Ukweli usiosemwa juu ya dini za Kiafrika

Ukweli usiosemwa juu ya dini za Kiafrika

Ufafanuzi : unapoenda kanisani unaambiwa jongea meza ya bwana (karibia meza ya bwana) altare ni meza ya bwana. Nauliza wewe mwafrika hukuwa na kilinge ?(sehemu ya kufanyia tambiko) Imarisha kilinge chako achana na utamaduni wa wazungu. Mf. Ukame umeingia, wewe ingia altareni kuomba mvua Nani niingie kwenye kilinge changu tuone nani zaidi. Mila zetu ni kila kitu sema tunazipuuza kwa uzuzu wetu.
 
Kuna vitu viwili kama sio vitatu vinavyoitafuna Africa mpaka Yesu anarudi.
1. Dini: sisi waafrika ndo tunaongoza kwa kufia Dino (die hards) na hii ni kuwa wabishi Wa kuelewa mambo hasa hasa historia za koo na mila zetu jwa undani. Mstari huo huo Wa Biblia alioutumia mkoloni kukufanyia wizi na dhuluma ndo tunautumia huo huo kwenye kuleta umoja ndani yetu. Watu wamekuwa Radicals mpaka tunawashinda waliotuletea dini.

2. Documentation: hii inajumuisha kila kitu kuanzia historia mpaka namna ya kufanya interaction na maandiko. Mzungu anaanza kuandika kutoka kushoto kwenda kulia. Mwarabu anatoka kulia kwenda kushoto.

Je ni kweli Africa hatukuwa na namna yetu ya kuweka maandishi? Ukihoji utaishia kupewa jina la mbumbumbu au mjinga. Documentation imeikandamiza sana Africa. Unataka kusema kuwa hakuna kitu kizuri ambacho Mwafrika amekifanya? Je kwanini baadhi ya Mashujaa Wa kiafrika hawaonekani kwenye historia?

Mungu ibariki Africa aisee maana tusiposhtuka utakuta hata maisha yetu ni maisha yao.
 
Ulivyotaja mwita.. Hapo mwita ana mtoto wa kike nataka kuja kumuoa[emoji3]
Mkuu
Tutakaokuelewa ni wachache sana humu, watu wengi walishafanyiwa kitu ninachookiita " kuuwawa kwa tabia zao halisi" Yaani karibu kila kitu hapa Afrika kimeharibiwa. Angalia maisha yetu, mathalani lugha zetu, mavazi yetu, sayansi yetu, dini zetu, usomaji wetu, majina yetu n.k hadi unajiuliza hivi sisi watu weusi tutaacha alama gani hapa duniani!!!???

Kuna jamaa mmoja nilimponda tukiwa wengi kwa kumwita mtoto wake mchanga jina la kiingereza la ajabu ajabu kisa tu eti ni zuri (si ni la kizungu bwana) nilipomwambia kuwa asiendekeze utumwa wa fikra aliniita mimi mshamba yaani akasema sijaelemika! Nikamtazamaaaa, nikamwambia waziwazi mimi naitwa TATA MKURIA na najisikia fahari kuwaita watoto wangu majina yao kama Bhoke, Ghati,Marwa, Mwita n.k.

Mkuu Frustration hakuna bara linadharauliwa kidini kama Afrika! Yaani ni aibu, halafu waafrika hawa wa sasa tena wasomi wanaendelea kuwatumikia wale jamaa wakidhani wapo sahihi yaani waafrika tumeenda hatua zaidi ya wao kujiona hizi dini zao ni bora sana hadi zinatugombanisha! Zinafanya tuuwane! Ni aibu.

Ukienda mabara mengine, huwaambii kitu kuhusu dini zao! Kama hujui nenda nchi za Ulaya, nenda nchi za Uarabuni, nenda Uhindini, nk. Ila sasa njoo Afrika! Yaani akili zetu ni nyepesi nyepesi mno. Kila kitu kinaaminika kirahisi tu, tumesoma sasa lakini bado tunaendekeza yale yale yaliyotuletea madhila siku za nyuma. Tumelala fofofo tunadhani kila kitu kipo sawa. Yaani hadi nimewakumbuka Prof Ngugi wa Thiong'o na maelekezo yake katika kitabu cha "Decolonizing the Mind" pamoja na Okoth p'Bitek na vile vitabu vyake pendwa (najua wengi mlisoma kile maarufu Song of Lawino na Song of Ocol) hawa waafrika wenzetu wametuandikia tushtuke kidogo lakini bado tupo ziii!

Wale wenzangu wanaopenda dini zetu, tuendelee nazo ingawa tunaitwa washirikina mi nasema ni sawa tu nitaendelea kutambika ila siyo kwa kafara za watu kama hawa washenzi wa baadhi ya dini hizi za kisasa wanavyofanya!

Najua tupo wengi tu ingawa makanisani na misikitini pia tunaingia mara kwa mara ila mioyoni mwetu tunaujua ukweli na pia tumeisha enda wapi na wapi kupata tiba zetu za kujikinga na mabalaa. Ukituona kwa nje tuna heshima lukuki katika jamii ila kiundani tunaamini dini za Kiafrika kimya kimya.

Tata mkuria.
 
Ufafanuzi : unapoenda kanisani unaambiwa jongea meza ya bwana (karibia meza ya bwana) altare ni meza ya bwana. Nauliza wewe mwafrika hukuwa na kilinge ?(sehemu ya kufanyia tambiko) Imarisha kilinge chako achana na utamaduni wa wazungu. Mf. Ukame umeingia, wewe ingia altareni kuomba mvua Nani niingie kwenye kilinge changu tuone nani zaidi. Mila zetu ni kila kitu sema tunazipuuza kwa uzuzu wetu.
Ahsante kwa ufafanuzi wako nà sasa nimekupata. Kila kitu wanachofanya makanisani au misikitini kinaendana na Afrika ila kwa kuwa saizi sema wame centralize basi wanajiona wamefika. Mm sioni sababu ya kuendelea kukumbatia vya watu.
 
Kuna vitu viwili kama sio vitatu vinavyoitafuna Africa mpaka Yesu anarudi.
1. Dini: sisi waafrika ndo tunaongoza kwa kufia Dino (die hards) na hii ni kuwa wabishi Wa kuelewa mambo hasa hasa historia za koo na mila zetu jwa undani. Mstari huo huo Wa Biblia alioutumia mkoloni kukufanyia wizi na dhuluma ndo tunautumia huo huo kwenye kuleta umoja ndani yetu. Watu wamekuwa Radicals mpaka tunawashinda waliotuletea dini.
2. Documentation: hii inajumuisha kila kitu kuanzia historia mpaka namna ya kufanya interaction na maandiko. Mzungu anaanza kuandika kutoka kushoto kwenda kulia. Mwarabu anatoka kulia kwenda kushoto. Je ni kweli Africa hatukuwa na namna yetu ya kuweka maandishi? Ukihoji utaishia kupewa jina la mbumbumbu au mjinga. Documentation imeikandamiza sana Africa. Unataka kusema kuwa hakuna kitu kizuri ambacho Mwafrika amekifanya? Je kwanini baadhi ya Mashujaa Wa kiafrika hawaonekani kwenye historia?
Mungu ibariki Africa aisee maana tusiposhtuka utakuta hata maisha yetu ni maisha yao.
[emoji37][emoji37][emoji37][emoji37][emoji37][emoji37]

Mkuu hongera kwa kuweka mchango chanya na wenye manufaa kwa bara la Afrika na Afrika kwa ujumla. Dini za wazungu in uhuni na zinafundisha ushenzi mwingi sana Zamani kulikuwa na Madaraweshi ambao Afrika tu walijitokeza kwa wingi.

Usanii ule sijui umeishia wapi. Dini ya Afrika in tamu haziweki fedha mbele kama za mashariki ya kati aka Asia. Ila Afrika itafika simama kama bara huruu oneday hata na wajukuu wangu.
 
Kweli kabisa umefichwa
Afrika ina dini ambazo ni nyingi sana kuliko bara lolote lile Duniani. Dini hizi nyingi zimepigwa ban na watu wa nje(whites) kwa sababu tu ya inferior ya mtu mweusi wa zamani. Kuishi kwa kumtegemea mzungu kwa kila kitu hadi ikapelekea hadi sasa watu wanategemea pia dini za kizungu.

Hakuna kabila hata moja Afrika ambalo limepoteza imani ya dini yao, ndio maana hata waendao makanisani hutembelea kwa mababu zao kupata kinga. Dini zote Afrika zilikuwa hazihusiani na uchawi ila mtu mweupe ndiye aliempa mtu mweusi uchawi kwa mafunzo maalumu akimdanganya ya kiimani.

Uchawi Afrika uliletwa na mzungu na ukweli huu haupingiki. ukiachana na hayo lakini pia upande wa maadili hapa nianze kwa salamu

U hai? ndugu hata kama haupo hai ila ukweli ukifikie huko huko ulipo. Nani aliyekuambia kuwa Afrika watu walikuwa wanavaa nguo full mwili mzima? Angalia wamasai japo na hao pia wamejaribu kubadilika. Ila hali ilikuwa mbaya sana zamani.

Watu walikuwa wanazuii tupu tu, Vikande vyote vya nyuma vilikuwa wazi na hakukuwa wa kushangaa katika hili kwa sababu ndiko tulikotoka. Ujio wa white man ukatibua hali ya hewa wakabadili,mtindo wa mavazi,dini, elimu, lugha, biashara na kila kitu.

Sasa katika mambo waliobadili pamoja na nidhamu na kusema nchi za Afrika hawajastarabika kwa sababu wanatembea uchi, wanaabudu madudu, wanaongea lugha chafu n.k. Watu wa Afrika walilazimishwa kukopi mila na mitindo yote ya Kizungu.

Unaposema vijana wetu hawana maadili ni kutukana wazee wetu wa zamani ambao walikuwa wanawinda,na kupiga ngoma uchi.

Hawa wapuuzi wa kizungu ndio walioita matabibu wetu kwa jina baya eti Matabibu wa kichawi(witch doctor) na wao kujiita Doctors, physician mara sijui wakemia n.k. Wakasema kupiga ngoma ni ushamba ila tupige miziki ya kisasa n.k.

Sioni jema la wazungu katika imani, wala tamaduni na wala technology kwa sababu naamini tungepigana na hali zetu. Wale wanaoenzi mababu zetu siku hizi wanajiita TIBA MBADALA sijui ndio nini. Wajiite wauguzi na wataalamu wa tiba na magonjwa mbalimbali.

Afrika without White's countries is possible, hatujachelewa sana tuanze ku uphold vya kwetu ili vitusaidie na sisi kwa masilai yetu. Hivi vya kuletewa havitufai kwani "NGUO YA KUAZIMA HAISITIRI MA**KO" na ndio mana mambo hayaendi kama ilivyotakiwa.

Nawachukia wa Asia na dini zao i.e Christian and Muslims. Ww ndugu yangu mtoto na mjuu wa Likangamai hayo mambo utayaweza? Ndio maana kulikuwa na mabala na aina ya watu na mila tofautitofauti, sasa ya nje ya nn na kuona kama vile ulichelewa kuvipata?

Kwani wao walikuwa hawajui kama Afrika kuna watu? mbona wamefika baada ya manyanyaso mauaji na dhulma kwa ndg zetu? Nini za Asia ni dini za ukweli kwa Asia na dini za Afrika ni za kweli kwa Afrika tu?

Jambo gani jema limewahi semwa na hao watu juu ya mababu zetu? wamewatukana sana kupitia imani zao na leo wamefanikisha kutufanya ndg,jamani tunaenda wapi na ilihali tunakotoka tunakudharau?

NAIPENDA AFRIKA SANA NA HATA NIKIWA JIRANI NA MZUNGU WOTE WE FEEL DIFFERENCES ON EACH AND EVERYTHING.RELIGION, LANGUAGE, STYLES,CUSTOMS, COLOUR, AWARENESS, ASSERTIVENESS STATUS, RECOGNITION e.t.c.

Ukweli haupingiki hata mniue hadi nife
 
Hapo kabla sisi tulikuwa tunafikiri vipi na tulikuwa tunakulaje ?
Naomba unipe faida,maana nijuavyo mimi ni kuwa kurudi katika asili ni jambo rahisi sana.
Ukienda kuhiji Makka unasamehewa dhambi zako unakuwa kama mtoto , !! jamani huu siupuuzi yaani unafanywa mtalii wenyewe wanapiga pesa wewe unadanganywa kusamehewa dhambi ahahahah
 
Hakuwa kuwepo kwetu huku hata na sisi kulikuwa na watu wenye miujiza ya kugeuka mawe,mara kinu, mara mtoto na mbwembwe za kila aina,so Yesu kama alikuwepo hakuwepo hiyo ni imani yao na haituhusu kiongozi.

Nabii K.Ngwale, Mkwawa, Mangungo,e.t.c. walikuwepo ila sisi tuliwaita viongozi wao wakawaita mitume na manabii. Wao waliamini uwezo wa Yesu/Muhammad ulitokana na Mungu wao na sisi tuliamini akina Kinjeketile walipewa uwezo wa ziada na Mungu wetu.
Au unafikili wale walitwaa wapi ule uwezo? na kama hapakuwahi tokea mtu nyuma yao i.e Baba,babu,mama,bibi, etc. Mungu wetu aliwainua ili kuleta mwanga na ukombozi katika bara letu. Ndio maana shida za Afrika ni the same but zipo tofauti sana na mabara mengine.
Babu yangu alikuwa na uwezo wa kuamisha mvua kutoka shamba moja kwenda jingine , tumeacha mambo aya tumekosa faida kubwa
 
Kwani dini za waafrika kabla ya wageni zilikuwa katika misingi gani ?
Jambo linapokuwa gumu kama mvua aitaki kunyesha tunakwenda milimani au mapangoni au njia ya panda tunafanya ibada zetu zikiambatana na kuvunja nazi, kumwaga mtama na kuchinja mnyama , kabla amjafika nyumbani mvua inaporomoka watu wanavuna mpaka wanasaza sasa , toka imekuja miungu ya mashariki ya mbali hakuna chochote cha maana zaidi ya watu kujivika mabomu na kujilipua ili kutetea miungu hiyo isiyo na meno wala isiyo weza kujitetea kutoka huko mashariki ya mbali , miungu hii imeleta tabu ata hapo kwa majirani zetu Somalia tunajionea vurugu tupu
 
Ukienda kuhiji Makka unasamehewa dhambi zako unakuwa kama mtoto , !! jamani huu siupuuzi yaani unafanywa mtalii wenyewe wanapiga pesa wewe unadanganywa kusamehewa dhambi ahahahah
Hijja ipo hata utalii haujulikani. Ungekuwa mwenye kutumia akili vizuri usingeuliza ujinga huu.

Umuhimu wa hijja ameufundisha mtume amani ya Allah iwe juu yake,kwahiyo suala la utalii si katika hijja na fadhila zake ameueleza mtume na hadtihi ziko wazi.

Sasa ndio uniambie ya kuwa je kipindi cha mtume kilikuwa na utalii ?

Lakini pili,ni kuwa suala la hijja ni kwa mtu mwenye uwezo.
 
Jambo linapokuwa gumu kama mvua aitaki kunyesha tunakwenda milimani au mapangoni au njia ya panda tunafanya ibada zetu zikiambatana na kuvunja nazi, kumwaga mtama na kuchinja mnyama , kabla amjafika nyumbani mvua inaporomoka watu wanavuna mpaka wanasaza sasa , toka imekuja miungu ya mashariki ya mbali hakuna chochote cha maana zaidi ya watu kujivika mabomu na kujilipua ili kutetea miungu hiyo isiyo na meno wala isiyo weza kujitetea kutoka huko mashariki ya mbali , miungu hii imeleta tabu ata hapo kwa majirani zetu Somalia tunajionea vurugu tupu

Hujajibu swali nimekwambia hivi misingi ya dini za mababu ilikuwa imejengeka katika nini ?

Usiniambie walivyokuwa wanafanya nataka uniambie misingi.
 
Mkuu tatizio ni mabadiliko na hizo imani za kiafrika zimeshindwa kuendana na mabadiliko,hata kama tusingeletewa dini ila kwa dunia ilipofika unafikiri waaafrika wangekuwa wanaenda mapangoni au kuomba mizimu? Hata hao wazungu na waarabu nao walikuwa na imani zao kabla ya hizi dini.
 
Babu yangu alikuwa na uwezo wa kuamisha mvua kutoka shamba moja kwenda jingine , tumeacha mambo aya tumekosa faida kubwa
Mkuu mababu wa aina hiyo wapo sana na sidhani kama inahusiana na masuala ya dini za kiafrika.
 
Mkuu
Tutakaokuelewa ni wachache sana humu, watu wengi walishafanyiwa kitu ninachookiita " kuuwawa kwa tabia zao halisi" Yaani karibu kila kitu hapa Afrika kimeharibiwa. Angalia maisha yetu, mathalani lugha zetu, mavazi yetu, sayansi yetu, dini zetu, usomaji wetu, majina yetu n.k hadi unajiuliza hivi sisi watu weusi tutaacha alama gani hapa duniani!!!???

Kuna jamaa mmoja nilimponda tukiwa wengi kwa kumwita mtoto wake mchanga jina la kiingereza la ajabu ajabu kisa tu eti ni zuri (si ni la kizungu bwana) nilipomwambia kuwa asiendekeze utumwa wa fikra aliniita mimi mshamba yaani akasema sijaelemika! Nikamtazamaaaa, nikamwambia waziwazi mimi naitwa TATA MKURIA na najisikia fahari kuwaita watoto wangu majina yao kama Bhoke, Ghati,Marwa, Mwita n.k.

Mkuu Frustration hakuna bara linadharauliwa kidini kama Afrika! Yaani ni aibu, halafu waafrika hawa wa sasa tena wasomi wanaendelea kuwatumikia wale jamaa wakidhani wapo sahihi yaani waafrika tumeenda hatua zaidi ya wao kujiona hizi dini zao ni bora sana hadi zinatugombanisha! Zinafanya tuuwane! Ni aibu.

Ukienda mabara mengine, huwaambii kitu kuhusu dini zao! Kama hujui nenda nchi za Ulaya, nenda nchi za Uarabuni, nenda Uhindini, nk. Ila sasa njoo Afrika! Yaani akili zetu ni nyepesi nyepesi mno. Kila kitu kinaaminika kirahisi tu, tumesoma sasa lakini bado tunaendekeza yale yale yaliyotuletea madhila siku za nyuma. Tumelala fofofo tunadhani kila kitu kipo sawa. Yaani hadi nimewakumbuka Prof Ngugi wa Thiong'o na maelekezo yake katika kitabu cha "Decolonizing the Mind" pamoja na Okoth p'Bitek na vile vitabu vyake pendwa (najua wengi mlisoma kile maarufu Song of Lawino na Song of Ocol) hawa waafrika wenzetu wametuandikia tushtuke kidogo lakini bado tupo ziii!

Wale wenzangu wanaopenda dini zetu, tuendelee nazo ingawa tunaitwa washirikina mi nasema ni sawa tu nitaendelea kutambika ila siyo kwa kafara za watu kama hawa washenzi wa baadhi ya dini hizi za kisasa wanavyofanya!

Najua tupo wengi tu ingawa makanisani na misikitini pia tunaingia mara kwa mara ila mioyoni mwetu tunaujua ukweli na pia tumeisha enda wapi na wapi kupata tiba zetu za kujikinga na mabalaa. Ukituona kwa nje tuna heshima lukuki katika jamii ila kiundani tunaamini dini za Kiafrika kimya kimya.

Tata mkuria.
hapo kwenye swala la majina nimegombana sana na huyu mwanamke. nilivyomwambia mtoto wetu atakua na jina la kiafrika alivimba vibaya mno na aliniona kama m'babu, mshamba, wa kuja. niliskitika sana kwasababu sio kosa lake, amekua programmed tangu utotoni kuona cha mzungu ni cha maana kuliko cha muafrika.. tangu utotoni anaambiwa binadamu kutoka israeli ndio Mungu wake, unatarajia nini?

Mabadiliko ya hili swala inabidi yaanzie ngazi ya kitaifa halafu yatufikie sisi, bila ya hivyo hamna kitu hapa kitabadilika. lazma serikali itie mkono wake.
 
Hujajibu swali nimekwambia hivi misingi ya dini za mababu ilikuwa imejengeka katika nini ?

Usiniambie walivyokuwa wanafanya nataka uniambie misingi.
Matendo( kulingana na umri, jinsia na wakati husika ) na miiko yake ndio misingi ya dini za kiafrika , ndio maana nikakwambia wakati ambao hakuna mvua watu wanakwenda mlimani wanafanya tambiko wana mwaga damu mambo saaafi, mambo ya kuvaa mabomu na kupigana mapanga ni miungu wa huko mashariki ya mbali , wanaotegemea watu wauane ili wapate kutajwa
 
Hijja ipo hata utalii haujulikani. Ungekuwa mwenye kutumia akili vizuri usingeuliza ujinga huu.

Umuhimu wa hijja ameufundisha mtume amani ya Allah iwe juu yake,kwahiyo suala la utalii si katika hijja na fadhila zake ameueleza mtume na hadtihi ziko wazi.

Sasa ndio uniambie ya kuwa je kipindi cha mtume kilikuwa na utalii ?

Lakini pili,ni kuwa suala la hijja ni kwa mtu mwenye uwezo.
Ahahahaahah wenzako wana future plan unafikiri ni mambumbu kama wewe !! hivi unafikir walipokuwa wakitangaza imani yao duniani walijua watu kama wewe mtaingia mkenge na kuamini tena mtakuwa wengi sanaaa, hii ni heshima kwa nchi yao na Pesa mnawapelekea , ahahahaahah unafikir kila mtu anawaza leo tu ,Mohammed alikuwa mjanja sana alijua kuna vilaza wataingia mkenga nchi itapata pesa mingi badae, eti ukienda kuhiji unasamehe dhambi unakuwa kama mtoto huu ni mpango mkakati ili mkatalii kwao mpeleke pesa hizo, amka wewe ata hili mpaka upigwe viboko ndio uelewe !!
 
Mkuu tatizio ni mabadiliko na hizo imani za kiafrika zimeshindwa kuendana na mabadiliko,hata kama tusingeletewa dini ila kwa dunia ilipofika unafikiri waaafrika wangekuwa wanaenda mapangoni au kuomba mizimu? Hata hao wazungu na waarabu nao walikuwa na imani zao kabla ya hizi dini.
Kama sio imani hizi za ovyo walizoleta hawa watu weupe mapangoni tungeenda bila tabu maana ndicho ambacho kingekuwa fahari yetu , tumeshindwa kupenda na kukienzi chetu kwa tamaa ya vitu vidogo kama elimu n.k tumepotoka
 
Back
Top Bottom