kityege Immanuel
Member
- Dec 24, 2016
- 50
- 19
Daaah bonge LA story kwel
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu Maalim Muhammed Said, mimi nilipenda kusoma hadithi toka mtoto na mpaka leo bado napenda hadithi, kwa vile uwezo wa kusimulia hadithi ni kipaji na sii wengi wenye kipaji hicho, nakiri kipaji unacho na nafurahia sana simulizi zako kama hadithi nyingine zozote.Paskali,
Ukisoma Nyaraka za Sykes kichwaa kitakuuma na utapigwa na bumbuzi kubwa
wakati mwingine kujiuliza hivi haya ninayosoma ni kweli?
Lakini ni kweli kwa kuwa ndiyo hizo nyaraka unazo mkononi unaziona, umezishika
na unazisoma.
Abdul anasema yeye kamuona baba yake na rafiki zake wakijenga ofisi ya African
Association New Street na Kariakoo Street akiwa mtoto mdogo.
Abdul anaongeza anasema baba yake alimwambia kuwa aliyekuwa anawawakilisha
Waafrika katika Legico miaka ya 1920 alikuwa Padri kutoka Misheni ya Minaki akiitwa
Father Gibbons.
Father Gibbons ndiye huyo hapo chini kwenye picha wa kwanza kushoto wa pili kulia
ni Chief Thomas Marealle na huyo mama wa kwanza waliokaa ni mke wa Chief
Marealle:
![]()
Unaendelea kupitia hizi nyaraka unakutana na barua ''handwriiten,'' za Chief Marealle
anaandikiana na Ally Sykes kuhusu harakati na uongozi wa Tanganyika itakapokuwa
huru.
Chief Marealle anaeleza fikra zake kuhusu Mwalimu Nyerere kama kiongozi na TANU
kama chama.
Ikiwa mtu hataki kuisikia historia hii basi lazima atakuwa ana lake jambo.
Pascal,Mkuu Maalim Muhammed Said, mimi nilipenda kusoma hadithi toka mtoto na mpaka leo bado napenda hadithi, kwa vile uwezo wa kusimulia hadithi ni kipaji na sii wengi wenye kipaji hicho, nakiri kipaji unacho na nafurahia sana simulizi zako kama hadithi nyingine zozote.
Hizo nyaraka. ..
Nitaendelea
MkuuPascal,
Mhariri wa kitabu mama mmoja wa Kiingereza alipomaliza kuhariri kitabu
cha Abdul Sykes alimpa, ''note,'' mhariri anifikishie salamu zake kwangu.
Yule mama alisema kuwa alikuwa anaona raha sana kuhariri kitabu changu.
Akamaliza kwa kuse kuwa, ''Mohamed you are a story teller...''
Mimi pia toka utoto ni msomaji sana wa vitabu na naamini hii style yangu
ya kuandika ambayo wengi wanaipenda ni kutokana na kuwaiga waandishi
kama Irving Wallace.
Hizo nyaraka...
Hakika nyaraka.
Waandishi wa historia ya TANU hawakupewa nyaraka hizi bali Hassan Upeka
aliwaonyesha ''notes,'' za mahojiano yake na Abdul Sykes kuhusu historia
ya uhuru.
Walizikataa.
Hakika nyaraka:
Mohamed Said: NYARAKA ZA SYKES KATIKA KAVAZI LA MWALIMU NYERERE
NYARAKA ZA SYKES KATIKA KAVAZI LA MWALIMU NYERERE
Mohamed Said September 29, 2016 0
![]()
Nyaraka kutoka kwa Kavazi la Mwalimu Nyerere ikionesha nyaraka kutoka jalada za Ally Sykes
Angalia uongozi wa TAA 1953 pamoja na Mwalimu Nyerere yuko Abdulwahid Sykes, Dome Budohi,
John Rupia, Dossa Aziz na Ally Sykes
![]()
Kushoto: Dossa Aziz, Julius Nyerere, Abdulwahid Sykes na Lawi Sijaona
Arnautoglo Hall 1957
![]()
Kulia: Zuberi Mtemvu, Julius Nyerere na John Rupia
Waliosimama nyuma ni Bantu Group wa pili kulia waliosimama ni Ali Msham
picha hii ilipigwa nyumbani kwake Magomeni Mapipa ambako alifungua tawi TANU, 1955
...Ally Sykes aliniruhusu nisome majalada yake binafsi, barua zake, shajara na kumbukumbu nyinginezo za ukoo wa Sykes. Ally Sykes alinifahamisha kuwa kumbukumbu hizi zilikuwa ndani ya sefu ambayo haikupatwa kufunguliwa kwa zaidi ya miaka therathini. Nikiyapitia majalada yake nilishangazwa na utaratibu wa Ally Sykes wa kupanga kila kitu na kila kipande cha habari mahali pake hata kingekuwa kidogo namna gani wakati ule wa harakati. Ally Sykes ana barua ya mwaka 1954 iliyoandikwa kwa penseli toka kwa Zuberi Mtemvu kwenda kwake akimtaarifu juu ya mazungumzo aliyokuwanayo (Mtemvu) na Nyerere kuhusu yeye na TANU; stakabadhi ya hundi ya posta toka kwa Ally Sykes kwenda kwa Japhet Kirilo wakati wa Mgogoro wa Ardhi ya Wameru; nakala ya barua isiyokuwa na tarehe kutoka TAA kwenda kwa Malkia Elizabeth iliyotiwa saini na viongozi wote wa TAA: Rais Julius Nyerere, Makamu wa Rais Abdulwahid Sykes, Katibu Mkuu Dome Okochi, Naibu Katibu Dossa Aziz, Mweka Hazina John Rupia, Naibu Mweka Hazina Ally Sykes ikimpongeza Malkia kwa kutawazwa; barua ya mwaka 1952 toka kwa Rashid Mfaume Kawawa kutoka Bukoba kwenda kwa Ally Sykes ikimfahamisha juu ya hali ya siasa katika Kanda ya Ziwa; barua ya mwaka 1963 toka kwa Lady Judith Listowel, Kenneth Kaunda, Julius Nyerere, Kasela Bantu, Chifu Thomas Marealle ...orodha haina mwisho. ..
![]()
Kleist Sykes na wanae kulia pembeni yake ni Abbas, nyuma kulia ni Abdulwahid na Ally
![]()
Chief Thomas Marealle
![]()
Kulia: Abdulwahid Kleist Sykes na Ally Kleist Sykes
Burma Infantry Vita Kuu ya Pili
Baadaye nilipofnya utafiti kuhusu maisha ya baba yake, Kleist Sykes, nilikuja kufahamu kwamba tabia hii ilirithiwa kutoka kwa baba yake ambae alikuwa akiweka ndani ya jalada kila kipande cha karatasi kilichokuwa na habari iliyostahili kukumbukwa. Ni jambo la kuhuzunisha kwamba sikuweza kupewa shajara za Abdulwahid ambazo nilielezwa kwamba baadhi ziko katika hati-mkato na hadi leo hazijafasiriwa. Shajara hizi nimezioana kwa macho yangu lakini kwa kukosa idhini sikuweza kuzifungua na kuzisoma. Vilevile vilevile sikuweza kupata kumbukumbu halisi za Vita Kuu ya Kwanza zilizoandikwa na Kleist Sykes kwa mkono wake mwenyewe. Hapana shaka yoyote kwamba nyaraka hizi ni hazina zenye thamani isiyo na mfano wake. Ni matumaini yangu kwamba siku moja nchi yetu itakubali na kuthamini mchango wa Abdulwahid katika taifa la Tanzania na nyaraka hizi kama kielelezo cha harakati dhidi ya ukoloni, zitakubalika na zitawekwa chini ya hifadhi ya Nyaraka za Taifa kwa faida ya vizazi vijavyo.
![]()
Kasella Bantu
![]()
Dome Okochi Budohi
![]()
Kulia ni Dome Okochi Budohi na kushoto ni Mwandishi Ruiru,
Nairobi 1972
Familia yangu ilifahamiana na Dome Budohi, mmoja wa wanaharakati kutoka Kenya. Wakati ule wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika alikuwa akiishi Dar es Salaam. Budohi alikuwa mmoja wa wazalendo walioasisi TANU na kadi yake ya uanachama no. 6 aliyopewa Julai 1954. Mwaka 1955 alikamatwa na serikali ya kikoloni kwa tuhuma ya kuwa mmoja wa askari wa Mau Mau harakati za wazalendo takriban wengi wao wakulima wadogo waliokuwa wakipigana na ukoloni wa Waingereza nchini Kenya. Ninazo kumbukumbu nyingi za utoto nikimtembelea Budohi ndani ya selo yake Kituo Cha Kati cha Polisi. Hivi sasa jengo hilo ni Makao Makuu ya Shirika la Reli la Tanzania.
![]()
Hili jengo mkonno wa kushoto ni Railway Station, jengo la mbele yake ndiyo
ilikuwa Central Police Station wakati wa ukoloni
Wakati huo mimi nilikuwa mtoto, si zaidi ya miaka minne hivi. Jambo la kwanza ninalokumbuka kuhusu Budohi ni kuwa kila mara tulipokwenda kumtembelea tulimkuta anasoma gazeti. Baadae Budohi alihamishiwa Kenya na aliwekwa kizuizini katika kisiwa cha Lamu. Alipofunguliwa toka kizuizini mwaka wa 1963 miezi michache kabla ya uhuru wa Kenya, Budohi alikwenda Uganda na akaajiriwa na gazeti la Uganda Argus. Hivi sasa ninaelewa kwa nini siku zile kila mara nilikuwa namkuta amezama ndani ya gazeti kila tulipokwenda kumtembelea pale rumande mjini Dar es Salaam. Niliweza kwa msaada wa rafiki yake Maxwell aliyelowea Tanganyika, kumpata Budohi mjini Nairobi mwaka 1972. Nilimtembelea mjini Nairobi wakati huo alikuwa akiishi Ruiru maili chache kutoka Nairobi mjini. Budohi alikuwa ametundika picha ya Nat King Cole sebuleni kwake. Mwaka 1974 nilimtembelea tena, safari hii katika nyumba yake ya Ngei Estate. Budohi alikuja kuwa mtu wa kwanza kabisa kunipa habari kuhusu historia ya harakati za Tanganyika dhidi ya ukoloni wa Waingereza. ...
(Kutoka Kitabu Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924 - 1968)...
![]()
Mwandishi na Mzee Maxwell 1997
Ingia hapo chini kwa historia zaidi:
Mohamed Said: NYARAKA ZA SYKES KATIKA KUIFAHAMU HISTORIA YA TANU NA UHURU WA TANGANYIKA 1
Mohamed Said: NYARAKA ZA MOHAMED SAID KATIKA KAVAZI LA MWALIMU NYERERE
Mohamed Said: KUTOKA JF: MAREHEMU HASSAN UPEKA (TANU INTELLIGENCE 1956) NA UANDISHI WA HISTORIA YA TANU
historia
Paskali,Mkuu
Mohamed Said
Ninachoweza kusema kwa sasa ni just asante kwa hii.
kupenda historia ni hobby, lakini uwezo wa kuihifadhi ni kipaji. Wenzetu wanavyofanya ni ku groom watu wa kuwapokea, kama wewe umeandika ulichoandika kwa mapenzi na kipaji, amini nakuambia wewe usipo groom mtu wa kuendeleza ulipoishia, then hizo hati mkato za skykes ni halali ya mchwa tuu!.
Kama Chuo chetu kikuu kimeanzishwa 1961 hadi leo hakuna any literature masterpieces za kweli zilizoandikwa, hadi leo wanafunzi wa literature wanatumia Chinua Achebe, James Ngungi wa Thiongo, Okot P Bitek and the likes!. Historia ya Tanganyika ni ile ya John Ilife! , unategemea nini?.
Kufikia 2020 mimi nitakuwa nimehudumu kwenye fani ya utangazaji kwa miaka 30, nikijitafakari enzi yangu na Kilchopo, nimegundua bado sijapata mtu wa kutembea kwenye viatu vyangu, hivyo sasa nimeamua kurudi kwa muda ili nifanye grooming, by 2020 nitakuwa 50+ hivyo nitastaafu rasmi huku nimefitisha watu kwenye viatu vyangu.
Mimi nimesoma hati mkato, kinachofundishwa ni basic tuu, mastering kila mwandishi hutengeneza personal style ambayo hakuna mtu mwingine yoyote anaweza kusoma unless kama ni muumini wa life after life, then m consult ma clairvoyant wamtafute medium wa after life wa Cleist kisha huyo medium apewe hizo manuscripts, atasoma kila kitu huku unaandika!. Vinginevyo ni ama mchwa, ama bacteria!.
Paskali
HahahaNinakumbuka nyimbo za mchaka mchaka sekondari tuliimba "Kambona ameolewa huko ulaya" propaganda ni kitu kibaya sana.
ShorthandMzee Mohamed Said hati mkato ndio nini?
SaidAlly,Wewe Mohamed Said una busara sana Mzee wangu.
Natamani ningepata nafasi ya kukaa na wewe walau kidogo nijifunze kuhusu hekima na busara kutoka kwako na sio mambo ya dini.
Mwenyezi Mungu akuzidishie yaliyo mema na uhai mrefu walau vijana wa sasa tujifunze toka kwako.
Ningekua muandishi nami ningeandika kitabu kuhusu maisha yako ili kumbukumbu yako pia iwepo kwa wale watakao kuja kutafuta ukweli hapo baadae.
Heshima nyingi kwako Mohamed Said!
Watawara na huu mchezo wa kuwaambia wenzako sio Raia uli anza siku nyingi
Sio kukupamba sana.SaidAlly,
Umenipamba sana.
Ahsante nasshukuru.
Yote sawa ila ujue Kambona alikuwa na mke wa kwanza ambaye alizaa naye mtoto wa kike. Fanya utafiti Flora alikuwa mke wa pili.Oscar Kambona ameacha mke na watoto wawili. Mtoto wao wa kwanza Mosi Kambona aliuawa mjini London katika mazingira ya kutatanisha. Roho ya Oscar Kambona na ndugu na jamaa wote waliotangulia MWENYEZI MUNGU aziweke pema peponi, Amin.