one time nchi nyingi na biashara nyingi zinakuwa na madeni (ndio sababu kuna venture capitalists wa kutoa mitaji) na hizo nchi zinatumia hiyo mikopo kujenga assets na kuinua per capita income. Kwa hiyo tatizo hapa halikuwa numbers bali dhana ya deni la Tanzania aliloacho Nyerere

Issue ya madeni ya Tanzania haina uhusiano wa pekee na ujamaa au ubepari na ninaamini hata wewe unaelewa hili.
 

Asante Maswali,

Unajua hii mada imekuwa kubwa sana kiasi kwamba ni kazi kuwa na kitu specific cha kujadili moja kwa moja. Kinachogomba hapa sijui tena kama ni uwezo wa Kambona au ubovu wa Nyerere.

Sina data kuhusu wasomi waliokuwepo Tanzania mwaka 1961 ila kama hizo ndizo namba basi kuna mengi sana ya kusema kuhusu kufanikiwa au kushindwa kwa uchumi wa Tanzania.

kitu kimoja ninajua kwa hakika ni kuwa, hakuna nchi duniani ambayo ubepari au ujamaa peke yake umefanikiwa. Nchi zote duniani zimechanganya ubepari na ujamaa zikafanikiwa. Kama nyerere angependa kuwa mwizi wa mali ya watanzania, angeidhinisha ubepari kiaina ili amiliki migodi kama Mwanafunzi wake Mkapa na kisha historia ingepima mafanikio yake pia.
 

Kijana unaongopa:

Sipendi wakoloni lakini walikuwa productive na waliacha uchumi mzuri. Na sehemu ya pato la taifa lililotumika kulipa deni lilikuwa kama vile hakuna. Na walijenga uchumi kwa kutumia sekta ya kilimo tu.

Masharti ya mikopo inatolewa kwa kufuata RISK FACTORS ya projects unazofanya. Pesa za mikopo hazitolewi kama vile unakwenda Vingunguti kununua mbuzi.

Project za Nyerere zilikuwa na RISK FACTORS kubwa ya kutofanikiwa.

Na kuhusu idadi ya ma-injinia na madaktari sio kweli waliacha ma-injinia 2 na madaktari 12. Hizo ni siasa tu za uzalendo. Idadi hiyo ni ya wazawa. Lakini aliacha wataalamu zaidi ya hao.

Workforce ya wataalamu ya Marekani inajumlisha wazawa na wageni. Hivyo ni upuuzi kutoa takwimu zinazoondoa wataalamu wasio wazawa.

Hivi mashirika kama ya reli, posta, meli, ujenzi yangeendeshwa vipi kama kulikuwa na injinia wawili tu. Uhuru hauna maana kuwa kila kitu tukifanye sisi.
 
Inapendeza, ndio maana huu si udaku...........watu makini ktk mada makini, dunia inawekwa kwenye finger tips...beatifully.
 

Mkuu hiyo statement ya kuongopa ni kali sana ila naona inakurudia wewe maana umesema kuwa ameongopa bila kutoa "ukweli" ili kuhakikisha vingine (prove otherwise).

Kwa kushindwa kutoa namba tofauti, inaonekana ni kweli kuwa nchi ilikuwa na wazawa 2, 12, 15% kama alivyosema Maswali hapo juu na hii ni big deal sana kwa nchi inayotaka kuendelea. Je wakati Nyerere akistaafu hiyo number ilikuwa imefikia wapi? (yaani kulikuwa na mainjinia na madakitari wazawa wangapi? na 15% ilikuwa imefikia ngapi?).

Bado nakusubiri upinge au ukubali hoja kuwa hakuna nchi duniani iliyotumia ubepari pekee au ujamaa pekee katika kuleta maendeleo na pia ujibu kama NASA nk ni uzalishaji wa kibepari au kijamaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…