Ukweli tunaotakiwa kuujua: Rais atakayekuwa hana wabunge wa kutosha Bungeni hataweza kuleta au kufanya mabadiliko yoyote na Urais wake hautadumu

Kweli tupu, hapo uchaguzi bado mwenzake kashaweka point 3 na magoli kadhaa wabunge bila kupingwa wao 0.Uchaguzi ukija si ndio thunami kabisa. Wana saccos, endeleeni kujisifia nyomi tu, mwaka huu mnaambulia kura chache kuliko zile za 2015 kwa hizo porojo zenu..
 
Hizo teuzi zake zitakuwa batili. Na akiendelea kuleta fyoko fyoko wanaume wanamuweka lockdown nyumbani kwake kama ilivyofanyika kwa Mzee Mugabe huko Zimbabwe.
Ok
 
Kuna upotoshaji unaufanya, kwa kujua, kutokujua au labda kwa kuzidiwa na mapenzi! Hoja yako ina ukweli nusu tu, sehemu ya pili hujazingatia!
Ni wabunge wangapi watakao kuwa na uhakika wa kurudi bila kubebwa na mamlaka?! Kwa raisi wa chama chenye uchache wa wabunge, uchaguzi ukirudiwa atakua na advantage kubwa Kwa sababu;
Ana serikali na vyombo vyake.
Hofu ya watu kufanya mabadiliko imeisha
Wabunge waliopita bila kupingwa, sasa watapingwa!
Wale waliokua wanasifu kiunafiki wataonesha makucha yao!
Hii propaganda yako haitutishi, alafu siyo kweli kwamba UKAWA walipata wabunge 18, 2015, kasome takwimu zako vizuri, usije ukafanana na Baba ako anayesema Nyerere alitawala miaka 27!
 
Kwa katiba ya sasa, bunge likileta fyoko dhidi ya rais anao uwezo wa kulivunja.
Mfano Lissu awe Rais na wabunge wake kiduchu, anaweza kulivunja Bunge au Bunge litakuwa linamwendesha linavyotaka ili mradi yeye ni Rais.
 
Dr. Akili tumianakili Basi..kwà hii katiba na hata hatafikia kwenye hiyo impeachment..Hadi Bunge likutane tayari ameshafanya mabadiliko meengi tuu Sana mnoo. Anaweza vunja hilo Bunge hata kabla ya impeachment. Na sijui wajua safari ya impeachment au waisikia tuu. Bunge ni barabara ya kuanzia tu bosi..Kati a hii kila kitu kinawezekana bosii hata Kama huna mbunge hata mmoja.
 
..Raisi wa Tz ana mamlaka makubwa mno aliyopewa na Katiba.

..akiwa hana wabunge wengi itasaidia asitumie madaraka yake vibaya.

..kwa maoni yangu hili litakuwa ni jambo la heri. Litaibadilisha Tz for good.
 
Haohao mliowatolea wagombea wao kwa ghirba (Lissu na Maalim) ndio tunawapa kura. tegemeo lenu labda NEC tu.
 
Haohao mliowatolea wagombea wao kwa ghirba (Lissu na Maalim) ndio tunawapa kura. tegemeo lenu labda NEC tu.
Kwani mlikuwa hamuwapi kura? Mwaka 2015 hamukuwapa kura?
Demokrasia ni utawala wa wale walo wengi. Sisi ndiyo tuliyo wengi.
 
Samahani, kwani bajeti ya kununulia ndege na kujenga uwanja Chato ilipitishwa lini bungeni?

Pia, maazimio ya kutokuwaongeza mishahara watumishi yalifanyika bunge la ngapi?

#MADARAKAYARAIS!
 

Kwani hao watakao mchagua Rais watashindwaje kumchagua mbunge pia wa eneo hilo
 
Kwani hao watakao mchagua Rais watashindwaje kumchagua mbunge pia wa eneo hilo
Hicho chama hakikuweza kupata/ kuweka mgombea ubunge kila jimbo. Na wagombea iliyowaweka wengi wao hawakuwa na sifa au hawakuweza kutimiza vigezo vinavyotakiwa na hivyo kuondolewa baada ya kuwekewa pingamizi kwa mjibu wa katiba na sheria zetu za uchaguzi. Yaani wengi wao walishindwa hata kujaza ile fomu.
Wengi waliobaki kugombea hawakubaliki majimboni kwao ukiwalinganisha na hao wa chama tawala eg Mdee vs Gwajima.

Pia kumbuka wapiga kura walio wengi hawako chama cho chote cha siasa. Kwa walio kwenye vyama vya siasa: ccm ndicho chama kongwe kikiwa na wanachama millioni 12 wakati chadema kina wanachama wasiozidi laki 7 tu! Huo ndiyo ukweli ndugu yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…