Ukweli usemwe Yanga ni Mabingwa tena

Ukweli usemwe Yanga ni Mabingwa tena

Mshuza2

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2010
Posts
11,261
Reaction score
17,202
Wala haihitaji akili nyingi kuona hili,timu inajituma uwanjani, unaona kabisa wana kiu na ushindi! Wachezaji kila mmoja kwa nafasi yake anatimiza majukumu yake.

Yanga sports club watachukua ubingwa mpaka wachoke wenyewe..kama timu nyingine hazitabadilika.Sio kama huku kwetu tumejaza "mafaza" watupu.

Ningeshauri TFF wangewatafutia yanga kombe zuri zaidi mapema maana wanastahili kilicho bora, Wanayanga vimbeni, mnastahili.
 
Nyie akikosekana Chama, mnakua kama Njombe mji. Sisi anatoka Fei, ila mpira unapigwa kama kawaida!

Nyie makolo endeleeni kujadili mkataba wa Feitoto. Mkija kushtuka, Casablanca hawa hapa, wakati tegemeo ni Kibudenga!
 
Hongereni watani Yanga sc kwa kutwaa taji la ubingwa wa msimu huu wa 2022/2023, Simba tujipange tufanye vizuri champions league japo group letu ni gumu.

Mambo ya ubingwa wa ligi kuu tuachane nayo msimu huu tujipange msimu ujao tu!

Hongereni uto!!
 
Umejiondoa Simba?
Hapana ila nawasifia kwa ubora wa kikosi chao.
Pia kwa upambanaji wao muda wote.
Simba wakifungwa goli moja kurudisha ni kwa mbinde sana na mechi zote walizotangulia kufungwa sana sana walifanikiwa kusawazisha tu na sio kushinda.

Yanga ndio timu nzuri msimu huu na ni mabingwa tena.
 
Back
Top Bottom