Ukweli usiosemwa juu ya dini za Kiafrika

Unamjuaje? Ulishawahi muona?

Namjua kama alivyojielezea kwenye Qur'aan na hadithi za mtume amani ya Allah iwe juu yake.

Sijamuona. Na Allah anijaalie niwe miongoni mwa wale watakao muona bila ya pazia siku ya kiyama.
 
Namjua kama alivyojielezea kwenye Qur'aan na hadithi za mtume amani ya Allah iwe juu yake.

Sijamuona. Na Allah anijaalie niwe miongoni mwa wale watakao muona bila ya pazia siku ya kiyama.
Daaah!! Sasa hiyo Quran kaileta nani?
 
ndio maana nlimwambi anajificha kwa msitu wa karanga Kwa kuzania haonikani.
 
Allah aliye juu kupitia malaika wake mbora Jibril mpaka kwa mtume Muhammad amani ya Allah iwe juu yake.
Ila ww msaliti mkubwa, unakataa athiri yako? Eti malaika Jibril alileta, hizo ni mbwembwe tu ila ninavyokuona hujui kitu zaidi ya yale wanayokuambia
 
Namjua kama alivyojielezea kwenye Qur'aan na hadithi za mtume amani ya Allah iwe juu yake.
Sijamuona. Na Allah anijaalie niwe miongoni mwa wale watakao muona bila ya pazia siku ya kiyama.
Kiama ndio siku gani? Ww acha kupotoka hyo siku ni nadharia tu kama vile, vampire, zombie, dragon etc ila kiuhalisia havipo na havitakuwepo.
 
Kiama ndio siku gani? Ww acha kupotoka hyo siku ni nadharia tu kama vile, vampire, zombie, dragon etc ila kiuhalisia havipo na havitakuwepo.

Subiri iwadie uone kama ni nadharia.
 
Kuna wakati mtoto wangu aliwa form v alipata ugonjwa wa kuanguka. Nikaenda hospital, wakaniambia ana kifafa. Nikatibia weeeee wapi, nikabadilo gea hewani. Nikaenda kwa wazee wa mila, wakaniambia hakuna kifafa hapa. Kapigwa huyo(karogwa). Wakapambana nae weeeee, sasa hivi kapona.
Mwingine wakampiga kukojoa kitandani na wakampa uhanithi. Akawa na hali hiyo mpaka akiwa form 3. Nikapambana nae kwa wazeee weeee, sasa hivi hakojoe tena na mashine yake inasimama.
Tuzinduke wazeeeee.
Tuzindike
 
Wakuu
Nimekuwa nikifuatilia hii mada ingawa sijachangia kwa muda kidogo hii ni kutokana na majukumu ya kutafuta riziki. Ila nimesoma mijadala mbailmballi ambayo imechangiwa na inaendelea kuchangiwa na wakuu wote na nashukuru kuwa watu wameamka na wanaelewa umuhimu wa dini zetu za kiafrika. Sitaki kuelezea maana ya dini kwani mkuu Frustration ameilezea vizuri kabisa na wale wanaodhani kuwa dini ni kwenda kuabudu tu watakuwa wameelewa kuwa wanakosea kujua maana halisi ya dini.

Kama haujui, elewa tu kwamba dini inaingia sehemu zote za maisha ya mtu anayeiamini dini hiyo. Mifumo yote ya maisha hujengwa juu ya imani ya mtu ambayo imani hiyo ndiyo inayomuunganisha na dini fulani. Kwa maana hiyo usijiulize inakuwaje hapa Tanzania viongozi wa kisiasa au hata shughuli za mahakama ambako haki inapatikana wanaapa kwa katiba (kwa viongozi wa kisiasa) ila pia wanaapa kwa kupitia misahafu ya dini zao mathalani biblia na korani. Sasa usijiulize kwa nini imani hizi zinakubalika mahakamani au katika kuwaapisha viongozi wa kisiasa?

Hii ni kwa sababu kila dini ina utaratibu wake na watu wanaiheshimu na kuitii na kuifuata ni huo utii unaofanya mahakama na serikali iamini kwamba mtu anayeapa hataenda kinyume na taratibu hizo. Hii ina maana kwamba kiongozi atatekeleza kazi zake pasipo kuwanyanyasa wengine kwani atakuwa na hofu ya mungu, na kama ni mahakamani, mtu huyo hatasema uongo kwani atakaposema uongo imani yake itamsuta kwamba hayupo sahihi.

Nimeshangaa kumsoma mkuu mmoja humu ndani akisema kuwa dini za kiafrika zilikuwa dhaifu ndio maana zilianguka mbele ya dini za kigeni jambo ambalo si sahihi. Sipo kulaumu dini za kigeni zilizokuwa kizingiti kwa dini nyingi za kiafrika la hasha! Ninachotaka kuongelea ni namna dini hizi (za kigeni) zilivyojitahidi kwa makusudi kabisa kuwalaghai waafrika wengi ambao walikuwa na tamaduni imara na zenye nguvu hadi wakadharau dini zao na kuziona hazifai na wakalazimishwa kuzifuata dini hizi za kigeni na kuzipiga teke dini zao. Kitu kikubwa walichokifanya ni kuua fikra za mtu mweusi hasa hasa suala la kuwa alitoka wapi? Yeye ni nani na ana nafasi gani hapa duniani? Vitu anavyovifanya (namaanisha kiteknolojia) vina maana gani na ni imara kiasi gani hapa duniani?

Je rangi yake ni bora kiasi gani hapa duniani? Elimu yake ipoje? Na pia anachokiamini (namaanisha imani ya kiroho) ina msaidia nini? Maswali haya ni baadhi tu ya mambo ambayo mtu mweusi alipandikizwa katika fikra zake na karibu yote niliyoyataja ukiondoa lile la binadamu wa kwanza alikuwa sokwe na aliishi Afrika, yalikuwa yakimwonesha mtu mweusi si chochote kwa wageni waliokuja na taratibu akajikuta yeye mwenyewe akianza kuwatukuza wageni. Wale walioonekana kuwa ni wagumu, namaanisha falme au jamii imara kabisa zilizoshikilia na kuamini taratibu zao za maisha, walijengewa shule ndani ya shule unapata kuna elimu ya dini ndani yake yaani elimu na sala!

Najua unajua hizi shule zilifanya nini kwa watoto wa kiafrika baada ya kuwa wamepata elimu za kigeni. Wengi walizidharau mila na desturi zetu na kuona hazifai, wakawadharau wazazi wao, ndugu na jamaa zao, marafiki zao, n.k. Mnaweza kunambia yale maeneo ambayo watu wake walipata elimu hizi hasa hapa Tanzania wapoje hadi leo? Mfumo wao wa siasa ulikuwaje kipindi hicho? Rejeeni maeneo ambako mnajua shule kongwe zilijengwa.

Kusema kuwa chako ni kizuri na kinakufaa si jambo baya, hata kama ni kidogo bado ni chako. Lazima ukienzi na kukitukuza. Taratibu tutayarudisha yale mazuri ambayo dini zetu ziliyafanya. Tunajua sasa kuwa dini ni mfumo mzima wa maisha unaingia kila sehemu. Nchi nyingi za kiafrika zinapata taabu sana kuendeleza mifumo ya kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni kwa sababu tu tulitupa vya kwetu. Najua taratibu lakini kwa uhakika tutapata namna ya kurekebisha kasoro zetu ili tuifanye Afrika yenye furaha na amani tele. Kwa kutumia fikra zetu walitudhoofisha na kwakumia fikra zetu tutaondoa huo udhoofu.

Asanteni.
 
Allah aliye juu kupitia malaika wake mbora Jibril mpaka kwa mtume Muhammad amani ya Allah iwe juu yake.
Sasa ndugu utajuaje kama hayo unayoyasema ni kweli na siyo porojo za watu fulani wanaotazama manufaa yao binafsi ?
 
Kama unaelimu waweza eleza dini nn?!

Unauhakika waafrika hatuna dini??
 
Kama unaelimu waweza eleza dini nn?!

Unauhakika waafrika hatuna dini??
Mkuu zinginary
Nimemshangaa sana huyu mkuu mwenzetu. Yeye anadhani dini ni ibada tu, asome post yangu #175 ili aelewe vema kuwa Afrika ilikuwa na dini tena imara kuliko za hao wageni.
 
Mkuu
Jibu lake ni jepesi tu, tuna usemi mmoja maarufu unaosema "mti wenye matunda ndio hutupiwa mawe" Sote tunajua kuwa hawa wazungu walipofika Afrika walikutana na tamaduni zilizokuwa ngumu kuvunjika ilihali wamezungukwa na utajiri mkubwa mno! Wenzetu ni wajanja wajanja sana na walijua kabisa utajiri tuliokuwa nao si wakuisha mapema, namaanisha ni wa muda mrefu hapa duniani. Kwa maana hiyo ili kuumiliki kwa muda mrefu ni kuhakikisha mfumo wa maisha wa kiafrika unavurugwa kwa kiasi kikubwa kama namna pekee ya kuhakikisha wanaupata utajiri wetu kwa muda mrefu na unaona wamefanikiwa hadi leo.

Sasa nadhani umepata picha kwa nini leo hii kuna mwafrika anaitwa Bob Jimmy ilihali ni black kama mimi, hili jina ukiliona tu waweza dhani ni mzungu kumbe ni ngozi nyeusi! Unadhani ukienda ulaya tuseme labda ukaishi mji kama Manchester mtaa wa Canal ukakuta kuna mtu anaitwa Bob Jimmy (ni mwafrika huyu) katika mtaa huo utamfuatilia kweli? Vipi ukikuta jina la Tata Mkuria mtaa huo! Najua lazima umtafute mfahamiane vizuri kwani hili ni jina la kiafrika na inawezekana kabisa huyu mtu ni mweusi mwenzio. Katika kufahamiana mtajenga mawasiliano ambayo yatawasaidia kuimarisha udugu wenu. Mzungu hataki haya yatokee ndio maana alishaua uafrika wetu kupitia mifumo hii ya kidini.
Mkuu nadhani kidogo umeelewa kwa nini dini zingine duniani zinaendelea na si za kiafrika.
 
Unachosema mkuu, ni Wazungu waliponda dini za kiafrika kwa lengo ya kutudhoofisha ili waweze kututawala na kukalia utajiri mkubwa uliopo hapa Afrika. Lakini kule Asia pia walitawala kwa lengo hii tu na kwa muda mrefu zaidi kuliko hapa Afrika, na hawakufaulu kusambaratisha dini za pale. Swali ni kwa nini dini za kiafrika zilipotea na dini za kiasia zilisimama imara mbele ya dini za wageni???!

Ninavyoona mimi, waasia walijitawala muda mrefu kabla kuingia wazungu na walijenga institutions (taasisi) yakusimamia dini zao. Baada ya mzungu kupokonya utawala, hizi institutions ziliendelea kuprotect wafuasi kutoka foreign influences. Institutions hizi zilihami mila, desturi na utamaduni za asili za Asia.
Hata leo hii nchi zenye utawala bora duniani wamewekeza zaidi kwenye kuimarisha taasisi zao za kusimamia haki na maendeleo ya raia. Ni vigumu sana kwa dictator kuvuruga mfumo kwenye nchi zenye taasisi imara!!!

Kwetu sisi hizi institutions zilikuwa hazipo na ilikuwa rahisi mno kutuvuruga na kutuchanganya. Halafu silaha aliyotumia mzungu kutuangamiza ilikuwa kali mno - ELIMU!!! Alipigania kutawala fikra zetu, na pole pole kadri tulivyoelimika tukaachana na mila na desturi za mababu zetu! Bila ya kuwa na taasisi za kulinda dini zetu za asili, hatukupata mwongozo jinsi ya kukabiliana na dini hii ya wageni. Halafu ya pili, hatukuwa na umoja baina ya makabila. Mzungu alitumia "divide and rule" kuchonganisha kabila mmoja dhidi ya nyingine. Wazungu hawakuleta majeshi makubwa hapa, walitupiganisha sisi kwa sisi. Kukosekana kwa umoja pia ilisababisha dini zetu kupotea. Hatukuweza kusema kwa sauti mmoja - Dini za wageni hatuzitaki!!

Sasa nini kifanyike kurejesha dini za kiafrika???? Changamoto ni kubwa sana. Ingawa kuna juhudi za watu hapa na pale, kuanzisha dini za kiafrika kama Ubuntu (SA), Kwanzaa (USA), nk impact zao na rate of conversion ni ndogo sana. Hii ni kwa sababu mzungu amejenga bad image ya dini ya waafrika - uchawi, ushirikina, mizimu, kafara za damu, nk. Wanachokifanya ni kuunganisha dini za wageni na za kiasili yaani dini ya kichotara. Inahitajika a charismatic leader mwenye elimu nzuri ya dini za kiafrika pamoja na institutions madhubuti yatakayo fanya research and development ya dini za asili.
 
Kama umeamua kumpinga mzungu basi mpinge kwa kila kitu... ni sawa na kuchagua dhambi.

Unakataa mavazi yao ila unatumia smartphone zao na kupost jf
 
Napenda namma unavyonena kiuhalisia na kwa mifano hai. Ndg yangu hata wanaojifanya wafia dini za wenzio pia ndani ya nafsi yao wanajua kuwa kuna mambo yapo chini ya kapeti na wanayafanya kila siku. Jiulize kwa nn wazee wote wanaenzi mila ila ss vijana ambao ni taifa la kesho wao wanapinga na kupuuza mila?.
 
 
Kama unaelimu waweza eleza dini nn?!
Unauhakika waafrika hatuna dini??
Huyo anatoa tafsiri ya dini kwa kuegemea mtazamo wa dini za Asia. Watapata tabu sana na dini za watu wa nje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…