Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,119
- 4,569
- Thread starter
- #41
Ubunge hautakiwi kuwa ni ajira. Ni uwakilishi wa wananchi. Enzi za Mwalimu hakuwa analipwa mshahara wo wote na hakukuwa na posho ya kikao ya laki tatu kwa siku. Mbunge alikuwa lazima awe ni mtu ambaye ana kazi yake inayompa kipato.Ubunge ni ajira siku hizi!
Tatizo linalotusumbua kwa sasa ni hilo la serikali kuwa inawalipa wabunge wetu mishahara na marupurupu makubwa kuliko mtu mwingine ye yote nchini. Hili ninakubaliana nawe kwamba wawakilishi wetu hawa badala ya kuwa part of us wamekuwa part of serikali.
Tulitegemea Lissu badala ya kusema ataongeza mishahara ya watumishi wa umma mara dufu, angesema atafuta misharaha na marupurupu ya wabunge. Hapo tungalimuunga mkono na kumpatia kura. Kuongeza mishahara ya watumishi wa umma na askari wetu mara dufu mapato yote ya serikali kupitia kodi zetu yangeishia kulipa mishahara tu ya watumishi hawa na bado hayangalitosha na hivyo kulazimishwa kuongezewa kodi. Hili halikubaliki.