Pia someni katika thread nyingine hapa Jamii Forums, "Kawawa vs Sokoine: A Myth or Reality?," kuhusu Kambona.
Katika mjadala huo, "Kawawa vs Sokoine: A Myth or Reality?," Mdau aliandika yafwatayo:
"Na pia kuna wengine wanasema Mwalimu alikua anapenda sana watu waliokua na utaratibu wa NDIYO MZEE....kumbukeni Kambona alivyoonekana mkorofi...anyway, kila mtu ana mapungufu yake, labda pia level ya elimu ilimfanya hayati kawawa awe mnyenyekevu..."
Nikajibu hivi:
Ebu nielimishe. Pia nisahihishe nikikosea.
Unasema Kawawa alikuwa mnyenyekevu (bila shaka unamaanisha kwa Mwalimu Nyerere) kwa sababu ya elimu yake; nadhani unamaanisha elimu yake ilikuwa ni ndogo.
Swali langu ni hili: Kambona alikuwa na elimu gani? Alimaliza masomo chuoni, katika chuo chochote, na kupata shahada? Shahada gani?
Kabla ya uhuru, aliwahi kuwa mwanafunzi Uingereza na alijaribu kusomea sheria lakini alifeli mitihani.
Pia ukorofi wa Kambona haukumsaidia ikiwa nia yake ilikuwa ni kujionyesha kwamba yeye ni kiongozi shupavu ambaye hamwogopi Mwalimu Nyerere na anaweza kupambana naye.
Angekuwa hivyo, asingetoroka na kukimbilia Uingereza kujificha. Kulikuwa na viongozi maarufu ambao walitofautiana na Mwalimu Nyerere lakini hawakukimbia na kwenda kuishi nchi za nje; viongozi kama akina Chifu Abdallah Said Fundikira, Kasella Bantu, na wengineo.
Hata Kambona aliporudi Tanzania 1992 baada ya kuishi Uingereza tangu Julai 1967, hakuwa na chochote cha kusema. Nakumbuka alipoondoka Tanzania. Nilikuwa secondary school. Nakumbuka pia ilisemekana mtoto wake wa kike wakati ule, waliyekimbilia naye Uingereza, alikuwa na umri wa miaka mitatu. Hakuna haja ya kutaja jina la mtoto huyo kwani anajulikana. Nimemzungumzia hapa kwa kifupi tu kuthibitisha kwamba nilikuwepo nyakati zile.
Aliporudi Tanzania, Kambona aliwaahidi wananchi kwamba atasema ukweli kuhusu Mwalimu na viongozi wengine ambao alidai waliipotosha nchi yetu. Alisema alizijua siri za Mwalimu na za viongozi wengine ambazo atazifichua kwa manufaa ya taifa. "Siri" aliyoifichua ni kusema Nyerere ni Mtusi. Upuuzi mtupu. Kambona alikuwa ni Mnyasa. Haimanishi hakuwa Mtanzania.
Kambona hakusema chochote pale Jangwani kwenye mkutano wa hadhara au mahali pengine baada ya hapo.
Kiongozi kama huyo ni mtu wa kuaminika? Unaweza kumwamini kiongozi kama huyo?
Na usiwalaumu walinzi wa Usalama Wa Taifa kwa nini hakusema chochote muhimu aliporudi Tanzania kuhusu Nyerere na viongozi wengine. Kumbuka kwamba, au ikiwa hujui inabidi ujulishwe kwamba, kabla hajaondoka Uingereza kurudi Tanzania, Kambona alisema hajali chochote. Yuko tayari kukamatwa - potelea mbali. Viongozi wa serikali na Usalama Wa Taifa wawe tayari kumkamata mara tu atakapotua uwanja wa ndege, Dar, wakitaka kufanya hivyo. Wapende, wasipende, anarudi Tanzania.
Alirudi. Hakukamatwa. Aliachwa huru. Lakini hakuenda popote na jitihada yake kuwa kiongozi wa taifa.
Sijui kama alikuwa mtupu kichwani. Ninachokumbuka ni nywele zake, Kambona style, ambazo Watanzania mbali mbali walijaribu kuiga.
Pia inasemekana kwamba Makaburu waliahidi kumsaidia Kambona kabla na baada ya kupindua serikali - angefanikiwa kufanya hivyo. Sijui kama kuna ushahidi kuhusu usaliti huo lakini inasemekana, kutokana na kesi ya uhaini ya 1970:
"The central prosecution witness was Potlako K. Leballo, a founder of the Pan-African Congress (Pan-Africanist Congress) of South Africa (PAC), which had its exile headquarters in Dar es Salaam.
The state maintained that seven defendants attempted to enlist Leballo in the plot but that he informed government officials and only appeared to go along with the plot in order to assist in capturing the conspirators.
Leballo testified that he frequently met with Kambona in London and that Kambona had shown him a cache of $500,000 and told him that he could "get more where that came from" by contacting a U.S. Information Service "friend" in London (New York Times, 19 July 1970, 12).
Leballo further testified that Kambona had an agreement with the South African foreign minister, Hilgard Muller, that South Africa would support the coup." - Colin Legum, ed., "Africa Contemporary Record, 1970 - 1971," pp. 170 - 71. See also Oscar Kambona in Jacqueline Audrey Kalley, Elna Schoeman, Lydia Eve Andor, "Southern African Political History: A Chronology of Key Political Events," page 594.
Sina chuki na Kambona. Alikuwa ni kiongozi wa taifa letu na alipigania uhuru wa nchi yetu, na bara letu, pamoja na viongozi wenzake. Pia alifanya makosa kama binadamu yeyote, pamoja na Mwalimu Nyerere na wenzao. Wote walifanya makosa. Lakini asipewe sifa ambazo hastahili.
Na ninyi mnaomponda Nyerere na Kawawa, na ambao mnafurahia mabadiliko nchini hasa za kiuchumi na kuwa huru kusema na kuandika chochote mnachotaka, kumbukeni tulikotoka kama nchi na taifa hata kama hamkuweko miaka ile kwa sababu mlikuwa bado hamjazaliwa. Someni na waullize waliowatangulia miaka mingi kwa umri.
Kumbukeni kwamba tusingekuwa na nchi yenye umoja na amani bila viongozi kama akina Nyerere na Kawawa au wengine wa aina hiyo na wenye uwezo wao. Pia walilinda taifa letu, na walitunza mali yetu - madini na kadhalika - kwa manufaa yetu.
Baada ya viongozi hao, tunaona nini kimetokea? Nchi yetu imeuzwa na wakombozi wenu wa kisasa na sera zao za kibepari. Viongozi hawa wanaongozwa, wanaamriwa, na wanatawaliwa, na wageni kutoka nchi za nje. Na sisi pia tunatawaliwa, tunakandamizwa, na tunanyonywa, kwa sababu nchi yetu si nchi yetu tena.
Imeuzwa.
Kabla Sekou Toure hajaondoka madarakani na kufariki, aliwaonya wananchi wenzake, "You will miss me."
Wafaransa wamerudi Guinea. Ni nchi yao tena.
Mkuu maelezo mazuri sana ila naomba kuuliza maswali
1. Kuna tuhuma kuwa Kambona aliondoka na fedha kwenda Uingereza, swali langu ni kuwa kwa nini hakupelekwa jela aliporudi? au sheria za Tanzania kuhusu wezi zinabagua kati ya viongozi na raia wa kawaida, kama kweli Kambona alikuwa mwizi alitakiwa akamatwe! period!
2. Kama alitaka kuipindua nchi, kuna watu waliowekwa kizuizini , kwa makosa ya uhaini, vipi KAMBONA kama alihusika na uhaini kwa nini hakupelekwa jela? au hapa tena sheria inabagua kati ya aliyekimbia akarudi na aliyekuwemo nchini?
3. Nimefurahi umefanya evaluation ya Kambona aliporudi! hakuna aibu kubwa ya kihistoria ambayo unaifanya hapa kwa kufikiri kuwa kambona aliyeondoka miaka ile ndiye atakuwa the same miaka ya 90? ilikuwa same generation? Kambona aliyeimbwa na kutukanwa kila kona kuwa ni mhaini na mrudisha maendeleo ya taifa hili, kambona aliyekuwa mocked usiku na mchana na chipukizi, mgambo na JKT!!!!!!!! mkuu unataka kusema nini?
History depicts clearly the difference was only on an open argument! akina Mtei mbona nao waliondoka nchini kwa kutofautiana na Nyerere?
Nyerere atasemwa tu na naomba nikuonee huruma tena na tena acha kufananisha maiti na vilivyo hai, uozo wa sasa hili taifa huwezi ukasema bora ya Nyerere na regime yake vyote havikufaa THE ONLY TIME TANZANIA WAS REAL ni kuanzia mwaka 61-66 kabla ya azimio, wakati tuna vyama vingi na chini inakuwa kwa kasi sana, introduction ya Ujamaa ikaua kabisa maendeleo ya taifa hili, that is history na iko documented!!!!!!
Unless kama unataka facts za each year kutoka mwaka 1967 ni vipi Tanzania ilidumaa kimaendeleo! facts are ready you just dig them.
Issue hapa ni kuwa JKN aheshimiwe kama rais, apewe sifa anapostahili, ila alipokosea atasemwa tena loud and clear you can not stop this, dare not to do that!
In next 50yrs our grandchildren will match and protest jina la Nyerere kufutwa kabisa kama jina la heshima kwenye hili taifa, I SAY SO AND WILL CONTINUE TO SAY: WE BETTER SAY IT NOW AND HAVE GOOD ANSWERS FROM PEOPLE WHO HAVE SEEN NYERERE.
Kwenye Library Nyingi sana in developed countries zimejaa article nyingi negative sana za Nyerere ambazo hauzikuti nyumbani , na hamtaki kuzisikia, na watoto wenu mnawapeleka huko huko ulaya! tuliokuja kibahati tumeziona!
Kusema tulikosea wapi tangu lini imekuwa kosa? Nyerere was only human, mwenye itikadi na urithi wa hulka za kichifu, mpenda watu na mwenye moyo mzuri! leadership is more than having good heart, ukikosea tu mahesabu unafeli!
Ujamaa wa Nyerere na sera zake umetuletea umaskini. we were poor before Mwinyi, na mpaka leo mizizi ile ile inaendelea.
Tell us all what you know about Kambona! sentensi ya JK Nyerere ya 'let him go' kwa mtu ambaye mlikesha naye usiku na mchana kuleta uhuru will never pass without being questioned!!!!!!!!!!!
Furthermore kukosa kiongozi yeyote leo aliyekuwa influnced na Nyerere is big failure kwa leader yoyote duniani! sitaki kuanza somo la saikolojia ya uongozi, something was wrong somewhere mkitaka kuficha ficheni! ila kwa dunia ya sasa i real pity you, mtahamia kusiko na internet ili tu msisikie mabaya ya Nyerere na Mkapa
Kilichompata Nyerere mwaka 66 kabla ya kutangaza azimio ndicho cha kulaumu, vyama vingi alivyofuta JK mwaka 67 ndivyo vimerudishwa mwaka 1992, still we have nothing to debate??? tukisema tunakuwa wabaya??
I will be against anyone atakaye tokea na kumtukana Nyerere, ila atakayesema alikosea wapi yeye na utawala wake sio tusi, leo tunawasema akina Kikwete , Mkapa Mwinyi, Nyerere asisemwe kwa nini ,mtume? malaika? eti alilinda mali zetu na kuleta umoja!!!!!!!!1 hoja dhaifu kabisa hizi, then umoja huu umepungua kwa kiasi gani baada ya wao kuondoka madarakani? kama haujapungua even a dimy, then how can someone draw a mere conclusion kuwa umoja uliletwa na Nyerere?? makabila 130 nani atampiga nani!