Ukweli usiosemwa juu ya dini za Kiafrika

Ukweli usiosemwa juu ya dini za Kiafrika

Frustration

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
3,134
Reaction score
4,124
Afrika ina dini ambazo ni nyingi sana kuliko bara lolote lile Duniani. Dini hizi nyingi zimepigwa ban na watu wa nje (whites) kwa sababu tu ya inferior ya mtu mweusi wa zamani. Kuishi kwa kumtegemea mzungu kwa kila kitu hadi ikapelekea hadi sasa watu wanategemea pia dini za Kizungu.

Hakuna kabila hata moja Afrika ambalo limepoteza imani ya dini yao, ndio maana hata waendao makanisani hutembelea kwa mababu zao kupata kinga. Dini zote Afrika zilikuwa hazihusiani na uchawi ila mtu mweupe ndiye aliempa mtu mweusi uchawi kwa mafunzo maalumu akimdanganya ya kiimani.

Uchawi Afrika uliletwa na mzungu na ukweli huu haupingiki. ukiachana na hayo lakini pia upande wa maadili hapa nianze kwa salamu

U hai? ndugu hata kama haupo hai ila ukweli ukifikie huko huko ulipo. Nani aliyekuambia kuwa Afrika watu walikuwa wanavaa nguo full mwili mzima? Angalia wamasai japo na hao pia wamejaribu kubadilika. Ila hali ilikuwa mbaya sana zamani.

Watu walikuwa wanazuii tupu tu, Vikande vyote vya nyuma vilikuwa wazi na hakukuwa wa kushangaa katika hili kwa sababu ndiko tulikotoka. Ujio wa white man ukatibua hali ya hewa wakabadili,mtindo wa mavazi,dini, elimu, lugha, biashara na kila kitu.

Sasa katika mambo waliobadili pamoja na nidhamu na kusema nchi za Afrika hawajastarabika kwa sababu wanatembea uchi, wanaabudu madudu, wanaongea lugha chafu n.k. Watu wa Afrika walilazimishwa kukopi mila na mitindo yote ya Kizungu.

Unaposema vijana wetu hawana maadili ni kutukana wazee wetu wa zamani ambao walikuwa wanawinda,na kupiga ngoma uchi.

Hawa wapuuzi wa kizungu ndio walioita matabibu wetu kwa jina baya eti Matabibu wa kichawi(witch doctor) na wao kujiita Doctors, physician mara sijui wakemia n.k. Wakasema kupiga ngoma ni ushamba ila tupige miziki ya kisasa n.k.
Sioni jema la wazungu katika imani, wala tamaduni na wala technology kwa sababu naamini tungepigana na hali zetu. Wale wanaoenzi mababu zetu siku hizi wanajiita TIBA MBADALA sijui ndio nini.

Wajiite wauguzi na wataalamu wa tiba na magonjwa mbalimbali.

Afrika without White's countries is possible, hatujachelewa sana tuanze ku uphold vya kwetu ili vitusaidie na sisi kwa masilai yetu. Hivi vya kuletewa havitufai kwani "NGUO YA KUAZIMA HAISITIRI MA**KO" na ndio mana mambo hayaendi kama ilivyotakiwa.

Nawachukia wa Asia na dini zao i.e Christian and Muslims. Wewe ndugu yangu mtoto na mjuu wa Likangamai hayo mambo utayaweza? Ndiyo maana kulikuwa na mabala na aina ya watu na mila tofautitofauti, sasa ya nje ya nini na kuona kama vile ulichelewa kuvipata?

Kwani wao walikuwa hawajui kama Afrika kuna watu? mbona wamefika baada ya manyanyaso mauaji na dhulma kwa ndg zetu? Nini za Asia ni dini za ukweli kwa Asia na dini za Afrika ni za kweli kwa Afrika tu?

Jambo gani jema limewahi semwa na hao watu juu ya mababu zetu? wamewatukana sana kupitia imani zao na leo wamefanikisha kutufanya ndg,jamani tunaenda wapi na ilihali tunakotoka tunakudharau?

NAIPENDA AFRIKA SANA NA HATA NIKIWA JIRANI NA MZUNGU WOTE WE FEEL DIFFERENCES ON EACH AND EVERYTHING.RELIGION, LANGUAGE, STYLES,CUSTOMS, COLOUR, AWARENESS, ASSERTIVENESS STATUS, RECOGNITION e.t.c.
Ukweli haupingiki hata mniue hadi nife

TO MAKE THINGS VERY CLEAR

Wachangiaji wengi ambao hawakubaliani na mtazamo wa mada hii,hoja hii wamejikita kwenye mizimu. Naomba nifahamishe kwamba mizimu ni jina la MTU yeyote wa taifa lolote na Rangi yoyote aliyekufa na kuaminika bado anaishi katika hali ya gesi (invisible & intangible).

GHOST: the soul of a dead person thought of as living in an unseen world or asappearing to living people: .
Hivyo basis neno MIZIMU (GHOST) lisitumike tu negatively kuponda watu waliokufa Afrika.

Pia Milima, miti mikubwa, mapango etc kwa Afrika ilikuwa teknolojia pekee kwa wakati huo kama icon & symbol (alama) ya watu kukutana na siyo walikuwa wanaabudu hivyo vitu vilivyotajwa hapo na vifananavyo.

Watu walikuwa wanaomba Mungu kupitia waliotangulia kwani kwa nyakati hizo walikuwa kioo na dira pekee na walikuwa wanafanikisha kwa imani hiyo.

To be continued soon.
 
Mkuu
Tutakaokuelewa ni wachache sana humu, watu wengi walishafanyiwa kitu ninachookiita " kuuwawa kwa tabia zao halisi" Yaani karibu kila kitu hapa Afrika kimeharibiwa. Angalia maisha yetu, mathalani lugha zetu, mavazi yetu, sayansi yetu, dini zetu, usomaji wetu, majina yetu n.k hadi unajiuliza hivi sisi watu weusi tutaacha alama gani hapa duniani!!!???

Kuna jamaa mmoja nilimponda tukiwa wengi kwa kumwita mtoto wake mchanga jina la kiingereza la ajabu ajabu kisa tu eti ni zuri (si ni la kizungu bwana) nilipomwambia kuwa asiendekeze utumwa wa fikra aliniita mimi mshamba yaani akasema sijaelemika! Nikamtazamaaaa, nikamwambia waziwazi mimi naitwa TATA MKURIA na najisikia fahari kuwaita watoto wangu majina yao kama Bhoke, Ghati,Marwa, Mwita n.k.

Mkuu Frustration hakuna bara linadharauliwa kidini kama Afrika! Yaani ni aibu, halafu waafrika hawa wa sasa tena wasomi wanaendelea kuwatumikia wale jamaa wakidhani wapo sahihi yaani waafrika tumeenda hatua zaidi ya wao kujiona hizi dini zao ni bora sana hadi zinatugombanisha! Zinafanya tuuwane! Ni aibu.

Ukienda mabara mengine, huwaambii kitu kuhusu dini zao! Kama hujui nenda nchi za Ulaya, nenda nchi za Uarabuni, nenda Uhindini, nk. Ila sasa njoo Afrika! Yaani akili zetu ni nyepesi nyepesi mno. Kila kitu kinaaminika kirahisi tu, tumesoma sasa lakini bado tunaendekeza yale yale yaliyotuletea madhila siku za nyuma. Tumelala fofofo tunadhani kila kitu kipo sawa. Yaani hadi nimewakumbuka Prof Ngugi wa Thiong'o na maelekezo yake katika kitabu cha "Decolonizing the Mind" pamoja na Okoth p'Bitek na vile vitabu vyake pendwa (najua wengi mlisoma kile maarufu Song of Lawino na Song of Ocol) hawa waafrika wenzetu wametuandikia tushtuke kidogo lakini bado tupo ziii!

Wale wenzangu wanaopenda dini zetu, tuendelee nazo ingawa tunaitwa washirikina mi nasema ni sawa tu nitaendelea kutambika ila siyo kwa kafara za watu kama hawa washenzi wa baadhi ya dini hizi za kisasa wanavyofanya!

Najua tupo wengi tu ingawa makanisani na misikitini pia tunaingia mara kwa mara ila mioyoni mwetu tunaujua ukweli na pia tumeisha enda wapi na wapi kupata tiba zetu za kujikinga na mabalaa. Ukituona kwa nje tuna heshima lukuki katika jamii ila kiundani tunaamini dini za Kiafrika kimya kimya.

Tata mkuria.
 
kila siku watu wanajiuliza nani katuroga? hatujarogwa ila tumelaaniwa na mababu na miungu yetu kwa kuisaliti, kuikana na kiita 'imani potofu' kisha tumekumbatia miungu/mizimu ya kigeni. badala ya kuongea na 'mzimu' wa bibi yako anayekujua unakomaa na 'mzimu' wa bikira maria. Turudi kwenye njia zetu za mababu zetu.
 
tuendelee
Mkuu Tata, hata hao wazungu unaowalaumu walikua na dini zao kama ambavyo wafrika wanavyodai wana dini yao. Lakini swali la kujiuliza: je, ni dini ipi ya wafrika ambayo wafrika wanadai ni yao, ambayo wazungu hawakuwa nayo?

Kwa hakika hakuna dini kwa maana ya Mungu au miungu ambayo wafrika wanasema ni yao ambayo wazungu hawajakuwa nayo. Hakuna! Kama ni dini za uongo-miungu, wazungu ndiyo wameanza.

Kilichopo leo Afrika, ambacho wafrika wanadai kuwa ni dini yao na kuitumikia ni uongo. Kama ilivyo kwa wafrika nyakati zetu na hata mababu zetu waliotutangulia walikataa ukristo kwa uongo huo wa kuwa tuna dini yetu. Hata wazungu walikataa ukristo kwa madai, dhana na upotofu kama huu huu tulionao Afrika.

Shida kubwa ya Afrika ni elimu. Wafrika hatujawa na elimu. Hatuelewi dini ni nini, inaundwa na mini na ina sifa gani. Lakini pia wafrika siyo tu kwamba hatujaweza kuandika historia ya maisha ya vizazi vyetu, lakini hatuna elimu ya historia ya ulimwengu na mwanadamu.
Sasa kama hatuna tu elimu na uelewa wa jambo dogo la historia ya ulimwengu na maisha ya mwanadamu yalivyoanza itawezekanaje kwa jambo kama dini?
 
Hivi kwa nini dini za kiasili za kiafrika zilipondwa na wazungu, lakini wazungu hao hao hawakufaulu kuangamiza dini za kiasia.

Hinduism, Buddhism, Taoism, Shinto, nk yanalingana sana na dini ya kiafrika, kwenye kuabudu mizimu na sanamu, na zote zinastawi mpaka leo! Halafu wazungu wenyewe wanahamia dini kama Buddhism kwa kishindo siku hizi. Kwa nini dini za kiafrika zimepuuzwa, lakini dini za kiasia zinapanuka, wakati zote zinashabiana?
 
kila siku watu wanajiuliza nani katuroga? hatujarogwa ila tumelaaniwa na mababu na miungu yetu kwa kuisaliti, kuikana na kiita 'imani potofu' kisha tumekumbatia miungu/mizimu ya kigeni. badala ya kuongea na 'mzimu' wa bibi yako anayekujua unakomaa na 'mzimu' wa bikira maria. Turudi kwenye njia zetu za mababu zetu.
Eti Mungu mmoja alafu alikuwa anawapa utume watu wa Asia tu, si upuuzi huu jamani.
 
Hivi kwa nini dini za kiasili za kiafrika zilipondwa na wazungu, lakini wazungu hao hao hawakufaulu kuangamiza dini za kiasia. Hinduism, Buddhism, Taoism, Shinto, nk yanalingana sana na dini ya kiafrika, kwenye kuabudu mizimu na sanamu, na zote zinastawi mpaka leo! Halafu wazungu wenyewe wanahamia dini kama Buddhism kwa kishindo siku hizi. Kwa nini dini za kiafrika zimepuuzwa, lakini dini za kiasia zinapanuka, wakati zote zinashabiana?????
Dini ni technology kama technology ya ma flyover,madege matelephone,nadaraja etc, wao wamefanikiwa kiasi kikubwa ktk dini. Hii ni vita kuu nyingine ya dunia dhidi ya Afrika. Kwa nn makanisa na misikiti inaenea kwa kasi Afrika tu na sio kwingine?.
 
Mkuu Tata, hata hao wazungu unaowalaumu walikua na dini zao kama ambavyo wafrika wanavyodai wana dini yao. Lakini swali la kujiuliza: je, ni dini ipi ya wafrika ambayo wafrika wanadai ni yao, ambayo wazungu hawakuwa nayo?
Kwa hakika hakuna dini kwa maana ya Mungu au miungu ambayo wafrika wanasema ni yao ambayo wazungu hawajakuwa nayo. Hakuna!
Kama ni dini za uongo-miungu, wazungu ndiyo wameanza.
Kilichopo leo Afrika, ambacho wafrika wanadai kuwa ni dini yao na kuitumikia ni uongo. Kama ilivyo kwa wafrika nyakati zetu na hata mababu zetu waliotutangulia walikataa ukristo kwa uongo huo wa kuwa tuna dini yetu. Hata wazungu walikataa ukristo kwa madai, dhana na upotofu kama huu huu tulionao Afrika.
Shida kubwa ya Afrika ni elimu. Wafrika hatujawa na elimu. Hatuelewi dini ni nini, inaundwa na mini na ina sifa gani. Lakini pia wafrika siyo tu kwamba hatujaweza kuandika historia ya maisha ya vizazi vyetu, lakini hatuna elimu ya historia ya ulimwengu na mwanadamu.
Sasa kama hatuna tu elimu na uelewa wa jambo dogo la historia ya ulimwengu na maisha ya mwanadamu yalivyoanza itawezekanaje kwa jambo kama dini?
Unatililika kama desa hivi. Dini mfano za Asia huwa zinafanana karibia Asia yote na dini za Afrika nazo huwa zinafanana kwa kiasi kikubwa. Lakini dini za Asia hazifanani na dini za Afrika na hili limethibitishwa na kitendo cha dini za Asia kupiga ban dini za Afrika.

Elimu ipo pia ya aina nyingi ila ipi yenye nguvu ni ya Europe na hii haifanyi dunia kuwa elimu ya UINGEREZA ni elimu inayotumiwa na mataifa yote. Nchi za kiarabu wana utaratibu wao wa kusoma na hata Afrika kulikuwa na utaratibu wetu ambao kama usingevurugika na wapuuzi wale basi tungefikia hatua kama china.

China wao walijitenga na Uasia na kubaki wao kama wao, kwa kila kutu dini,lugha,mfumo wa elimu, biashara uongozi etc.

I sait it again that Africa without European was possible.
 
kila siku watu wanajiuliza nani katuroga? hatujarogwa ila tumelaaniwa na mababu na miungu yetu kwa kuisaliti, kuikana na kiita 'imani potofu' kisha tumekumbatia miungu/mizimu ya kigeni. badala ya kuongea na 'mzimu' wa bibi yako anayekujua unakomaa na 'mzimu' wa bikira maria. Turudi kwenye njia zetu za mababu zetu.
Mkuu umenena vema kabisa. Mimi kama wengi wetu humu tumezaliwa tukajikuta tumo ndani ya dini hizi za kigeni, tukaamini ndizo sahihi. Ila baadhi yetu baada ya kusoma na kudadisi nje ya box tumegundua kuna mambo hayahusiani na sisi watu weusi kabisa ila waliobaki kule kwenye hizo dini wamo wanakomaa ile mbaya! Ni uhuru wao hata siingilii!

Ni kweli laana za babu na bibi zetu zinatula ndani kwa ndani, acha nikupe mfano; dini mfano ya kikristo inafundisha kuwa watu wapendane mathalani biblia inasema tuwapende jirani zetu kama nafsi zetu wenyewe. Sasa ona kichekesho, waafrika hasa watanzania wanaosema wanampenda Mungu tena wasiyemjua wala hawajapata kumwona wao ndio wa kwanza kuwachukia wenzao! Yaani wanasali kinafki huku mioyoni mwao wanachuki kwa marafiki, ndugu na jamaa zao tena ambao wanaowaona kila siku. Jiulize inakuwaje wanasema wanampenda Mungu tena wasiyemwona! Sasa umeelewa kwa nini watu wanasema waafrika hatupendani! Tunaigiza sana hizi imani za watu!

Dini nyingi za kiafrika zinafanana na ni moja ya utambulisho wa mwafrika kama ilivyo kwa wazungu, wachina, waarabu, waamerika, wahindi na dini zao. Kuna haja ya waafrika kulitambua hili na kufanya bidii kuimarisha dini zetu. Tunaweza kabisa kuzifanya ziwe za kisasa na ikawa poa tu. Acha nikuchekeshe kidogo; siku za nyuma nilikuwa nasikiliza bbc swahili walikuwa wakiongelea juu ya wataalam fulani nchini Kenya waliiomba kufanya mbio za ushindani ( yaani kama marathon) wakiwa na wanyama wa mwitu kama fisi, viboko nk mida ya usiku ili watu waone walivyowataalam ila nasikia serikali iliwapiga stop, mi nadhani wangewabadilishia muda ikawa mchana ingependeza sana.
 
Ungeweka na rwference ya vitabu kusapoti argument yako ili kutupanua uelewa mkuu.Vinginevyo hii ni story tuu kama ile ya gazeti la Tanzanite
 
I say it again that Africa without European was possible. By mkuu Frustration
Kabisa mkuu absolutely! Ile issue ya kule Afrika Kusini ya waziri aliyependekeza pawepo na University ya Mambo ya Kiafrika uliisikia! Yaani iruhusu kila mwenye ujuzi wa mambo ya kiafrika apeleke ujuzi wake ili ufanywe technology ya mwafrika ila sijui hii iliishia wapi kwani alipingwa na waafrika wenyewe wakimwita mshirikina. Ila alikuwa na logic, ebu fikiri wale wanaopaa na ungo wakaitumia ile sayansi kwa manufaa na kikatengenezwa chombo kama ungo kusafirisha watu mchana kweupee tena kwa spidi kali! Mzungu si angejiona bado sana na ma boeing yake!? Ila nyie mnawaita wachawi wakifa na sayansi yao kwisha!
Someni kidogo issue ya Bsc in Witchcraft hapa chini.

Mfano mwingine hamkuwahi kusikia issue ya Mwanamalundi huyu ndugu yetu alikuwa na uwezo mbalimbali, mfano aliweza otesha mwembe kwa muda mfupi ukakua na kuzaa matunda na watu wakala maembe siku hiyo hiyo! Inapendeza enhe! Sasa sisi na dini za kigeni eti tunamwita witch-doctor au wizard! Yaani mwanasayansi mkubwa huyu ni witch-doctor au wizard! Wazungu bhana.... Tunajilaani wenyewe!
 
Katika kitu kigumu sana kufanya katika karne hii ni kumwambia & kumbadilisha mwafrika atoke kwenye mlengo wake wa mawazo uliopandikizwa na mzungu na kurudi kwenye mlengo huru.
Sio kila Mtu yupo free kuruhusu mawazo huru.....
 
Afrika ina dini ambazo ni nyingi sana kuliko bara lolote lile Duniani. Dini hizi nyingi zimepigwa ban na watu wa nje(whites) kwa sababu tu ya inferior ya mtu mweusi wa zamani. Kuishi kwa kumtegemea mzungu kwa kila kitu hadi ikapelekea hadi sasa watu wanategemea pia dini za kizungu.

Hakuna kabila hata moja Afrika ambalo limepoteza imani ya dini yao, ndio maana hata waendao makanisani hutembelea kwa mababu zao kupata kinga. Dini zote Afrika zilikuwa hazihusiani na uchawi ila mtu mweupe ndiye aliempa mtu mweusi uchawi kwa mafunzo maalumu akimdanganya ya kiimani.

Uchawi Afrika uliletwa na mzungu na ukweli huu haupingiki. ukiachana na hayo lakini pia upande wa maadili hapa nianze kwa salamu

U hai? ndugu hata kama haupo hai ila ukweli ukifikie huko huko ulipo. Nani aliyekuambia kuwa Afrika watu walikuwa wanavaa nguo full mwili mzima? Angalia wamasai japo na hao pia wamejaribu kubadilika. Ila hali ilikuwa mbaya sana zamani.

Watu walikuwa wanazuii tupu tu, Vikande vyote vya nyuma vilikuwa wazi na hakukuwa wa kushangaa katika hili kwa sababu ndiko tulikotoka. Ujio wa white man ukatibua hali ya hewa wakabadili,mtindo wa mavazi,dini, elimu, lugha, biashara na kila kitu.

Sasa katika mambo waliobadili pamoja na nidhamu na kusema nchi za Afrika hawajastarabika kwa sababu wanatembea uchi, wanaabudu madudu, wanaongea lugha chafu n.k. Watu wa Afrika walilazimishwa kukopi mila na mitindo yote ya Kizungu.

Unaposema vijana wetu hawana maadili ni kutukana wazee wetu wa zamani ambao walikuwa wanawinda,na kupiga ngoma uchi.

Hawa wapuuzi wa kizungu ndio walioita matabibu wetu kwa jina baya eti Matabibu wa kichawi(witch doctor) na wao kujiita Doctors, physician mara sijui wakemia n.k. Wakasema kupiga ngoma ni ushamba ila tupige miziki ya kisasa n.k.

Sioni jema la wazungu katika imani, wala tamaduni na wala technology kwa sababu naamini tungepigana na hali zetu. Wale wanaoenzi mababu zetu siku hizi wanajiita TIBA MBADALA sijui ndio nini. Wajiite wauguzi na wataalamu wa tiba na magonjwa mbalimbali.

Afrika without White's countries is possible, hatujachelewa sana tuanze ku uphold vya kwetu ili vitusaidie na sisi kwa masilai yetu. Hivi vya kuletewa havitufai kwani "NGUO YA KUAZIMA HAISITIRI MA**KO" na ndio mana mambo hayaendi kama ilivyotakiwa.

Nawachukia wa Asia na dini zao i.e Christian and Muslims. Ww ndugu yangu mtoto na mjuu wa Likangamai hayo mambo utayaweza? Ndio maana kulikuwa na mabala na aina ya watu na mila tofautitofauti, sasa ya nje ya nn na kuona kama vile ulichelewa kuvipata?

Kwani wao walikuwa hawajui kama Afrika kuna watu? mbona wamefika baada ya manyanyaso mauaji na dhulma kwa ndg zetu? Nini za Asia ni dini za ukweli kwa Asia na dini za Afrika ni za kweli kwa Afrika tu?

Jambo gani jema limewahi semwa na hao watu juu ya mababu zetu? wamewatukana sana kupitia imani zao na leo wamefanikisha kutufanya ndg,jamani tunaenda wapi na ilihali tunakotoka tunakudharau?

NAIPENDA AFRIKA SANA NA HATA NIKIWA JIRANI NA MZUNGU WOTE WE FEEL DIFFERENCES ON EACH AND EVERYTHING.RELIGION, LANGUAGE, STYLES,CUSTOMS, COLOUR, AWARENESS, ASSERTIVENESS STATUS, RECOGNITION e.t.c.

Ukweli haupingiki hata mniue hadi nife
Kwani dini za waafrika kabla ya wageni zilikuwa katika misingi gani ?
 
Kwani dini za waafrika kabla ya wageni zilikuwaje ?
Hivi kwa nini dini za kiasili za kiafrika zilipondwa na wazungu, lakini wazungu hao hao hawakufaulu kuangamiza dini za kiasia. Hinduism, Buddhism, Taoism, Shinto, nk yanalingana sana na dini ya kiafrika, kwenye kuabudu mizimu na sanamu, na zote zinastawi mpaka leo! Halafu wazungu wenyewe wanahamia dini kama Buddhism kwa kishindo siku hizi. Kwa nini dini za kiafrika zimepuuzwa, lakini dini za kiasia zinapanuka, wakati zote zinashabiana?????
 
I say it again that Africa without European was possible. By mkuu Frustration
Kabisa mkuu absolutely! Ile issue ya kule Afrika Kusini ya waziri aliyependekeza pawepo na University ya Mambo ya Kiafrika uliisikia! Yaani iruhusu kila mwenye ujuzi wa mambo ya kiafrika apeleke ujuzi wake ili ufanywe technology ya mwafrika ila sijui hii iliishia wapi kwani alipingwa na waafrika wenyewe wakimwita mshirikina. Ila alikuwa na logic, ebu fikiri wale wanaopaa na ungo wakaitumia ile sayansi kwa manufaa na kikatengenezwa chombo kama ungo kusafirisha watu mchana kweupee tena kwa spidi kali! Mzungu si angejiona bado sana na ma boeing yake!? Ila nyie mnawaita wachawi wakifa na sayansi yao kwisha!
Someni kidogo issue ya Bsc in Witchcraft hapa chini.
Mfano mwingine hamkuwahi kusikia issue ya Mwanamalundi huyu ndugu yetu alikuwa na uwezo mbalimbali, mfano aliweza otesha mwembe kwa muda mfupi ukakua na kuzaa matunda na watu wakala maembe siku hiyo hiyo! Inapendeza enhe! Sasa sisi na dini za kigeni eti tunamwita witch-doctor au wizard! Yaani mwanasayansi mkubwa huyu ni witch-doctor au wizard! Wazungu bhana.... Tunajilaani wenyewe!
Harry Potter angekuwa Afrika asinge fika alipofika, jiulize kwa nn anaigiza vile? Huku BASATA wasingemwacha ungesikia anaitwa kuhojiwa na kupigwa BAN.
Elimu yetu tunayoichukua inatujengea chuki dhidi yetu, Huwa nacheka sana kwa elimu zetu Afrika yaani sasa Afrika ni Kama Ulaya. Samaki haishi nchi kavu na bora akae kwenye mto mdogo kuliko kwenye bwawa kubwa la kufugwa. HANENEPI NG'OOOOOOOOOOO.
 
Katika kitu kigumu sana kufanya katika karne hii ni kumwambia & kumbadilisha mwafrika atoke kwenye mlengo wake aa mawazo uliopandikizwa na mzungu na kurudi kwenye mlengo huru.
Sio kila Mtu yupo free kuruhusu mawazl huru.....
Kama wezee walipinga hizi dini na wajukuu zao kwa kupewa mashati wakazikubali,basi na ss vitukuu tunaweza kuzikataa pia. Kama vipi waende huko Asia wakafanye dini hizi na kama kweli wapo sahihi. 4% Christian, 3% Muslims na hawa sio wote ambao kwa mafundisho yao wataenda sijui peponi mara mbinguni.

Jamani kwa hyo 97% to go in hell, how crazy it's? Basi nitamlaumu huyo mungu kwa nn aliniumba akijua naenda kuzaliwa sehemu ya Buddha,Hindu,Masai, etc.
 
Kwani dini za waafrika kabla ya wageni zilikuwa katika misingi gani ?
Inategemeana na Kabila lako,ongea na wazee watakupa dini na usipate tabu kwa sababu dini ni jina tu ila ni namna ya kufanikisha mambo kiimani na kiroho. Mfano mila ya mti aina ya Horo na matambiko. Mungu wa Afrika anapenda yale mambo na ndio maana akatuumba black. Miungu iligawana mabara sio kwa bahati mbaya kama udhaniavyo.
 
Kweli kabisa mkuu
Kama wezee walipinga hizi dini na wajukuu zao kwa kupewa mashati wakazikubali,basi na ss vitukuu tunaweza kuzikataa pia. Kama vipi waende huko Asia wakafanye dini hizi na kama kweli wapo sahihi. 4% Christian, 3% Muslims na hawa sio wote ambao kwa mafundisho yao wataenda sijui peponi mara mbinguni. Jamani kwa hyo 97% to go in hell, how crazy it's? Basi nitamlaumu huyo mungu kwa nn aliniumba akijua naenda kuzaliwa sehemu ya Buddha,Hindu,Masai, etc.
 
Back
Top Bottom