sinza pazuri
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 3,344
- 9,066
Juzi kati hapa tumeona Nandy akiwashambulia Wasafi media akiwatuhumu mambo ya kitoto yasiyo na kichwa wala miguu.
Wote tunajua Nandy hajawai toa ushirikiano kwa Wasafi media akiombwa interview au kumshirikisha kwa namna yoyote anachomoa. Lengo kutengeneza kitu kwa mashabiki kuwa anabaniwa ili apate huruma. Tuachane na hayo.
Shida kubwa ya Nandy kwa sasa ni Zuchu. Amejawa hofu akiona Zuchu yupo pale kileleni na anazidi kupanda. Hii ni normal kwa binadamu yoyote aliyekuwa juu alafu ghafla anatokea mtu anampiku lazima ashikwe na bumbuwazi.
Alikuwa anatuma watu mitandaoni wamchafue Zuchu. Many thanks kwa Mwijaku alituvujishia sauti ya mipango yake miovu aliyokuwa anapanga sirini kutuma watu wamchafue Zuchu. Watu waliisikia na bado wakakausha Zuchu alitumia hekma kuepusha bifu ambalo unalitafuta likubebe kama style aliyotumia Kiba na Mmakonde.
Kitu kinamtisha zaidi ni ile generation iliyo active na muziki inavyomkubali Zuchu....watoto wadogo wanaimba nyimbo za Zuchu kama wametunga nae...watoto wa secondary mpaka vyuoni ni Zuchu hii kwa kweli inamuogopesha.
Pole sana Nandy utazoea kila zama na vitabu vyake. Hata wewe uliwakuta kina Lady Jaydee na Vanessa Mdee wakasanda tena Vanessa akaingia mpaka kwenye uraibu.
Huu sasa ni wakati wa Zuchu. Zuchu ndio msanii wa kike namba moja East Africa kwa sasa. Kubali na uzoee lasivyo na wewe utaishia kula unga.
Unajiliza kutengeneza huruma ili watu wakuokoe na kibano cha Zuchu ila haitosaidia kukandwa kupo pale pale.