Ukweli tunaotakiwa kuujua: Rais atakayekuwa hana wabunge wa kutosha Bungeni hataweza kuleta au kufanya mabadiliko yoyote na Urais wake hautadumu

Ubunge ni ajira siku hizi!
Ubunge hautakiwi kuwa ni ajira. Ni uwakilishi wa wananchi. Enzi za Mwalimu hakuwa analipwa mshahara wo wote na hakukuwa na posho ya kikao ya laki tatu kwa siku. Mbunge alikuwa lazima awe ni mtu ambaye ana kazi yake inayompa kipato.

Tatizo linalotusumbua kwa sasa ni hilo la serikali kuwa inawalipa wabunge wetu mishahara na marupurupu makubwa kuliko mtu mwingine ye yote nchini. Hili ninakubaliana nawe kwamba wawakilishi wetu hawa badala ya kuwa part of us wamekuwa part of serikali.

Tulitegemea Lissu badala ya kusema ataongeza mishahara ya watumishi wa umma mara dufu, angesema atafuta misharaha na marupurupu ya wabunge. Hapo tungalimuunga mkono na kumpatia kura. Kuongeza mishahara ya watumishi wa umma na askari wetu mara dufu mapato yote ya serikali kupitia kodi zetu yangeishia kulipa mishahara tu ya watumishi hawa na bado hayangalitosha na hivyo kulazimishwa kuongezewa kodi. Hili halikubaliki.
 
Rais wa aina hiyo kwa mjibu wa katiba yetu hana mamlaka hayo. See above threads.
 

..bunge haliwezi ku-impeach raisi anayeungwa mkono na wananchi.

..lakini itakuwa ni bahati njema kwa taifa kama tutalazimika kuunda serikali ya mseto.

..kwa kweli hilo likitokea tutaweza kuzi-sanitize siasa zetu ili ziwe kwa manufaa ya nchi na siyo vyama.

..naamini kila upande, kwa maana ya bunge na executive, watafanya kila jitihada kufanya kazi kwa mashirikiano.
 
Hakuna mbunge atakubali bunge livunjwe.
 
Hata wana CCM wengi tu wanataka uhuru na haki wanamuogopa jiwe. Wakipata uhuru wa kusema utaona nchi itakavyochangamka.
Kwa hiyo jiwe huwa anawashikia mawe siku za uchaguzi
 
JPM hafanyi kampeni kwa ajili ya kuomba kura zake. Yeye tayari ni Rais kilichobaki ni kuapishwa tu. Anafanya kampeni kwa ajili ya kuwaombea kura Wabunge na Madiwani.
 
Kweli Katiba yetu inahitaji marekebisho makubwa Sana, endeleeni kushusha nondo wakuu, hoja zenu zinajenga
 
Wewe unatoka nchi gani? Dunia yote inajua jinsi Tanzania ilivyo uteketeza ufisadi. Hadi nchi mbali mbali za Afrika huwa zinatuomba tuwaazime JPM akawe rais wao angalao kwa kipindi kifupi ili akakomeshe ufisadi uliokithiri kwenye nchi zao.
 
Bwashee wabunge wanawakilisha matumbo yao hawakuwakilishi wewe!
 
Mbunge gani anataka bunge livunjwe? Wakishaingia hutawasikia maana wakileta ujinga Rais anavunja bunge tunarudi kwenye uchaguzi wa wabunge na yeye ndiye anasimamia uchaguzi. Thubutuuuuu!
Kwani hukuona au kusikia pale Zitto alipojaribu kukusanya sahihi za wabunge kutaka kupeleka hoja ya kumuondoa JPM kuwa rais wa JMT ili bunge livunjwe na uchaguzi urudiwe? Wabunge wote wa upinzani waliweka saini zao lakini idadi yao haikufikia ile idadi inayotakiwa na katiba kupeleka hoja hiyo bungeni. Wabunge wa chama tawala hawakusaini hilo likaratasi lake na likaishia hapo. Sasa Lissu akipata urais wabunge wote wa ccm watafanya kama alivyfanya Zitto, na kwa kuwa ni wengi idadi inayotakiwa kikatiba itafikiwa na Lissu atakuwa out!
 
CCM haitakubali kuwa pamoja na vibaraka wa mabeberu. Shida ndiyo inaanzia hapo. Angalikuwa Lipumba au Mbatia hapo ingalikuwa poa. Si hawa jamaa zetu.
 
CCM haitakubali kuwa pamoja na vibaraka wa mabeberu. Shida ndiyo inaazia hapo. Angalikuwa Lipumba au Mbatia hapo ingalikuwa poa. Si hawa jamaa zetu.

..raisi anayekuwa impeached ni yule asiyeungwa mkono na wananchi.

..na ccm wakijaribu kumu-impeach raisi wanaweza kukutana na resistance ya wenzao wanaounga mkono serikali ya mseto.

..na impeachment proceedings is a risky business, ukiijaribu na ikashindwa, chama kinaweza kupoteza uungwaji mkono na wananchi.

..njia bora ni kufanya kazi pamoja. kuweka mbele maslahi ya nchi badala ya maslahi ya vyama.
 
Mmeshindwa kuipata hiyo demokrasia mnayoililia ndani ya Chadema mtaweza kuipata ya nchi nzima? Chadema ipo kwenye dictatorship ya Mbowe ingawa ukweli huu mkiambiwa mnachukia. Huyo mlevi wa konyagi sijui aliwaloga vipi.

Kubadili nchi yoyote ile ni rahisi sana kama huko kwenye chama chenu mko na demokrasia ya kweli, lakini huko kwenu wote mnawewesekaweweseka tu nani atawaamini? Angalia kina Zito Kabwe, Membe et al ni aibu tupu, uchu wa madaraka ndio umewatawala.

To be honest with you JPM and CCM hawana mshindani wanavinjari tu. You better cleanse your parties.
 
Akiwa out sheria inasemaje? Nani atashikilia uongozi ili kufanya uchaguzi wa Rais mwingine?
 
Kabla hawajamaliza kuweka sahihi rais anatangaza kulivunja bunge. Wakati huo yeye alishajiteulia madc wakurugenzi sasa hapo ndio ccm inaenda kufia hapo
 
Kabla hawajamaliza kuweka sahihi rais anatangaza kulivunja bunge. Wakati huo yeye alishajiteulia madc wakurugenzi sasa hapo ndio ccm inaenda kufia hapo
Hizo teuzi zake zitakuwa batili. Na akiendelea kuleta fyoko fyoko wanaume wanamuweka lockdown nyumbani kwake kama ilivyofanyika kwa Mzee Mugabe huko Zimbabwe.
 
Itakuwa serikali ya mseto, kwani katiba inasema waziri mkuu atatoka kwenye chama chenye wabunge wengi. Hivyo chama kitakacho mtoa waziri mkuu pia kitatoa mwaziri kadhaa. Na hapo nchi yetu itasitawi kidemokrasia na mijadala huru ya kibunge, maana hatutakuwa na bughudha au ubaguzi wa kichama. Kimoja kina prezidaa na kingine kina pm, halafu vyote vimechangia mawaziri.

Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…