Ukweli tuuweke hapa kuhusu Kassim Mganga!

Ukweli tuuweke hapa kuhusu Kassim Mganga!

Penzi langu penzi lako
Pumzi umeshika
Bibiee bibiee masikio weka pamba
Wambie kwako nimeshatia nanga
Naapa milele sitolivunja abadaani
Napiga vigelee pete ya ndoa kidoleni
 
Full respect to this boy... ... Amekosa network nzuri tu, any way, its all about time
 
Tajiri wa mahaba ! Mi awena inaniachaga hoiii mpaka kesho siichoki masikioni!
 
Dunia imebadilika sana. Wasanii wasipobadili malengo yao na aina ya muziki wao wataendelea kuona wachache wanatusua
 
Tena nawaambia dude lake la manuari ni kitu nyingine ambayo ni ngumu sn kuiskia kwa msanii yeyote hapa bongo!!hila na fitina na pia kutojielewa ni moja ya 7bu za kupoteza wasanii wazur hapa bongo.Kassim habar nyingine bana so hawa jamaa zetu kelele mingi hamna kitu
 
Sasa kama Kassim ni Icon ya bongo je Diamond Platnumz baba tifah Dangote mtoto wa tandale young bilioner, icon ya africa mashariki na kati na mashariki ya mbali a.k.a Simba, Kifaru, atakuwa nani sasa?
Me/ke???
 
Habari zenu wakuu!

Nimefikiria kitu kuhusu huyu jamaa, katika tasnia ya mziki hapa Tanzania! Huyu jamaa yupo vizuri, ukisikiliza nyimbo zake kuna tungo nzuri kwa lugha yetu ya kiswahili fasaha pasipo kuchanganya lugha za kigeni, pia ana mashairi yaliyotulia pasipo kuwa na matusi au misamiati ya kipuuzi!

Hakika jamaa anatisha sana kuliko hata hawa 'waramba midomo' wa sasa.

Ongeza ulichoona kutoka kwa huyu jamaa!
Tatizo huyu dogo ana mashauzi sana na ukale ukale flan hivi nadhani ni athari za UTanga(udigo),but kuimba anajua tang enzi zile za Aweza na Haiwezekani hajawahi kukosea
 
Hivi waga ana wimbo na christian bella? Kuna wimbo bella kashirikishwa na mtu ana sauti kama kassim mganga...imetulia sana
 
Wachangiaji wengi humu wanafiki wakubwa!!
Nyimbo za kassim wanazisikia kwa majirani tu...playlists zao zimejaa nyimbo za Dabliusibi
 
Sasa kama Kassim ni Icon ya bongo je Diamond Platnumz baba tifah Dangote mtoto wa tandale young bilioner, icon ya africa mashariki na kati na mashariki ya mbali a.k.a Simba, Kifaru, atakuwa nani sasa?

umeogopa bure, Icon wanaweza kuwa wengi pia

halafu kakuambia kabisa "hachanganyi lugha" ana kiswahili fasaha...hapo Mond hayupo

darasani lazima ulikuwa unapata pata 20/100 ukifaulu sana 30/100 halafu unarembesha mwandiko
 
Back
Top Bottom