Victor wa happy
JF-Expert Member
- Apr 24, 2013
- 11,660
- 11,654
Hao wazungu na waarabu wametuharibia sana maisha yetu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Inategemeana na Kabila lako,ongea na wazee watakupa dini na usipate tabu kwa sababu dini ni jina tu ila ni namna ya kufanikisha mambo kiimani na kiroho. Mfano mila ya mti aina ya Horo na matambiko. Mungu wa Afrika anapenda yale mambo na ndio maana akatuumba black. Miungu iligawana mabara sio kwa bahati mbaya kama udhaniavyo.
Hao wazungu na waarabu wametuharibia sana maisha yetu
Umetumia kigezo gani kujua hili ?
Hakuna kitu nakichukia kama utumwa. Uwe ule wa kiuchumi, ule wa kiutamaduni, ule wa kisiasa na hata wa kifikra. Mtu mtumwa huonekana dhalili kabisa mbele ya mtwana. Mtwana humfanya atakavyo mtumwa wake! Ndio maana siku ikitokea mtwana kasafiri au kaondoka basi mtumwa ataiga ayafanyayo mtwana kama vile kujitupa katika kitanda cha mtwana, kuzungumza kwa kumwiga mtwana, kulia chakula vyombo vya mtwana n.k, n.k. Kitimtim ni pale atakapojua mtwana amerejea tena ghafla! Atakuwa na mashaka makubwa huyo!Hao wazungu na waarabu wametuharibia sana maisha yetu
Wameharibu mfumo mzima wa maisha yetu kuanzia kufikiri hadi tunavyokula
Afrika ina dini ambazo ni nyingi sana kuliko bara lolote lile Duniani. Dini hizi nyingi zimepigwa ban na watu wa nje(whites) kwa sababu tu ya inferior ya mtu mweusi wa zamani. Kuishi kwa kumtegemea mzungu kwa kila kitu hadi ikapelekea hadi sasa watu wanategemea pia dini za kizungu.
Hakuna kabila hata moja Afrika ambalo limepoteza imani ya dini yao, ndio maana hata waendao makanisani hutembelea kwa mababu zao kupata kinga. Dini zote Afrika zilikuwa hazihusiani na uchawi ila mtu mweupe ndiye aliempa mtu mweusi uchawi kwa mafunzo maalumu akimdanganya ya kiimani.
Uchawi Afrika uliletwa na mzungu na ukweli huu haupingiki. ukiachana na hayo lakini pia upande wa maadili hapa nianze kwa salamu
U hai? ndugu hata kama haupo hai ila ukweli ukifikie huko huko ulipo. Nani aliyekuambia kuwa Afrika watu walikuwa wanavaa nguo full mwili mzima? Angalia wamasai japo na hao pia wamejaribu kubadilika. Ila hali ilikuwa mbaya sana zamani.
Watu walikuwa wanazuii tupu tu, Vikande vyote vya nyuma vilikuwa wazi na hakukuwa wa kushangaa katika hili kwa sababu ndiko tulikotoka. Ujio wa white man ukatibua hali ya hewa wakabadili,mtindo wa mavazi,dini, elimu, lugha, biashara na kila kitu.
Sasa katika mambo waliobadili pamoja na nidhamu na kusema nchi za Afrika hawajastarabika kwa sababu wanatembea uchi, wanaabudu madudu, wanaongea lugha chafu n.k. Watu wa Afrika walilazimishwa kukopi mila na mitindo yote ya Kizungu.
Unaposema vijana wetu hawana maadili ni kutukana wazee wetu wa zamani ambao walikuwa wanawinda,na kupiga ngoma uchi.
Hawa wapuuzi wa kizungu ndio walioita matabibu wetu kwa jina baya eti Matabibu wa kichawi(witch doctor) na wao kujiita Doctors, physician mara sijui wakemia n.k. Wakasema kupiga ngoma ni ushamba ila tupige miziki ya kisasa n.k.
Sioni jema la wazungu katika imani, wala tamaduni na wala technology kwa sababu naamini tungepigana na hali zetu. Wale wanaoenzi mababu zetu siku hizi wanajiita TIBA MBADALA sijui ndio nini. Wajiite wauguzi na wataalamu wa tiba na magonjwa mbalimbali.
Afrika without White's countries is possible, hatujachelewa sana tuanze ku uphold vya kwetu ili vitusaidie na sisi kwa masilai yetu. Hivi vya kuletewa havitufai kwani "NGUO YA KUAZIMA HAISITIRI MA**KO" na ndio mana mambo hayaendi kama ilivyotakiwa.
Nawachukia wa Asia na dini zao i.e Christian and Muslims. Ww ndugu yangu mtoto na mjuu wa Likangamai hayo mambo utayaweza? Ndio maana kulikuwa na mabala na aina ya watu na mila tofautitofauti, sasa ya nje ya nn na kuona kama vile ulichelewa kuvipata?
Kwani wao walikuwa hawajui kama Afrika kuna watu? mbona wamefika baada ya manyanyaso mauaji na dhulma kwa ndg zetu? Nini za Asia ni dini za ukweli kwa Asia na dini za Afrika ni za kweli kwa Afrika tu?
Jambo gani jema limewahi semwa na hao watu juu ya mababu zetu? wamewatukana sana kupitia imani zao na leo wamefanikisha kutufanya ndg,jamani tunaenda wapi na ilihali tunakotoka tunakudharau?
NAIPENDA AFRIKA SANA NA HATA NIKIWA JIRANI NA MZUNGU WOTE WE FEEL DIFFERENCES ON EACH AND EVERYTHING.RELIGION, LANGUAGE, STYLES,CUSTOMS, COLOUR, AWARENESS, ASSERTIVENESS STATUS, RECOGNITION e.t.c.
Ukweli haupingiki hata mniue hadi nife
Hao wazungu na waarabu wametuharibia sana maisha yetu
Kwa hiyo wewe mwanaume mwenzangu sasa nyakati hizi Uko tayari kuvaa bikini za miti kama mababu zetu enzi hizo walivyokuwa wanavaa?
Usipo elewa-ukikosa elimu utaona dini ya Kristo ni kinyume na dini ya asili. Wafrika kwasababu ya kutokuwa na elimu na pia wao kwa wao yaani wafrika wenyewe kutofundishana kutoka kizazi hadi kizazi ndiyo maana, siyo nyakati zetu;wametuteka
Labda kwa mtazamo wako dini ni nini?Usipo elewa-ukikosa elimu utaona dini ya Kristo ni kinyume na dini ya asili. Wafrika kwasababu ya kutokuwa na elimu na pia wao kwa wao yaani wafrika wenyewe kutofundishana kutoka kizazi hadi kizazi ndiyo maana, siyo nyakati zetu; hata mababu waliotutangulia waliishi na kutumikia upotofu huu, ambao leo nasi tunaishi na kutumikia. Kudai kwamba wafrika tuna dini yetu ni upotofu unaotokana na ujinga, lakini pia unatokana na uzushi wa baadhi ya wafrika kwa kujua au kutojua wanawapotosha wafrika wenzao wengi (majority) kwa manufaa ya utawala na uchumi.
Unaposoma, unaposikia, unapojua au unapoelewa dini unakuwa unarejelea Mungu au miungu. Kwahiyo, dini ni mafundisho yote ya utaratibu wa mtu kuabudu Mungu au miungu,mafundisho ya maonyo na jinsi ya kuishi na kuenenda katika maisha.dini
Uko sahihi kwa mtazamo wako ila kwa mtazamo wangu naamini dini za mababu zetu na jinsi walivyoweza kufikisha matatizo yao kwa mungu wao na kuyatatua na hiyo ndo naita dini ya kiafrika.Unaposoma, unaposikia, unapojua au unapoelewa dini unakuwa unarejelea Mungu au miungu. Kwahiyo, dini ni mafundisho yote ya utaratibu wa mtu kuabudu Mungu au miungu,mafundisho ya maonyo na jinsi ya kuishi na kuenenda katika maisha.
Dini inaporejelea Mungu inarejelea ukweli-ndiye Mungu aliyeumba vitu vyote. Yeye ndiye mwanga, elimu, maarifa, maisha, uhai, usalama, uzima na umilele wa mtu.
Dini inaporejelea miungu inarejelea upotofu na uongo wa mtu kukataa ukweli na kuelekea uharibifu. Kwa kuishi miungu mtu anamkataa Mungu na hivyo ana haribu uhai, uzima, usalama, umilele na maisha yake yeye na wanaomfuata badae.
Dini ikirejelea Mungu inarejelea muumba wa vitu vyote na mwenye utaratibu na watu wenye kufanya tambiko wanayo sifa ya pekee inayowatofautisha na ndugu zao wengine.
Hakuwa kuwepo kwetu huku hata na sisi kulikuwa na watu wenye miujiza ya kugeuka mawe,mara kinu, mara mtoto na mbwembwe za kila aina,so Yesu kama alikuwepo hakuwepo hiyo ni imani yao na haituhusu kiongozi.Uko sahihi iwapo tu takribani miaka 2019 iliyopita, Yesu hakuwahi kuwepo Duniani, ila kama unakubali kuwa aliwahi kuwepo, basi wazungu wako sahihi zaidi ya 100%
Huyo labda atakuwa anatoka bara la Asia ila kama ni Afrika na ni mwafrika basi anatakiwa afanyiwe mila na desturi nyingi za kiafrika(dini ya Afrika). Anazungumza kwa kutumia maneno ya Asia huyo namwonea huruma sana kwani yy anafikili ni mueshia?Uko sahihi kwa mtazamo wako ila kwa mtazamo wangu naamini dini za mababu zetu na jinsi walivyoweza kufikisha matatizo yao kwa mungu wao na kuyatatua na hiyo ndo naita dini ya kiafrika.
Kabla ya kuingia wamisionari na waarabu Afrika na kuanza kuzieneza hizo dini zilizotupatia majina mazuri na ya kuvutia tulikuwa na utaratibu wetu na imani .
Mizimu haipo duniani ndg,mizimu ndio nn sasa.Mungu yupo,Mizimu ipo na Shetani yupo..
Dini ni kama daraja tu la kukufikisha kwa hivyo hapo juu nilivyotaja.
Dini inaweza kuwa batili kulingana na matakwa ya mtu..
Kama hautumii akili Dini itakuumiza.
Na kwa mujibu wa imani za Afrika wataadhibiwa vibaya sana.Hao wazungu na waarabu wametuharibia sana maisha yetu
Inaonekana hichi ulichokiandika huna elimu nacho.
Msingi wingi wake ni misingi,kwa maana ya haraka haraka juu yake kunajengwa mengine. Si kweli dini ni jina tu,ndio maana wewe leo hii ukajua dini si ada na desturi za watu. Kwa minajili hiyo dini ni zaidi ya hivyo unavyofikiria.
Umemgusia Mungu wa Afrika ni kwa waafrika,hili naomba unithibitishie na umejuaje kwamba Mungu wa Afrika ni tofauti na wa wazungu na mfano wake ?
Sasa kama Mungu wa wa afrika ni mmoja kwanini kila kabila lina dini yake kama ulivyoashiria huko juu ?
Ilikuwaje Miungu ikagawana mabara ? Hapa unatakiwa ujue kila jambo linataka elimu,sasa kama unaleta habari za kutunga na wasi wasi useme mapema,usije kushindwa kutetea hiki unachokisema.
Kama ulikubali ya kuwa uchawi uliletwa a wageni hasa wazungu kwanini unaleta uhusiano wa dini za kiafrika na matambiko ? Angalizo usijibu swali hili kama hujaelewa,usije kufanya kama kwenye swali langu la awali.
Nipo ....