Ukweli usiosemwa juu ya dini za Kiafrika

Mkuu
Jibu lake ni jepesi tu, tuna usemi mmoja maarufu unaosema "mti wenye matunda ndio hutupiwa mawe" Sote tunajua kuwa hawa wazungu walipofika Afrika walikutana na tamaduni zilizokuwa ngumu kuvunjika ilihali wamezungukwa na utajiri mkubwa mno! Wenzetu ni wajanja wajanja sana na walijua kabisa utajiri tuliokuwa nao si wakuisha mapema, namaanisha ni wa muda mrefu hapa duniani. Kwa maana hiyo ili kuumiliki kwa muda mrefu ni kuhakikisha mfumo wa maisha wa kiafrika unavurugwa kwa kiasi kikubwa kama namna pekee ya kuhakikisha wanaupata utajiri wetu kwa muda mrefu na unaona wamefanikiwa hadi leo.
Sasa nadhani umepata picha kwa nini leo hii kuna mwafrika anaitwa Bob Jimmy ilihali ni black kama mimi, hili jina ukiliona tu waweza dhani ni mzungu kumbe ni ngozi nyeusi! Unadhani ukienda ulaya tuseme labda ukaishi mji kama Manchester mtaa wa Canal ukakuta kuna mtu anaitwa Bob Jimmy (ni mwafrika huyu) katika mtaa huo utamfuatilia kweli? Vipi ukikuta jina la Tata Mkuria mtaa huo! Najua lazima umtafute mfahamiane vizuri kwani hili ni jina la kiafrika na inawezekana kabisa huyu mtu ni mweusi mwenzio. Katika kufahamiana mtajenga mawasiliano ambayo yatawasaidia kuimarisha udugu wenu. Mzungu hataki haya yatokee ndio maana alishaua uafrika wetu kupitia mifumo hii ya kidini.
Mkuu nadhani kidogo umeelewa kwa nini dini zingine duniani zinaendelea na si za kiafrika.
Hakika kabisa! mfumo wa majina pia unaathari kwa namna moja au nyingine na ndio maana kupitia majina wanaweza jua dini zao zinanguvu kiasi gani.

Siku hizi kuna kubadili majina ya asili kwa mfano, wanaojifanya waisilamu wao kipindi cha jando jina wanabadili kama alipewa jina la kiafrika. Wakristo nao pia ili abatizwe basi lazima awe na jina la Asia. Hawajiulizi kunamahusiano gani kati ya jina na imani ya mtu ila wameziba masikio kwa imani potofu ya uisilamu au ukristo. Na tatitizo la sasa kwa nchi za Afrika ni dini na hawataweza badili mfumo wa elimu hadi pale mifumi ya dini za wazungu ambazo zinanufaika na mfumo wa elimu uliyopo, zitakapo futwa na kutokomezwa kabisa Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Mfumo uliopo ni mfumo unaowajenga watanzania kuwa tegemezi kwa wazungu na kuendelea kutunyonya. Dini zilizopo zinapingana na mfumo wa uchumi wa Afrika na ndio chanzo kikuu cha kudorora. Ufisadi, Rushwa, Wizi wa mali za uma n. k zinafanyika kupitia migongo ya ibada
 
Unachosema mkuu, ni Wazungu waliponda dini za kiafrika kwa lengo ya kutudhoofisha ili waweze kututawala na kukalia utajiri mkubwa uliopo hapa Afrika. Lakini kule Asia pia walitawala kwa lengo hii tu na kwa muda mrefu zaidi kuliko hapa Afrika, na hawakufaulu kusambaratisha dini za pale. Swali ni kwa nini dini za kiafrika zilipotea na dini za kiasia zilisimama imara mbele ya dini za wageni???! Ninavyoona mimi, waasia walijitawala muda mrefu kabla kuingia wazungu na walijenga institutions (taasisi) yakusimamia dini zao. Baada ya mzungu kupokonya utawala, hizi institutions ziliendelea kuprotect wafuasi kutoka foreign influences. Institutions hizi zilihami mila, desturi na utamaduni za asili za Asia. Hata leo hii nchi zenye utawala bora duniani wamewekeza zaidi kwenye kuimarisha taasisi zao za kusimamia haki na maendeleo ya raia. Ni vigumu sana kwa dictator kuvuruga mfumo kwenye nchi zenye taasisi imara!!!
Kwetu sisi hizi institutions zilikuwa hazipo na ilikuwa rahisi mno kutuvuruga na kutuchanganya. Halafu silaha aliyotumia mzungu kutuangamiza ilikuwa kali mno - ELIMU!!! Alipigania kutawala fikra zetu, na pole pole kadri tulivyoelimika tukaachana na mila na desturi za mababu zetu! Bila ya kuwa na taasisi za kulinda dini zetu za asili, hatukupata mwongozo jinsi ya kukabiliana na dini hii ya wageni. Halafu ya pili, hatukuwa na umoja baina ya makabila. Mzungu alitumia "divide and rule" kuchonganisha kabila mmoja dhidi ya nyingine. Wazungu hawakuleta majeshi makubwa hapa, walitupiganisha sisi kwa sisi. Kukosekana kwa umoja pia ilisababisha dini zetu kupotea. Hatukuweza kusema kwa sauti mmoja - Dini za wageni hatuzitaki!!
Sasa nini kifanyike kurejesha dini za kiafrika???? Changamoto ni kubwa sana. Ingawa kuna juhudi za watu hapa na pale, kuanzisha dini za kiafrika kama Ubuntu (SA), Kwanzaa (USA), nk impact zao na rate of conversion ni ndogo sana. Hii ni kwa sababu mzungu amejenga bad image ya dini ya waafrika - uchawi, ushirikina, mizimu, kafara za damu, nk. Wanachokifanya ni kuunganisha dini za wageni na za kiasili yaani dini ya kichotara. Inahitajika a charismatic leader mwenye elimu nzuri ya dini za kiafrika pamoja na institutions madhubuti yatakayo fanya research and development ya dini za asili.
Kurudisha dini zetu ni kazi ngumu ila inawezekana.
 
Ni vizuri tukawa wakweli. Siyo vema kusema na kufundisha opotofu. Ni dini gani ambayo unasema wafrika walikuwa nayo ambayo wazungu hawajawa nayo katika historia? Iseme hapa!
Mkuu
Mimi sifundishi upotofu kama unavyodai. Dini za wazungu na dini za waafrika zina utofauti mkuu. Hakuna sehemu ambayo nimesema kuhusu dini ambayo waafrika walikuwa nayo na wazungu hawakuwa nayo. Ebu pitia hapa chini ili uone habari za dini za kiafrika;

"Dini asilia za Kiafrika ni kati ya dini za jadi ambazo zinadumu hata leo, ingawa wafuasi wake wanapungua mwaka hadi mwaka kulingana na dini zilizotokea Mashariki ya Kati, hasa Ukristo na Uislamu, ambazo zinazidi kuenea barani Afrika.

Dini za Kiafrika zinafuata imani maalumu, sawa kabisa na hizo za nchi za ughaibuni ambazo zimeleta mfumo mpya wa kuabudu. Badala ya kuabudia mapangoni au misituni kama Waafrika walio wengi walivyofanya kwa karne nyingi, zimehimiza kujenga makanisa na misikiti kwa ajili ya kumwabudu Mungu kadiri ya ufunuo wake mwenyewe.

Madhehebu mengi ya Kikristo yamekuwa yakimuabudu Mungu kwa kushirikiana na wafu wanaoheshimiwa kama watakatifu, wakati Waafrika tangu zamani waliwaenzi wazee wao waliokufa na kuwaita mizimu. Waafrika hao tangu zamani waliwaheshimu wafu kwenye makaburi yao, lakini baadhi ya Wakristo waliwaheshimu wafu kanisani kwa sala zao pamoja na kusujudu pengine masalia au picha za hao wafu.

Katika Amri Kumi za Biblia, Waafrika kwa jumla walikuwa nazo hata kabla ya kuja kwa Wazungu: walijua kwamba imewapasa kuwaheshimu wazazi wao, kutoua, kutoiba wala kufanya kinyume na maagizo ya wazee wao.

Pamoja na hayo yote, bado baadhi ya makabila yanaendelea na mila zao za kuheshimu wafu ingawa dini zenye asili ya Mashariki ya Kati zinakataza namna hiyo"

Anyway sijajua unataka nikujibu nini, naomba utuwekee hiyo historia hapa tuipitie tafadhali.
 
Hakuwa kuwepo kwetu huku hata na sisi kulikuwa na watu wenye miujiza ya kugeuka mawe,mara kinu, mara mtoto na mbwembwe za kila aina,so Yesu kama alikuwepo hakuwepo hiyo ni imani yao na haituhusu kiongozi.

Nabii K.Ngwale, Mkwawa, Mangungo,e.t.c. walikuwepo ila sisi tuliwaita viongozi wao wakawaita mitume na manabii. Wao waliamini uwezo wa Yesu/Muhammad ulitokana na Mungu wao na sisi tuliamini akina Kinjeketile walipewa uwezo wa ziada na Mungu wetu.
Au unafikili wale walitwaa wapi ule uwezo? na kama hapakuwahi tokea mtu nyuma yao i.e Baba,babu,mama,bibi, etc. Mungu wetu aliwainua ili kuleta mwanga na ukombozi katika bara letu. Ndio maana shida za Afrika ni the same but zipo tofauti sana na mabara mengine.
sasa dunian kote history inaonyesha ni kwel yesu alikuwe[po...ebu jiulize kwann miaka inaadikwa bc ..before christ?????
 
Hivi kwa dunia ilipofika hapa kweli tunaweza kuanza kufuata imani za mababu walizokuwa wakizifuata enzi hizo? Kama sasa tu watu wanaacha kufuata hizi dini zilizopo ambazo zinaitwa za kuletewa je kipi cha kuwafanya wazigeukie hizo imani za mababu? Ni wazi lazima kuwe na sababu za msingi zenye kuwafanya watu waone imani hizo ndio zafaa kufuata na kuacha.

Leo watu wamefikia kushindanisha maelezo ya kisayansi na maelezo ya hizi dini za kuletewa,je imani za mababu(dini za afrika) zinaweza kuingia hapo? Maana mambo yanabadilika hoja za kwamba wazee waliomba mvua zikaja sidhani kama yana nafasi enzi hizi.
 
Wanaposena jongea meza ya bwana usiyemjua, wewe mwafrika jongea kwenye kilinge chako cha asili
 
Sisi wenye Afro-centric views tunapigwa vita sana na hawa hawa Waafrika wenzetu,yaani sisi Waafrika nikama tuna laana
Adui wa pili wa Afrika baada ya whites ni Waafrika wenyewe. Tambua hill nchi kama Algeria,misri,Angola etc ni sehemu ya whites.
 
Mkuu
Mimi sifundishi upotofu kama unavyodai. Dini za wazungu na dini za waafrika zina utofauti mkuu. Hakuna sehemu ambayo nimesema kuhusu dini ambayo waafrika walikuwa nayo na wazungu hawakuwa nayo. Ebu pitia hapa chini ili uone habari za dini za kiafrika;
"Dini asilia za Kiafrika ni kati ya dini za jadi ambazo zinadumu hata leo, ingawa wafuasi wake wanapungua mwaka hadi mwaka kulingana na dini zilizotokea Mashariki ya Kati, hasa Ukristo na Uislamu, ambazo zinazidi kuenea barani Afrika.
Dini za Kiafrika zinafuata imani maalumu, sawa kabisa na hizo za nchi za ughaibuni ambazo zimeleta mfumo mpya wa kuabudu. Badala ya kuabudia mapangoni au misituni kama Waafrika walio wengi walivyofanya kwa karne nyingi, zimehimiza kujenga makanisa na misikiti kwa ajili ya kumwabudu Mungu kadiri ya ufunuo wake mwenyewe.
Madhehebu mengi ya Kikristo yamekuwa yakimuabudu Mungu kwa kushirikiana na wafu wanaoheshimiwa kama watakatifu, wakati Waafrika tangu zamani waliwaenzi wazee wao waliokufa na kuwaita mizimu. Waafrika hao tangu zamani waliwaheshimu wafu kwenye makaburi yao, lakini baadhi ya Wakristo waliwaheshimu wafu kanisani kwa sala zao pamoja na kusujudu pengine masalia au picha za hao wafu.
Katika Amri Kumi za Biblia, Waafrika kwa jumla walikuwa nazo hata kabla ya kuja kwa Wazungu: walijua kwamba imewapasa kuwaheshimu wazazi wao, kutoua, kutoiba wala kufanya kinyume na maagizo ya wazee wao.
Pamoja na hayo yote, bado baadhi ya makabila yanaendelea na mila zao za kuheshimu wafu ingawa dini zenye asili ya Mashariki ya Kati zinakataza namna hiyo"
Anyway sijajua unataka nikujibu nini, naomba utuwekee hiyo historia hapa tuipitie tafadhali.
Tata thank you so much kwa maelezo yako na unaweza ongeza nyama kwenye Uzi huu usisubiri kujibu tu. Nafikiri unavitu Vinci ambavyo watu wanatakiwa kujua.
 
Hivi kwa dunia ilipofika hapa kweli tunaweza kuanza kufuata imani za mababu walizokuwa wakizifuata enzi hizo? Kama sasa tu watu wanaacha kufuata hizi dini zilizopo ambazo zinaitwa za kuletewa je kipi cha kuwafanya wazigeukie hizo imani za mababu? Ni wazi lazima kuwe na sababu za msingi zenye kuwafanya watu waone imani hizo ndio zafaa kufuata na kuacha.
Leo watu wamefikia kushindanisha maelezo ya kisayansi na maelezo ya hizi dini za kuletewa,je imani za mababu(dini za afrika) zinaweza kuingia hapo? Maana mambo yanabadilika hoja za kwamba wazee waliomba mvua zikaja sidhani kama yana nafasi enzi hizi.
Wazee kuomba mvua na kunyesha ni ushahidi kuwa mababu zetu walikuwa kwenye right truck.
 
Back
Top Bottom