mikonomiwili katika mada hii Post ya
117 nilijibu swali linalofanana na lako kama ifuatavyo:
Asili ya vimwondo
Vimwondo ni miamba, mawe, mchanga au maumbo ya mkusanyiko wa madini yanalolizunguka jua ama yanayozunguka sayari nyinginezo, inategemeana tu na umbali lakini yote yako katika mizunguko (orbits) tofauti. Kuna wakati vinasogea karibu na hivyo kuingia kwenye mzunguko wa sayari yetu. Vinakuwa na majina tofauti kitaalam kutokana na size composition eneo vinapozungukia na hata vile vinavyoangukia duniani basi jina linabadilika kama tayari kimeshaanguka. Mfano meteor (ule mwanga wake kikiwa kinaanguka na kuwaka moto) alafu meteorite kile kipisi cha mwamba au jiwe au chuma kilichobaki baada ya kuanguka.
Vimwondo vipo siku zote katika solar system na pale vinapochomoka kwenye orbit zake mara nyingi vinakuwa either vimetokea katika Oort cloud au kwenye Kuiper belt ile inayozunguka sayari ya Neptune. Lakini kuna belts nyingine ambazo zimejaza haya mawe na mabonge ya barafu kuanzia kwenye mzunguko wa sayari ya Mars mpaka ile ya Jupiter. Asili ya vimwondo inasemekana ni wakati ule Big-Bang ilipotokea na ni mabaki ya sayari ndogo zilizopasuka na vipande vyake vimekuwa vikigongana na kuvunjana mpaka sasa hivyo sio matokeo ya nyota moja kwa moja.
Mara nyingi vimwondo vinaishia hewani.
Dunia imeshagongwa na vimwondo mara nyingi sana na hata ushahidi tunao pale mbozi Mbeya na sehemu nyingine maarufu lakini kwa silimia kubwa huishia na kuyeyuka hewani kabla ya kugonga dunia. Binafsi nimesha tembelea pale Mbozi na kwa kweli ni kitu cha kujivunia kuwa na kivutio kama kile lakini hakijajengewa au kutengewa eneo linaloendana nacho (hadhi). Kama ingekuwa sehemu nyingine pale pasingekuwa vile.
Kile kilichoanguka Urusi mwaka jana (February 15, 2013) katika mji mdogo wa Chelyabinsk ndio kilitoa somo zuri maana tayari kuna technology zenye kupima na kurekodi karibu kila kitu kinachotakiwa. Ukubwa wake ulikuwa mita 15 na uzito wake kama 7000 metric tons kabla ya kuingia katika anga la dunia. Mwendo wake ulikuwa 65,000km/h hiyo ni velocity kali sana na ndio pona pona yetu maana kwa mwendo huo kikiingia tu kwenye anga la dunia "Earth atmosphere" kinaanza kuungua kutokana na msuguano mkali sana. Kumbuka mwendo wa risasi ni kilomita elfu moja na mia mbili kwa saa (1,200km/h) hivyo ni wazi kimwondo kile kilikuwa na mwendo mkali mara nyingi sana zaidi ya risasi. Vipande vidogo tu viligusa ardhi baada ya kuungua na kulipuka ila shockwave na sauti yake watu wengi waliumia kwa kupanic, madidisha ya vioo yalipasuka na kuta za nyumba nyingi zilianguka. Na kama kingetua kama kilivyo bila kuungua na kulipuka basi ni impact yake ingekuwa zaidi ya bomu lilioangushwa hiroshima.
Wastani wa vimwondo kugonga Dunia.
Kila mwaka zaidi ya tani mia moja za vumbi na mchanga kutoka angani zinatua duniani na kwa wastani wa mara moja kwa mwaka kimwondo chenye size ya gari dogo huingia kwenye anga la dunia (Earth atmosphere) lakini huungua chote kabla ya kutua duniani. Kwa wastani wa kila miaka 2000 kimwondo cha ukubwa wa saizi ya uwanja wa mpira hugonga dunia na kusababisha madhara makubwa katika eneo husika.
Na katika wastani wa miaka milioni 10 hadi 100 kimwondo kikubwa zaidi kama saizi ya jiwe kubwa lenye upana wa kilomita 2 hadi 7 hugonga dunia na kutengeneza shimo kubwa sana, mlipuko zaidi ya bomu la nuclear, tetemeko, moto, vumbi, hewa chafu na moshi mzito ambao unaweza kukaa duniani kwa zaidi ya miaka elfu moja na hivyo kubadili majira ya dunia kwa kutoruhusu mwanga wa jua kupenya. Hiki ndicho kinachohofiwa sana maana ni wazi viumbe vingi vitafutika lakini sio maisha kwa ujumla.
Mfano mzuri wa hili unaelekezwa kwenye kimwondo kikubwa zaidi kilichoanguka zamani sana kabla binadamu hatujawa katika hali hii ambacho kinadhaniwa kuchangia kufuta wale reptiles wakubwa waliokuwa wametapakaa duniani (Dinosaurs) miaka millioni 65 iliyopita na pia kubadili majira na hali ya hewa ya dunia. Ingawa uwezekano wa kugongwa na kimwondo kikubwa ambacho kitaleta madhara mazito ni mdogo sana, lakini upon na inadhaniwa hutokea mara moja kwa kipindi kirefu labda miaka millioni mia moja. Kwa kuhofia hilo kuna baadhi ya programs zenye technologia ya juu sana zimejikita kuchunguza mwenendo wa vimwondo hasa vile vikubwa vinavyoweza kuleta madhara.
Labda pia labda ni bahati kwamba kimwondo kilibadili mazingira ya dunia na kutufanya binadamu taratibu tuongezeke kwa kuwa wale kina T-rex wasingetuacha. Si ajabu kujificha