Ukweli wa Kustaajabisha Kuhusu Nyota za Angani

Ukweli wa Kustaajabisha Kuhusu Nyota za Angani

Status
Not open for further replies.
Aisee kama ni breakthrough ya elimu ya nyota basi hapa nimeipata. Much appreciated mkuu Mgalanjuka
 
Dah Bonge la elimu mkuu shukrani sanaaa kwa kutushilikisha na sisi. Mkuu hivi hawa viumbe wafahamika ka Alliens.. Wapo kweli na walishawahi kuoneka duniani.. Walionekana mwaka gani au kuna ushaidi gani juu ya hili?

Mkuu hivi utafiti wa kisayans unaonyesha viumbe hapa dunian vilitokeaje tokeaje?

Najiulizaga sana haya maswali..
 
Mkuu Mgalanjuka, swali langu lina sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo.
umetuambia kuhusu idadi ya galaxy kwamba ni nyingi sana na sisi tupo kwenye kagalax kamoja tu kanakoitwa milky way, sasa je,
(a) Hakuna uwezekano wa kuwepo sayari kama hii katika galaxy nyingine yenye binadamu wazuri wazuri kama hii na wenye akili kama/zaidi ya sisi?
(b) Katika maafa yanayoweza kuikumba dunia, je, kitu kinachoitwa nibru (sijui kama nimepatia kuandika) kinachozungumzwa sana miaka ya karibuni unakizingumziake?
SWALI LA NYONGEZA:
Kuna utafiti wowote wa kisayansi uliowahi kufanywa kuhusu sehemu (a) hapo juu na majibu yalikuwaje?
 
Last edited by a moderator:
Pale ambapo akili yetu inaishia,ndipo Mungu huanzia.
Kuwaza Mungu atakuwaje,ni sawa na kuchota maji baharini na kuyamwaga Kisimani,Hupunguzi hata theluthi ya Bahari.Mungu atabaki kuwa Mungu.
 
Aisee nimegumdua we mtu ni hatari sana.....haya madini hata google sio hivi.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Tunashukuru kwa ILMU. Ndio maana MUNGU alieumba mbingu na aldhi hataniwi dah!
 
kuna watu walisha lifanya jukwaa hili ni sehemu ya mabishano yasiyoisha kati ya waamini wa uwepo wa mungu na wasio amini uwepo wa mungu.angalau sasa GT Mgalanjuka kaja na kitu tofauti.nina hakika 100% ilm hii hata Kiranga na wale wapinzani wake imewashangaza.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mgalanjuka, swali langu lina sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo.
umetuambia kuhusu idadi ya galaxy kwamba ni nyingi sana na sisi tupo kwenye kagalax kamoja tu kanakoitwa milky way, sasa je,
(a) Hakuna uwezekano wa kuwepo sayari kama hii katika galaxy nyingine yenye binadamu wazuri wazuri kama hii na wenye akili kama/zaidi ya sisi?
(b) Katika maafa yanayoweza kuikumba dunia, je, kitu kinachoitwa nibru (sijui kama nimepatia kuandika) kinachozungumzwa sana miaka ya karibuni unakizingumziake?
SWALI LA NYONGEZA:
Kuna utafiti wowote wa kisayansi uliowahi kufanywa kuhusu sehemu (a) hapo juu na majibu yalikuwaje?

Mkuu Capitalist, nitaelezea kwa kifupi na kwa lugha nyepesi.

Tuanze na kipengele (a)Uwezekano wa kuwepo sayari kama hii katika galaxy nyingine yenye binadamu wazuri wazuri kama hii na wenye akili kama/zaidi ya sisi.

Ni ukweli usio na shaka kwamba kuna nyota nyingi sana zinazofanana na jua letu katika maeneo mengine ya mbali sana katika universe. Wanasayansi wanasema nyota zinazofanana na Jua letu ni kati ya asilimia 5 hadi 20 ya nyota zote katika universe tunayoweza kuiona (observable universe). Hili neno la universe tunayoweza kuiona lina maana kwamba pale tusipoona basi kuna uwezekano universe inaendelea au kunavitu vingine tusivyovijua lakini makadirio yanayofanyika ni ya ulimwengu tunaoweza kuuona. Sasa ukumbuke katika mada nilisema nyota zinakadiriwa kuwa sextillion 100 au zaidi katika ulimwengu tunaoweza kuuona sasa tukisema mfano tuchukue tu asilimia 5 yake, basi tutakuwa tunaongelea nyota bilioni-bilioni 500 zinafanana kimazingira (joto, ukubwa, umri, aina, uwepo wa sayari) na jua letu.

Sasa kwa number hizi basi ina maana uwezekano wa kuwepo sayari zenye maisha ni mkubwa ingawa maisha yanaweza yasiwe haya tunayoyajua sisi. Hapo kabla niligusia tafiti iliyofanywa na PNAS (Proceedings of the National Academy of Sciences) ambayo inapendekeza kwamba kuna angalau asilimia moja (1%) ya sayari zinazofanana sana na dunia yetu katika hizi nyota zinazofanana na jua.

Kuwa na binadamu wanaofanana na sisi hilo linawezekana lakini kumbuka kisanyansi mazingira yanachangia sana mwonekano au matokeo ya viumbe. Kama mazingira yakiwa tofauti kidogo basi matokeo ya maisha au viumbe yatafuata mkondo. Hili tunaliona hata katika viumbe wa kawaida wa duniani jinsi wanavyokuwa na vigezo vinavyoendana na wao kumudu mazingira yao. Kwa kuwa hata hizi sayari zinazofanana na dunia haziwezi kuwa na mfanano pacha yani circumstance zile zile basi tusitegemee kukutana na viumbe "wanaofanana asilimia mia na sisi". Jinsi kila kitu kinavyoonekana leo hii ni matokeo ya jinsi mazingira yalivyokuwa miaka milioni iliyopita na vivyo hivyo kadri muda unavyoenda.

Kuwa na akili zaidi yetu au kuwa na maendeleo na technology kubwa sana zaidi yetu hili ni wazi na lina sababu zake. Kwanza kuna uwezekano wa utofauti wa maisha kuanza hivyo kufanya viumbe wengine kama wapo basi wendine wanaweza kuwa wame-evolve zaidi yetu kwa kuwa na muda mrefu zaidi katika ulimwengu. Kama tukichukua mfano wa dunia yetu (Earth), maisha yanakadiriwa kuevolve kutoka katika simple form kati ya miaka bilioni 3.5 iliyopita hii ni kutoka kwa evolutionists. Kuna sayari zilizo na muda mrefu zaidi ya dunia na hapa lazima utaona katika hali ya kawaida sisi ndo tunaanza na kuna wengine waliokwisha piga hatua kubwa sana. Na hata tukisema katika sayari nyingine kuna viumbe waliumbwa kabla yetu (Creationists) alafu sasa tujilinganishe nao lazima watakuwa wametuzidi mbali.

Pili, kama kuna kiumbe kikifika katika sayari yetu basi hii ina maana technology inayowezesha kusafiri umbali huo si ya kawaida. Katika mada nimeongelea huge distances kutoka eneo moja hadi jingine. Hata nyota iliyo jirani yetu si rahisi kuifikia kwa technolojia ya usafiri tuliyonayo sasa. Miaka elfu sabini njiani kwa speed kali kabisa ambayo space shuttle inaweza kwenda.

(b)Kuhusu Nibiru. Hii ya Nibiru au planet X haina ukweli wowote na wala haipo. Astronomers na wanasayansi (sio wote) wala hawahangaiki na habari hii kwa kuwa haina uthibitisho wa kisayansi zaidi ya tafsiri flani za symbols za jamii za zamani. Ila kama kuna mwenye uthibitisho au misingi iliyosimama vizuri kuhusu hili atuwekee tujadili.
 
mkuu Mgalanjuka kuna jambo niliwahi kulisoma,linaitwa forbidden knowledge.yaani ni maarifa yanayofahamika kwa watu wachache tu wenye upeo mkubwa duniani na ambao wapo ktk jumuiya za vyama vya siri (secret societies).
inasemekana ni nadra sana kukuta yapo ktk mitaala ya elimu ya vyuo vikuu.

je elimu hii ya maswala ya anga na sayari unayotuwekea hapa,inafundishwa ktk vyuo vikuu bila kuficha baadhi ya vitu?.kama inafundishwa,course yake inaitwajwe?.na huchukua miaka mingapi kuhitimu?.

kwanini ktk lile bandiko la UFOs and Aliens ulitoa tahadhari kuwa mengine huto eleza kuhofia usalama wako?.
 
Last edited by a moderator:
!
!
mleta uzi ana undugu na Makamba nini!? maana hizi ni fix tena za mchana kweupe....nyota six trillion 100 sijui miaka 70000 kwa spidi kali. Nishushe mkuu imetosha.
Hizi ni nyororo ka siyo kamba ngumu.
 
mkuu Mgalanjuka kuna jambo niliwahi kulisoma,linaitwa forbidden knowledge.yaani ni maarifa yanayofahamika kwa watu wachache tu wenye upeo mkubwa duniani na ambao wapo ktk jumuiya za vyama vya siri (secret societies).
inasemekana ni nadra sana kukuta yapo ktk mitaala ya elimu ya vyuo vikuu.

je elimu hii ya maswala ya anga na sayari unayotuwekea hapa,inafundishwa ktk vyuo vikuu bila kuficha baadhi ya vitu?.kama inafundishwa,course yake inaitwajwe?.na huchukua miaka mingapi kuhitimu?.

kwanini ktk lile bandiko la UFOs and Aliens ulitoa tahadhari kuwa mengine huto eleza kuhofia usalama wako?.

Mkuu kadoda11, Kwa "forbidden knowledge" sidhani kama inahusiana na elimu ya anga ambayo iko wazi kwa mtu yeyote. Astronomy ipo miaka nenda rudi na wala haijawahi kuwa siri na kwa wale wenye interests wanaweza kujifunza na kuelewa mambo mengi sana ambayo kwa kweli yanaweza kukufanya utafakari vizuri na kutambua hata mambo mengine yasiyo ya moja kwa moja kwa upeo mkubwa.

Secret societies? No, ila kuna "big boy clubs" kadhaa hawa wanajua na wanashare vitu vikubwa vya hatari sana.

Watu wengi sana wanafanya au wanajihusisha na astronomy kama hobby huku wakiendelea na shughuli zao za kujitafutia kipato kama kawaida. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kujua baadhi ya mambo kuna furaha yake na aina fulani ya kuchangamsha ubongo au akili.

Astronomy kama career pia inawezekana, maana kuna baadhi ya vyuo vikuu kwa wenzetu vinavyofundisha either Astronomy au masomo yanayoendana na Astronomy kwa hiyo utajifunza sayansi inayohusiana na vitu pamoja na matukio yaliyo nje ya uso wa dunia. Kazi zinazohusiana na mambo haya pia zipo ingawa kwa nchi kama za kina sie inaweza kuwa tatizo.

Kitu kimoja muhimu ni kwamba kama unataka kuwa Astronomer lazima msingi uwe kwenye Mathematics na Physics ingawa unapoenda mbele zaidi unakuta eneo hili haliegemei kwenye somo au field moja kwa maana ya kwamba useme utasoma course fulani then umemaliza na unajua kila kitu, hapana. Hapa ni science nzima kwa ujumla na inaweza pia kuhusisha maeneo mengine ambayo sio ya sayansi katika kutafuta pa kuanzia. Wataalamu wanaopelekea majibu ya maswali magumu tunayofafanua wana grounds mbalimbali. Kuna astrophysicists, astrobiologists, mathematicians, technicians, researchers wa fani mbalimbali na other scientists wanaoweza ku-contribute their knowledge katika kusolve issues fulani.

Kuhusu bandiko la civillized beings sikutoa tahadhari kuhusu usalama wangu bali nilitoa angalizo kwamba sitatoa majina na information za moja kwa moja kutoka kwa mtu mmoja aliyepata kunishirikisha juu ya utafiti fulani. Hivyo nikasema nitaielezea ile habari kama hadithi na kwa lugha nyepesi ili wenye kumeza wameze na pia wengine waichukulie kama hadithi. Ile habari ina hypothesis na assumptions nyingi hivyo huwezi kuiweka kama fact. Ila kwa hili la nyota za angani ni crystal clear.

Cheers
 
!
!
mleta uzi ana undugu na Makamba nini!? maana hizi ni fix tena za mchana kweupe....nyota six trillion 100 sijui miaka 70000
Hizi ni nyororo ka siyo kamba ngumu.

Hahahah! Makamba tena? Haya twende taratibu usikurupuke. Elezea vizuri fix ni wapi na wewe unachojua ambayo ndio ukweli kiandike vizuri ni kipi. Nina uhakika hujasoma vizuri na huna uelewa wa kutosha kujua hiyo comparison ya distance na kwa nini miaka elfu sabini imewekwa hapo. Wengi wanaelewa nazungumzia nini na sijui kama naweza kubishana na wewe kama huna mbadala wa "nyororo na kamba ngumu"

Hilo jina la namba unayo-refer unakosea siyo "six trillion" inaitwa Sextillion. Kuchanganya kitu kilichoandikwa wazi namna hiyo it is a sign of your incompetence. Usiwe mvivu jiridhishe hapa what is sextillion:

Sextillion | Define Sextillion at Dictionary.com

noun, plural sex·til·lions ( as after a numeral ) sex·til·lion.1.a cardinal number represented in the U.S. by 1 followed by 21 zeros, and in Great Britain by 1 followed by 36 zeros.


adjective2.amounting to one sextillion in number.



Origin:
1680&#8211;90; < French < Latin sext ( us ) sixth + -illion, as in million


Related formssex·til·lionth, adjective, noun



 
Shukrani Mkuu Swat.

Mkuu Mgalanjuka asante kwa elimu.Please mkuu,be honesty and tell me who are you.Are you an alien?Do u have any association with them or does ur DNA have any similarities with that of Alien/UFO
/ET?If you are any of the questions above,if possible please let's meet
Siyo kwa ubaya.
 
Mkuu Mgalanjuka asante kwa elimu.Please mkuu,be honesty and tell me who are you.Are you an alien?Do u have any association with them or does ur DNA have any similarities with that of Alien/UFO
/ET?If you are any of the questions above,if possible please let's meet
Siyo kwa ubaya.

Mkuu Extraterrestrial, Am just another Tanzanian guy. That's just an avatar it got nothing to do with who I really am. Thanks.
 
Mkuu Mgalanjuka asante kwa elimu.Please mkuu,be honesty and tell me who are you.Are you an alien?Do u have any association with them or does ur DNA have any similarities with that of Alien/UFO
/ET?If you are any of the questions above,if possible please let's meet
Siyo kwa ubaya.


Mmmmmmmmh.....hapa hata sielewi mkuu_does alien exist in the real world..?

Anyway...ngoja aje tumsikie mwenyewe mkuu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom