Ukweli usemwe: Hayati Magufuli ndio alileta siasa za "Uchawa" kwa kupenda kusifiwa na kutotaka kukosolewa

Siasa za uchawa zilianza kipindi cha Kikwete,hapa Magufuri anaonewa.
 
Huu ndio ukweli. Ila misukule yake haitakuelewa. Hata kama mtu umetimiza wajibu wake haina haja kumuabudu kulikopitiliza kiivyo.

Kwanza unamsifia vipi mtu alietimiza wajibu wake? Hivi utaichukuliaje familia yenye watoto ambao wanapita mtaani kumsifia baba yao kwa kuwapa malezi bora? Wanakula vizuri? Wanalala pazuri? Si wataonekana machizi? Tena wanaweza kurushiwa hadi mawe.

Ila nina uhakika familia itakayoandamana mtaani kulalamikia juu ya tabia za baba yao kutowapa chakula, malazi na lishe bora watu watawasikiliza na hata wanaweza kuingilia kati na kumuwajibisha baba wa hiyo familia.

Kiukweli chawa wa Magu walizidi hadi jamaa akajijengea chuki miongoni mwa watanzania wengi wenye akili timamu. Nimesema wenye akili timamu, narudia tena, wenye akili timamu!
 
Kwa kiwango kidogo,ila awamu ya 5 ndio uchawa ulipata kibali rasmi kwa mpenda sifa. Na Sasa Samia ameamua kufuata approach ile ile japo yeye sio dhalimu kama bwana yule.
Jpm alikuwa dhalimu kwa watu dhalimu,na alikuwa mwema kwa watu wema,leo watu dhalimu na waovu kama wewe wana uhuru na wanafanya udhalimu wao kwa uhuru.
 
Skuizi mnaita uChawa, lakini siku za nyuma tuliita uPambe "nuksi" na hii ilikua kwasababu kazi yao ni kuuma na kupuliza.
Hawa walikuepo rasmi tangu baada ya mkapa kuingia madarakani.
 
Unaumwa wewe, kabla hata magufuli hajawa rais kinyang'anyiro cha kupata ugombea kwa ccm kuna aliyekuwa na machawa kumzidi lowasa? Wale friends of lowasa.
 
UONGO

JPM ALIKUWA NA KILA SABABU YA KUSIFIWA KWA SABABU ALIFANYA VITU VINAVYOONEKANA

UCHAWA UMEZALISHWA AWAMU YA SITA KWA UJINGA WA KUTAKA KUCOPY VITU VYA AWAMU YA TANO AMBAVYO VINGI HAMVIWEZI MMEAMUA KUISHIA KUWA MDUDU CHAWA
 
Jpm alikuwa dhalimu kwa watu dhalimu,na alikuwa mwema kwa watu wema,leo watu dhalimu na waovu kama wewe wana uhuru na wanafanya udhalimu wao kwa uhuru.
Hakuwa mwema, Bali alikuwa anajifanya mwema kwa watu waliomsujudia. Mtu yoyote alipaswa kushughuliwa na Sheria, sio kwa ulevi wa madaraka. Na kwa kukusaidia tu, ingekuwa nchi yetu Sheria zinafuatwa itakiwavyo, yeye pia alikuwa ni muhalifu.
 
Huyo mwamba mtamtaja kwa vinywa vyemu mpaka yesu atakaprudi, shenz kabisa
 
So what!!! Mpuuzi mmoja wewe
 
Mange anawageuza CHAWA anavyotaka badala ya kupambana na Mange wewe unaanzisha ligi na marehemu. Pathetic
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…