Ukweli uliofichika kwa Dunia ya Leo

Morg

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2018
Posts
1,301
Reaction score
1,788
Acha kuhamasisha mila za Kizungu za Uzinifu/ mahusiano ( girlfriend na boyfriend) kwa kuwa zinamdhalilisha mwanamke. Na kupitia huo Uzinifu ndipo Wazungu wakaja na mawazo ya kuwa mwanamke ajitafutie pesa ili asimtegemee mwanaume hivyo lengo na makusudi ni kuhakikisha Uzinifu unaendelea ambapo mwanamke naye atakuwa na uwezo wa kubadilisha wanaume atakavyo.
Ndoa ya halali iliyoamrishwa na Mungu ndio iliyohimiza mwanaume kuwa kichwa cha familia, kutoa huduma na kumpa haki zake mwanamke.

Yafuatayo ni madhara ya Uzinifu/ mahusiano.

1. Wanawake kukosa thamani ambapo watakuwa wanaonekana ni chombo cha starehe.

2. Mwanamke kutotambuliwa upande wa Mme na hata akitambuliwa hukosa thamani.

3. Kukosa haki zake za kuhudumiwa na haki nyingezo kwa kuwa mwanaume halazimishwi na maandiko wala serikali kuhudumia.

4. Watoto kukosa msaada kutoka upande wa Mme kwa kuwa mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa ni rahisi kukataliwa na mwanaume na ukoo wake kwa kuwa wasiwasi ni mwingi.

5. Kuongezeka kwa usingo mother na maovu mengine kama vile ukahaba n.k.

6. Mwanamke kupata tabu sana kumpata mwanaume mwingine mwenye nia ya kuoa kwa kuwa wanaume wengi hawapendi wanawake waliozaa au wasio bikra.

7. Wazazi wa mwanamke kukosa heshima ktk jamii kwa kuwa binti yao anaziniwa bila ndoa.

8. Mwanamke kutoridhika tendo la ndoa pindi aolewapo kuwa keshaliwa na kuachwa na wanaume wengi wenye Size tofauti tofauti kipindi cha mahusiano.

Nb: Hivyo wanawake hamasisheni ndoa za halali ambayo ndo maagizo ya Mungu ili tuwape heshima yenu na si mila za Kizungu za Uzinifu/ mahusiano ( boyfriend na girlfriend).
 
Kwa nini huwa tunapenda kudanganyana Waafrika?Hivi ni nani aliyewaambia mila za Wazungu ni ufuska/kuzini hovyo na mabalaa mengine.Mkae mtulie.Ina maana huko uzunguni hakuna wenye kufuata malezi,makuzi na staha njema maishani?Hayo mambo ya hovyohovyo ndiyo yamo kwenye katiba zao na wanazifuata au mnajitungia tu.Tuache uzushi.
 
Kwenye katiba zao umo mpaka ushoga, wazungu hawana maadili
 
Wee jamaa ndio umeshatutisa wana nini.
Maana sikuelewi elewi siku hizi au umeokoka mwanetu
1 Wakorintho 6:18-20

Jiepusheni kabisa na uzinzi. Dhambi nyingine zote hutendwa nje ya mwili lakini mzinzi hutenda dhambi dhidi ya mwili wake mwenyewe. Je, hamjui kwamba miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, ambaye mlimpokea kutoka kwa Mungu? Nyinyi basi, si mali yenu wenyewe. Mlinunuliwa kwa bei kubwa. Kwa hiyo, itumieni miili yenu kwa ajili ya kumtukuza Mungu.
 
Wee jamaa ndio umeshatutisa wana nini.
Maana sikuelewi elewi siku hizi au umeokoka mwanetu
Katika Mithali 6:32 Biblia inasema “Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake”

na pia katika Mithali 6:26 inasema “Maana kwa Malaya mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate; na kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya thamani”
 
Umekuwa muhubiri
 
Ngoja nijiunge nawe
Karibu sana mzabzab kumtumikia Mungu kuna faida sana.

Nilikuwa naongea na mfanyakazi mwenzangu saa mbili kama na dk 40 asubuhi, inafika saa tatu na dk tano napigiwa simu mtu kafaaa.. nikasema oooh maaai.. sina changu duniani acha nimtumikie Mungu.. mtu mzima unaweza ukawa chochote na mda wowote bora kuwake hadhina mbinguni ambapo kutu haiwezi haribu wala wevi kufika na kuiba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…