Ukweli ni upi "Rais kafanya" au "Serikali imefanya"?

MATAGA wakijadiliana kuwa Rais katoa mabilioni ya hela kwa ajili ya bima ya Afya kwa wote😁😁😁
 
Ukweli Ni kwamba Bunge ndo linatenga fedha za matumizi yote ya serikali, hata zile za maendeleo. Nakumbuka zamani bunge la bajeti lilipokuwa linakaa kuanzia mwezi Juni Hadi Julai. Ikifika tarehe moja Julai Kama bajeti haijapitishwa Basi shughuli za serikali zilisimama Hadi bajeti ikamilike. Rais alikuwa hahusiki, sijui Kama siku hizi Sheria imebadilika!

Sent from my TECNO BC2 using JamiiForums mobile app
 
Mungu ibariki Tanzania
 
Kabla ya muswada kuwa sheria lazima Rais asaini chief
 
Wewe ni jabali la porojo!

Miradi ya maendeleo hupata fedha baada ya kuidhinishwa na bunge. Kazi ya serikali ni kutafuta fedha kwa njia ambazo waziri wa fedha atazipendekeza na kupitishwa na bunge. Hivyo fedha zikipatikana zitapelekwa katika miradi yote iliyoombewa fedha na kuidhinishwa na bunge.

Rais kama kiongozi wa serikali ana wajibu wa kuhakikisha fedha zinazohitajika katika matumizi ya kawaida na maendeleo ya serikali zinapatikana kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopitishwa na bunge. Kwa hiyo ni serikali ambayo hutafuta fedha na kuzitoa. Rais hatoi fedha na wala haitatokea Rais kutoa fedha. Kitendo cha kusema Rais katoa fedha ni kujipendekeza na kijitafutia ujiko kwa Rais kwa lengo la kutafuta uteuzi au kumfumba macho Rais asione maovu yao ambayo yanaweza kupelekea kuondolewa katika nafasi zao za uteuzi!
 
Vipi kuhusu Ilani
 
Futa No.1 weka
UMILIKI WA VYOMBO VYA DOLA NA TUME YA UCHAGUZI.
 
Vipi kuhusu Ilani
Ilani ni ya chama na siyo serikali! Endapo chama kitashinda Uchaguzi hapo kinalazimika kuwasilisha ilani yake bungeni ili itengenezewe mpango wa utekelezaji na bajeti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…