Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,119
- 4,569
Utawala wa nchi yetu na nchi zote za kidemokrasia ni utawala wa sheria. Na sheria hizo tunazitunga wenyewe wananchi kupitia wawakilishi wetu kwenye bunge letu. Sisi ndiyo tunaoamua nchi yetu tuiendeshe namna gani kupitia sheria tutakazozitunga au kuzibadilisha kupitia wawakilishi wetu (wabunge) bungeni. Yaani mamlaka yote ya nchi ni ya kwetu sisi wananchi kupitia bunge letu. Yaani hata huyo rais atakayechaguliwa tuna mamlaka ya kumuondoa madarakani hata baada ya siku chache tu baada ya kuchaguliwa kupitia wawakilishi wetu bungeni. Hii ndiyo maana ya demokrasia. 'The government of the people by the people for the people'
Kwa msingi huo wa utawala wa sheria, kama rais atakayechaguliwa kama hatakuwa na wabunge wa kutosha bungeni hataweza hata kidogo kufanya mabadiliko ye yote ya utendaji kazi serikalini. Hataweza kutekeleza hata moja ya anayoyaahidi kwenye hizi kampeni hususani eti kufumua TRA, Traffic police, NHIF, kuongeza mishahara ya watumishi wa umma mara dufu, kutoa matibabu na ubwabwa bure kwa kila mtanzania, kuruhusu uvuvi haramu na wa nyaya ndogo utakaomaliza samaki wote nk.
Ili hayo yote anayoahidi yaweze kutekelezwa ni lazima yaidhinishwe na wabunge wetu kupitia utungaji au marekebisho ya sheria. Ukweli tunaojua ni kuwa hawa jamaa zetu wanaotoa hizi ahadi za porojo zinazofurahisha lakini si za uhalisia hawataweza hata kidogo kuwa na wabunge wa kutosha huko bungeni. Yaani idadi ya wabunge wao watakaoshinda haitafika hata robo ya wabunge wote. Maana yake ni kuwa miswada yao bungeni itapigwa chini na wabunge wa ccm ambao idadi yao itazidi theruthi mbili, idadi inayoruhusu kubadili hata katiba kwa jinsi wanavyotaka. Idadi inayoruhusu kumtoa madarakani rais wa nchi saa yo yote wanayotaka
Huu ndiyo ukweli wananchi wanaopaswa kuujua. Wao ndiyo wenye nchi.