Ukweli unaoogopwa na kufichwa na watawala; Wanaharakati ni bora kuliko wanasiasa.

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Unaweza kujiuliza nini kinasababisha tabaka tawala kushambulia na kuchukia sana wanaharakati. Jibu ni rahisi sana, wanaharakati wanatishia "status quo" ya watawala, popote pale Dunia katika Karne ya 20 na 21 hakuna mabadiliko makubwa ya kubadilisha au mageuzi ya utawala yaliyowezekana bila msukumo wa wanaharakati.

Watu maarufu wote unaowafahamu walioleta mabadiliko katika hizo karne mbili walianza kama wanaharakati au walikuwa ni wa wanaharakati. Wanaharakati ndio Waanzilishi wa mabadiliko makubwa ya kimfumo.
 
Ni kwa sababu Taasisi za kiutawala zenyewe ni zao la maandamano na mapambano ya wanaharakati.

Mfumo wowote unaojitawala wenyewe hauwezi kujirekebisha bila nguvu ya nje.
 
Hilo tunalifahamu sana! Kiujumla hakuna namna hawa watawala wataweza kutufanya wajinga Tena!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…