Ukweli usemwe Yanga wamefika mwisho, ligi ya mabingwa sio lelemama

Ulivyoandika ni kama Simba wameshafuzu....ushabiki mbaya sana
Hilo kundi si lelemama. Lina mabingwa watupu wa Misri, Algeria, Tanzania na Ghana...hakuna mshindi wa pili hapo.

Kwa uchanga wako wa kufuatilia soka na ushabiki wako unaona kuwa mambo yameshaisha. Jua kuwa hapo hakuna mwenye uhakika wa kufuzu hadi sasa. Kama hujui kwenye jambo, vyema kukaa kimya.

Huyo Al Ahly ameshinda mechi moja tu na kutoa sare mbili. Amepoteza alama nne. Naye leo ametoa suluhu nyumbani.
 
Unaongea maneno meengii na unarudi kwenye point Ile Ile ya yanga akishinda nyumbani, makolo uwa mna akili kweli nyie? Mi nikadhani tiyali yanga keshaondolewa kwenye mbio za kwenda robo kumbe unatuletea hadithi za abunwasi hapa, si usubili zichezwe izo mechi xaxa ndio ulete uozo wako hapa, KUNDI bado liko wazi kwa yeyote ndio maana ya droo za Leo yeyote Ana uwezo wa kwenda robo!
 
Ujui kitu wewe amka ukakojoe ukalale kijana wa mangungu!
 
Si walishasema wao Ni kufika makundi ndio lengo Lao ....unapoteza muda kuchambua
Kauli ilikuwa ni kwamba "Nyinyi kila mwaka mnaishia robo fainali, sisi tumekuja huku kuwaonyesha kazi"

Wakati makundi yamepangwa, mashabiki wa Yanga walisema Belouzdad na Madeama ndio vibonde wa kundi (watapiga nje ndani).

Lakini ni jambo jema kama heshima imerudi.
 

Huo ni utabiri ulio ufanya
Sasa tusubiri tuone uhalisia
 
Alipigwa 5 huyo unaemficha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…