1. mzee historia inategemea nani anaisimulia... mzee mambo yote yaliyosemwa hapo yametokana na simulizi. Sasa kabla hatujaanza kuruka ruka kuwa we found "it" ni vizuri kujiuliza.
a. Msimulizi ana lengo lolote jingine la kutusimulia anachotusimulia? b. Msimulizi anahusika vipi katika kisa anachosimulia (is he a hero or the anti hero "villain")?
c. Je, msimulizi ananufaika vipi na masimulizi anayoyasimulia?
d. Katika kisa cha historia je kuna watu wengine wanaoweza kutupa masimulizi yanayolingana na msimulizi huyo na watu hao wako huru kiasi gani?
2. lakini kwa wasomi we need outside source.
3. Je, Kawawa ni reliable source wa matukio ya awali ya historia yetu..?
Mkuu Heshima mbele, basically historia duniani huandikwa na walioko kwenye power, Mwalimu na kina Kawawa, wameandika ya kutosha kuhusiana na ishu ya Kambona, toka tukiwa watoto, sasa hii ni kwa mara ya kwanza tunapata story kutoka the other side, binafsi sihitaji kuambiwa anymore kuhusu Kambona, maana nimeiamba toka primary school jinsi alivyokuwa malaya na kukimbilia Uk, secondary, JKT, vyuoni nimeimba vya kutosha story ya Kambona kutoka kwa side ya Mwalimu,
Nimekutana na viongozi wengi waliosoma na Kambona, kama kina Lusinde, Marehemu Kanyama, Hashim Mbita, Nyirenda, nimeongea na waliofanya kazi naye kwenye siasa, imetosha, yanayosemwa sasa ndio hasa ya upande wake, Mwalimu pia aliwahi kusema baadhi yake, kama vile Kambona kuondoka na masanduku ya pesa nyingi sana alizokamtwa nazo Nairobi, airport, na akasema kuwa askari wa Kenya walipomuuliza what to do na Kambona, Mwalimu akaawambia kuwa wamuachie aende zake, sasa leo tunaambiwa kuwa ulikuwa ni uongo maana na yeye aliwataka serikali watoe ushidhi toka kwa askari wa Kenya, lakini hakuna kitu,
Sasa cha muhimu hapa kwenye ishu kama hizi ni kukubaliana kutokubaliaana, maana ya kumsubiri Kawawa eti aje aweke hii habari sawa hayo mimi simo, the main point yako kama ninakuelewa ni the motive za waanaoandika hizi story, which is great argument ila unachosahau ni kuwa it works both ways, yaani upande wa Kambona na Mwalimu!
Otherwise, I am enjoying this yaani to the bottom of my soul!