Ukweli Usemwe Ali Kiba hajawahi kuwa na Enzi ya Ufalme kwenye Bongo Flavor sana sana Amedumu kwenye Mziki wa Bongo tu

Hao wote uliowataja hawapo au wamefifia kwenye tasnia ya muziki.
Hapo ndiyo ufalme wa Ali Kiba unapodhihirika.
 
Afande Selle alistahili kwa wimbo wa mtazamo alitisha sana
 
Kitaalamu Ali Kiba ni Mwanamuziki mzuri....bakhti mbaya soko halijamkubali.....Hao wengine ni waburudishaji na angalau sokoni.....
 
Ni kweli usemayo
Ila kitendo cha yeye kudumu kwenye muziki tayari ni ufalme huo
Ameweza jambo lililowashinda wengi wakiwemo hao uliowataja
πŸ‘
Hapa nipo zangu Makumbusho kwenye li Pub namalizia weekend na sikiliza ngoma za Kiba. My All time favourite Artist
 
Prof j aliingua na Usinitenge ilikua ngumu kutoboa,feruzi nyimbo ya starehe ilikua bado haijatoka,hao wengine wote hawakua na hit kali kama darubini kali ya afande kipindi kile,ndio mana mshindi wa pili alikua inspector ,wa watatu wakawa mandojo na domo kaya ,ni sawa na kusema sele aliwaacha mbali sana
1.sele
2.sele
3.sele
4.inspector
Kwa mtazamo wangu
 
Feruzi asingeingia kwenye Shidano kwa sababu hakuna Mtu wa Kufoka foka..
Unasema Soggy hakua Na hit?, Solo thang na Proff jay?? Na Jay mo Unataka Kumsahau??
Kumbuka hapo tunazungumzia mwaka 2004..

Nakukumbusha Professor Jay/Nigga J aliamua kuwa solo artist na Kutoka HBC (Hard Blaster crew)..
Mwaka 2001 akatoa albamu yake ya kwanza inayoitwa "Machozi Jasho na Damu".

Unaijua machozi jasho na Damu wewe?????
Ndo iliyomfanya Sugu akastaafu muziki..

Usisahau mwaka huo 2001 alipata tuzo ya kuwa mtunzi bora wa Hip Hop Tanzania kwa wimbo wake wa 'Ndio Mzee' kutoka kwenye albamu hiyo,umo kuna nyimbo kama "Piga Makofi na "Bongo Dar es Salaam", "Chemsha Bongo" na 'Mamsapu'

Pia usisahau Mwaka 2003 alitoa albamu ya pili inayoitwa "Mapinduzi Halisi" ambayo nayo ilishinda tuzo ya Kili Music Awards kuwa albamu bora ya muziki wa Hip Hop nchini Tanzania kwa mwaka 2003. Albamu hii ilibeba nyimbo kama "Zali la Mentali", "Msinitenge," "Promota Anabeep" nakadhalika...

Na hiyo ni kabla ya mwaka 2006 miezi ya mwanzoni ambapo alitoa album ya J.O.S.E.P.H..


Sasa mwaka 2004 Proff alikuwa na Album mbili yenye Nyimbo za Moto zote karibu 20 na zote zimeshinda tuzo ya Kili uje mlinganishe na Afande ambaye alikuwa na Album ina nyimbo kumi??

Ambazo nyimbo Maarufu zilikuwa 5 tu
 
Reactions: K11
Additional
πŸ‘‡πŸ»
Afande sele ni kweli hakustahili kupata ile tuzo lakini ukweli usiopingika kipindi kile ndo alikua ametoa Nyimbo ya Darubini kali featuring Dogo D (Lamek Dito) na ndo ngoma ilikua inasumbua sana kwa kipindi kile km ngoma ya Hakunaga by sumalee au Mziki ya Darasa zilivyotoka, so kutokana na hilo ,hii ndo ilifanya ma judge wampe hiyo tuzo ya Mfalme wa rymes

Ukija kwa soggy Dog kipindi kile walikua na bifu ila kwa sasa wameshasahau hizo tofauti zao na wamekua washkaji kama huamini hili pitia post za afande sele, mara kadhaa amekua akimualika Soggy kule Moro maskani kwake (Peponi camp) na sio soggy tuu hata Oten ,sahv hawa watu washakua watu wazima 50+ ni ngumu kuwa na bifu kwa mambo ya 20 years back
 
Unajua, anaweza asiwe mfalme kwako ila akawa kwa wengine.

Wengine tunamuona ni mfalme kwa sbb:

1.Muziki wake hautegemei scandal/kiki

2.Muziki wake ni wa rika zote, unaweza sikiliza na wazazi na watoto (hazina tafsiri ya matusi na ngono).
Hata kanisani unaweza piga.

3.Maisha yake binafsi (lifestyle) yanakubalika na wengi.
-Hafungamani na mashoga,hafugi mashoga.
- Maisha yake binafsi ni yake na sio ya kitaifa; Nani anajua maisha ya mamake? babake? dada zake?
Wengine hawa unasikia baba anatia huyu dogo dogo;
mama anatiwa na yule kijana wa rika moja na mwanae!,
dada anatiwa na huyu na yule!
Na Yeye anatia/kutiwa na huyu na yule.
(unaweza fikiria wao tu ndio wenye sehemu za siri)
 
Cinderella, nakishi nakishi, mac mugs, Sabrina,sikuoni
Mazee hii ilikua bonge la albam na lilienda Sana viral..

😊😊
 
Basi we ndo mfalme,but nilikuwa nampenda sana dully sikes
Na ukiniambia nitaje wasanii wangu waliozaliwa na kipaji na sio kuforce basi mmojawapo na Ali salehe Kiba
 
Mzee acha Kum underrate AFANDE SELE..
Jamaa alikua Ni game change ukisikiliza Yale mangoma yake yote ya kwenye darubini Kali

Baadae,
WATU PORI a.k.a WASHAMBA wakali wa vina ujumbe ndio unatamba MC KOBA, MDOGO DITO bonge la kombinenga..

AFANDE ana mchango wake kwenye game la bongo flavor
 
Unamchukia mtu ambae hajui hata kama kuna mtu kama wewe duniani
 
Pale unapojidai unajua kumbe hujui.
 
Yeye ni mkongwe tu kwenye game hana historia ya maajabu hajawahi kushika enzi kwenye game, alikuwa chawa wa Ruge na Bado ni Chawa wa Couds Media
Mkuu hii comment yako imeharibu andiko lako umeonyesha dhahiri una chuki binafsi na Alikiba na Clouds kwahiyo madai yako yanajenngwa katika chuki na si hoja ya msingi
 
Nakubaliana na Weww kwa 100%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…