tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,327
- 4,624
Nimeshindwa niweke wapi hii comment, JF mnaweza unganisha na uzi wowote.
Tukio la Janeth Magufuli kulazwa Muhimbili Novemba 2016 linapaswa kufafanuliwa kwa muktadha wa ukweli na uwazi. Huwa inahuzunisha sana kuona watu wanaweza wakawa wanaongelea tukio la kusimuliwa, wakalifanya ukweli wakati halina ukweli. Magufuli pamoja na madhaifu mengi aliyokuwa nayo, alisingiziwa mengi sana, na wengi hayo waliyoyasikia wameyafanya kuwa ndio maisha ya Magufuli wakati wa Uhai wake. Na mmoja wa waliodanganywa, lakini anadhani ana habari ya kweli ni Erick Kabendera. Lakini unaelewa kwa namna Erick alivyopita katika tanuru la moto, anaweza asiyafikirie vyema hata yale aliyosimuliwa.
Wakati Mama Janeth Magufuli analazwa Muhimbili Novemba 2016, huyu Mama hakupata kipigo chochote, lakini ndio ilikuwa habari ya mjini. Ni muhimu kwa wale waliohusika kwa namna moja au nyingine na matibabu yake bila kusimuliwa kuweka wazi kwamba hali yake ya kiafya kipindi kile haikuwa na uhusiano wowote na kipigo au ukatili wa aina yoyote. Badala yake, lilikuwa jambo la kiafya ambalo lilihitaji matibabu ya kitaalamu na uangalizi wa karibu. Kama kila mtu siri zake za matibabu zingetolewa nje, basi labda tungekuwa na mtazamo tofauti kuhusu mambo mengi sana kuhusu watu na vitu. Mfano kwa waliofariki unaweza ukaondoa imani za kurogwa, kupigwa n.k, na kwa wale wanaoishi unaweza gundua kwamba wengine labda wamebakiza siku chache, na hata ukisikia wamefariki, hutoshtuka.
Kwa wale waliokuwa karibu na mazingira hayo ya hospitali wakati Janeth amelazwa, dalili na hali iliyoshughulikiwa hospitalini kipindi hicho haikuonyesha ishara yoyote ya majeraha yanayoweza kuhusishwa na ukatili wa kimwili. Uchunguzi uliofanywa ulionyesha sababu za kiafya zinazohusiana na matatizo ya kawaida yanayoweza kumpata mtu yeyote na hakika yanawapata watu wengi tu kila siku. Shida ukiwa mke wa Rais, watu wanadhani haupaswi kulazwa.
Katika kipindi hicho, Janeth akiwa amelazwa, Magufuli alionekana kujali sana na alikuwa karibu na mkewe, akihakikisha kuwa anapata huduma bora. Hayati Magufuli, alitumia muda wake mwingi usiku kukaa na mkewe wodini Muhimbili. Hakuna waandishi wa habari wajualo hilo, maana walilishwa matango pori. Taarifa za uvumi zinazohusiana na tukio hili hazina msingi wowote wa kweli, na ni muhimu kutozizingatia ili kuepuka kueneza dhana potofu.
Kutokana na Erick Kabendera kulishwa tango pori hilo (najua anajiamini sana na aliloandika), inaonesha hata habari nyingine kuhusu Magufuli, zitakuwa ni hekaya, zisizokuwa na ukweli.
Ni muhimu sana sisi binadamu kuacha kuongelea habari tusizokuwa na uhakika nazo hasa za kifamilia. Ukiwa na hizo tabia, usishangae watu wakiongelea habari zako, ambazo nawe hata huzijui. Karma is real.