Ukweli ni upi "Rais kafanya" au "Serikali imefanya"?

CHADEMA wanataka useme ni mabeberu yamefanya au wananchi wamefanya, Wanaogopa sana jina Samia
Hii ni kejeli. Jiulize ni motve gani kutaja mtu badala ya serikali.
Tulizoea kusikia serikali ime... Hata kama ni mkuu wa wilaya, waziri au katibu mkuu.
Kuna kujipendekeza kusiko na tija bali kusaka tu kutamblwa na rais, ulafi na unafiki wa kiwango cha juu.
 
Happy Boxing Day kwa hisani ya Mhe Samia Suluhu Hassan
 
Miradi yote iliyoachwa na Hayati Dkt John John Joseph Pombe Magufuli Rais Samia Suluhu Hassan anaitekeleza kwa 100%

Sihiyo tu tayari mingine mipya inaendelea na Ujenzi,

Tunawajibu wa kumwombea Mama huyu,
 
#2025Fever itawapotezea muda wenu bure,hakuna wakumuangusha Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi hizi kubwa na nzuri anazozifanya,

#KAZIIENDELEE NA MAMA
 
Hakika kama mambo yataendelea kuwa hivi Rais Samia Suluhu Hassan atashinda Uchaguzi Huru na Haki wa 2025 kwa zaidi ya 76%
 
" Kwa mwendo huu Tanzania tutafika tunakotaka kwenda tena kwa kuwahi sana, Hongera Mama Samia, Watanzania tuko nyuma yako We chapa kazi achana na Wasio na jema "
 
Ni ujinga kusema Rais kafanya. Ni halali kusema, Serikali imefanya.
 
Maneno haya yanamaana sawa kimantiki " Rais kafanya X " " Serikali imefanya Y " au " " Tumefanya Z " tumia lolote utakuwa sahihi tu.​

Kunabaadhi ya wenzetu wameishiwa hoja hasa huku mitandaoni kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakipinga kwa nguvu zote kutumika kwa sentesi " Rais X kafanya mradi Y".

Watu hawa mara zote wanahoji niwapi huyu Rais X kapata huu ukwasi wa kutekeleza mradi Y? Jambo ambalo kisiasa wanadhani linamuinua zaidi huyu Rais X kwa kupewa endorsement ya mradi "Y".

Wakati wote watu hawa ambao wengi wao ni watu kutoka Upinzani wamependekeza itumike sentesi " Serikali X imetekeleza mradi Y".

UFAFANUZI WANGU
____________________

Kwanza, Kisiasa :
Sote tunafahamu ili tuweze kushinda Uchaguzi wowote ule popote tunahitaji mambo matano makubwa ambayo ni,

1. Mgombea Mzuri

2. Mtandao au Chama

3. Agenda|Ilani ya Uchaguzi

4. Organization au timu kampeni

5. Rasilimali, fedha, vitu na watu

Sasa kwahoja hii naomba tuangazie hitaji la tatu la kushinda Uchaguzi ambalo ni " ILANI YA UCHAGUZI " Ilani ya Uchaguzi inaweza kuwa yakuandikwa au yakutamkwa,

ILANI YA UCHAGUZI maana yake ni ahadi za mgombea au chama kwa Wapigakura au wananchi.
Tuelewane vizuri hapa tumesema Ilani ni ahadi ya mgombea au Chama wala sio ahadi ya Serikali kwa wapigakura au wananchi, nadhani hapa tunakubaliana wote,

Tukubaliane pia huyu mgombea baadae anaweza kushinda na kuwa Rais X, Sasa bila kusahau kuna ahadi aliwaahidi wapigakura wake yeye kama yeye yaani akishinda atafanya miradi X,Y,Z.

Kwaufafanuzi huu wa Ilani ya Uchaguzi kama miradi X,Y,Z ikitekelezwa na aliyekuwa Mgombea wa nafasi X ambae alishinda Uchaguzi huo kwa ahadi hizo na sasa anazitekeleza kama alivyoahidi ubaya unatoka wapi tukisema " Rais X katekeleza miradi X,Y,Z? "

Pili kimuundo :
Rais wa JMT ndio Raia namba moja wa JMT ndie mkuu wa Serikali ndio afisa manunuzi mkuu, ndie mshauri mkuu wa bajeti ndie mtia saini wa mwisho wa sheria ya bajeti unakataaje hajafanya wakati kila kitu kinaanzia na kuishia kwake!!

Tatu, Rais ndie mwenye mamlaka ya kusimamia pesa yote ya nchi kabla na baada ya bajeti kwenye kutekeleza miradi ya nchi kwani ndie aliyepewa dhamana na ndio atakayeulizwa ifikapo mwaka 2025 kulingana na Ilani yake iliyopita hivyo anafanya kwa niaba yetu

Nne, Urais ni taasisi, Sisi sote tuko chini ya Rais wa JMT akiwa kama Raia namba moja wa nchi, Hivyo tuvifanyavyo tunavifanya kwa niaba ya Nchi na Rais wetu ndio maana likitokea baya lawama zote kwa Rais wa nchi kwanini linapotokea jema mnasita kusema kafanya hili Jema iweje Rais apokee mabaya tu mema asipokee?

||Serikali inafanya kwa niaba ya R ais na Rais anafanya kwa niaba ya wanachi||
Kaziindelee
 
Rais anazidi kufanya.Moshi mpoo👇

Screenshot_20220125-083415.png
 
____________________

Kwanza, Kisiasa :
Sote tunafahamu ili tuweze kushinda Uchaguzi wowote ule popote tunahitaji mambo matano makubwa ambayo ni,

1. Mgombea Mzuri

2. Mtandao au Chama

3. Agenda|Ilani ya Uchaguzi

4. Organization au timu kampeni

5. Rasilimali, fedha, vitu na watu

....................

||Serikali inafanya kwa niaba ya Rais na Rais anafanya kwa niaba ya wanachi||
Unaishi Nchi gani? Marekani?
Ili ushinde hapa Tanzania, unahitaji mambo 3 tu yafuatayo
1. Uwe na mamlaka ya kuchagua wajumbe wa Tume ya Uchaguzi.
2. Uwe na mamlaka ya kuchagua Wasimamizi wa Uchaguzi katika Halmashauri zote.
3. Uwe na mamlaka ya kuwaagiza Jeshi la Polisi wawashike Wapinzani ambao hawataki kukiri kuwa Uchaguzi ni kiini macho cha kuuhadaa Ulimwengu

Mpaka hapo Wananchi watakapokuja kushituka juu ya haki yao inayoporwa, tutaendelea kuwa na aina ya akina Musiba wanaojitoa ufahamu na kujiita Wanaharakati huru kwa lengo la kushibisha matumbo yao.
Siku tutakapokuwa na TUME HURU YA UCHAGUZI, ushindi hautatokana na karatasi zilizoandikwa jina Ilani.
Utatokana na utashi na uamuzi wa Watanzania waliopiga kura.
 
Binafsi hili neno Mama Samia atoa mabilioni kujenga shule badala ya Serikali yatoa mabilioni kujenga shule linanikera sana.
Ni wazi kuwa nchi inakosa dira hata ktk kuwasilisha taarifa kwa Umma, tujisahihishe mlio na dhamana ktk Nchi yetu.
 
Kazi ni nzuri kila Mahali,
Kauli ya SSH kwa mabenki kushusha riba imekuwa ya vitendo.Ikumbukwe matamko mengi ya awamu za awali hayakuwahi kuleta tija.

SSH ni level zingine,hatimaye crdb washusha viwango vya riba,ni kicheko kwa wafanyabiashara,wafanyakazi na wakulima 👇

Screenshot_20220125-114134.png
 
Binafsi hili neno Mama Samia atoa mabilioni kujenga shule badala ya Serikali yatoa mabilioni kujenga shule linanikera sana.
Ni wazi kuwa nchi inakosa dira hata ktk kuwasilisha taarifa kwa Umma, tujisahihishe mlio na dhamana ktk Nchi yetu.
Kwa nini likukere? Dhamana iko kwa Rais na Serikali ni ya Rais ..

Ngoja nikukere zaidi 😆😆

Screenshot_20220125-203624.png

Screenshot_20220125-215009.png
 
Maneno haya yanamaana sawa kimantiki " Rais kafanya X " " Serikali imefanya Y " au " " Tumefanya Z " tumia lolote utakuwa sahihi tu.​

Kunabaadhi ya wenzetu wameishiwa hoja hasa huku mitandaoni kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakipinga kwa nguvu zote kutumika kwa sentesi " Rais X kafanya mradi Y".

Watu hawa mara zote wanahoji niwapi huyu Rais X kapata huu ukwasi wa kutekeleza mradi Y? Jambo ambalo kisiasa wanadhani linamuinua zaidi huyu Rais X kwa kupewa endorsement ya mradi "Y".

Wakati wote watu hawa ambao wengi wao ni watu kutoka Upinzani wamependekeza itumike sentesi " Serikali X imetekeleza mradi Y".

UFAFANUZI WANGU
____________________

Kwanza, Kisiasa :
Sote tunafahamu ili tuweze kushinda Uchaguzi wowote ule popote tunahitaji mambo matano makubwa ambayo ni,

1. Mgombea Mzuri

2. Mtandao au Chama

3. Agenda|Ilani ya Uchaguzi

4. Organization au timu kampeni

5. Rasilimali, fedha, vitu na watu

Sasa kwahoja hii naomba tuangazie hitaji la tatu la kushinda Uchaguzi ambalo ni " ILANI YA UCHAGUZI " Ilani ya Uchaguzi inaweza kuwa yakuandikwa au yakutamkwa,

ILANI YA UCHAGUZI maana yake ni ahadi za mgombea au chama kwa Wapigakura au wananchi.
Tuelewane vizuri hapa tumesema Ilani ni ahadi ya mgombea au Chama wala sio ahadi ya Serikali kwa wapigakura au wananchi, nadhani hapa tunakubaliana wote,

Tukubaliane pia huyu mgombea baadae anaweza kushinda na kuwa Rais X, Sasa bila kusahau kuna ahadi aliwaahidi wapigakura wake yeye kama yeye yaani akishinda atafanya miradi X,Y,Z.

Kwaufafanuzi huu wa Ilani ya Uchaguzi kama miradi X,Y,Z ikitekelezwa na aliyekuwa Mgombea wa nafasi X ambae alishinda Uchaguzi huo kwa ahadi hizo na sasa anazitekeleza kama alivyoahidi ubaya unatoka wapi tukisema " Rais X katekeleza miradi X,Y,Z? "

Pili kimuundo :
Rais wa JMT ndio Raia namba moja wa JMT ndie mkuu wa Serikali ndio afisa manunuzi mkuu, ndie mshauri mkuu wa bajeti ndie mtia saini wa mwisho wa sheria ya bajeti unakataaje hajafanya wakati kila kitu kinaanzia na kuishia kwake!!

Tatu, Rais ndie mwenye mamlaka ya kusimamia pesa yote ya nchi kabla na baada ya bajeti kwenye kutekeleza miradi ya nchi kwani ndie aliyepewa dhamana na ndio atakayeulizwa ifikapo mwaka 2025 kulingana na Ilani yake iliyopita hivyo anafanya kwa niaba yetu

Nne, Urais ni taasisi, Sisi sote tuko chini ya Rais wa JMT akiwa kama Raia namba moja wa nchi, Hivyo tuvifanyavyo tunavifanya kwa niaba ya Nchi na Rais wetu ndio maana likitokea baya lawama zote kwa Rais wa nchi kwanini linapotokea jema mnasita kusema kafanya hili Jema iweje Rais apokee mabaya tu mema asipokee?

||Serikali inafanya kwa niaba ya Rais na Rais anafanya kwa niaba ya wanachi||

JamiiForums-1303142312.jpeg
 
Back
Top Bottom