Monstgala
JF-Expert Member
- Aug 25, 2009
- 1,079
- 1,036
- Thread starter
- #81
Dah Bonge la elimu mkuu shukrani sanaaa kwa kutushilikisha na sisi. Mkuu hivi hawa viumbe wafahamika ka Alliens.. Wapo kweli na walishawahi kuoneka duniani.. Walionekana mwaka gani au kuna ushaidi gani juu ya hili?
Mkuu hivi utafiti wa kisayans unaonyesha viumbe hapa dunian vilitokeaje tokeaje?
Najiulizaga sana haya maswali..
Mkuu geek jo, naomba swali lako la kwanza nilijibu katika uzi mwingine ujao (specific kwa area hiyo) na unamajibu mazuri ya swali lako. Nafanya hivi ili tusi-diverge sana kutoka kwenye mada kuu jambo ambalo litasababisha nisieleweke kwa wale wanaosoma vipande vifupi vifupi kama bwana mdogo mmoja aliyeibukia hapo kati.
Swali la pili ambalo unauliza ni jinsi gani viumbe hapa duniani vilitokea au kwa lugha nyingine labda unamaanisha maisha yalianza vipi hapa duniani nalo nitalijibu kwa ufupi na kwa lugha nyepesi maana ni mada pana sana hii. Naam, utafiti wa kisanyansi haujatoa jibu moja katika hili na kuna theories nyingi na zote zinatoa majibu fulani lakini pia ziaacha gaps ambazo zinasababisha kusiwe na jibu la kutosheleza kwa asilimia mia. Naomba nieleweke kwamba kama mdau alivyouliza akibase kwenye sayansi nami nitajibu kutoka huko huko lakini hii haina maana ya kufuta logic ya uumbaji maana wapo wanasayansi wengi tu wanaamini katika uumbaji (creationists). Hizi theories nazotaja zinaacha ile logic ya kwamba tuliumbwa na zinatafuta au zinafuata logic ya kuibuka kwa bahati fulani.
Tuziangalie kwa kifupi.
Kutoka kwenye dunia iliyokuwa imeganda kwa barafu (Chilly start theory)
Hawa wanasema barafu inawezakuwa ilifunika sehemu kubwa ya dunia na bahari zote miaka billion 3 iliyopita maana jua halikuwa linawaka sana kama ilivyo sasa. Sasa hizi layer kubwa sana za barafu zilitunza organic compounds katika sehemu yake ya ndani hivyo kuzikinga na uharibifu kutoka katika vurumai la anga lilokuwepo wakati huo. Pia baridi ilisaidia kutunza molecules hizi kukaa kwa muda mrefu sana bila kuharibika na hivyo kupelekea maisha kuanza. Lakini ugumu (gap) unakuja pale kwenye nini hasa aina ya chagizo iliyopelekea maisha kuanza.
Did life begin in ice?
Kutoka kwenye matundu ya volcano chini ya bahari (Deep-sea vents theory)
Hii theory inasema inawezekana maisha yalianza kutokana na hydrothermal vents zilizoko chini ya bahari ambazo hutoa molecules zenye hydrogen nyingi sana. Sasa katika miamba yake inawekekana moleules hizi zilijazana sana na kusababisha aina fulani ya reaction iliyosababisha maisha kuanza. Hawa wanasansi wana egemea kwenye ukweli kwamba hata leo hii anao lenye aina hii ya geothermal vents kuna nichati kubwa ya joto na kemikali na viumbe vingi sana vya baharini huendesha maisha kando kando na ndani ya yake. Ugumu unakuja ukitengeneza simulation katika maabara yenye condition sawa na zinazopendekezwa katika theory hii bado haileti pure results.
Earth Life May Have Originated at Deep-Sea Vents
Kutokana na radi yenye chaji ya umeme (Electric spark theory)
Hii ya charge ya umeme ilileta changamoto sana maana chaji au cheche za umeme zinaweza kutengeneza amino acids na sugars(hivi ni vyanzo vikuu vya maisha) katika mazingira yaliyojazwa maji, methane, ammonia na hydrogen. Ilikuwa mwaka 1953 katika jaribio lililoonesha labda radi (kwa kuwa na electric charges) ilisaidia kutengeneza vyanzo vikuu vya maisha. baada ya hapo ugumu kwa hii theory ukaja pale tafiti nying zilipoonesha hakukuwa na hydrogen nyingi ya kuwezesha hii kitu ingawa inaonekana methane, ammonia na radi zilikuwa nyingi katika wakati huo.
The Spark of Life | Astrobiology Magazine
Kutokana na msukumo wa udongo (Community clay)
Theory hii inapendekeza molecules za mwanzo za maisha zinaweza zikawa zimekutana katika udongo hii ni idea aliyoijenga mtaalam wa kemia wa Scotland, Alexander Graham Cairns-Smith katika chuo kikuu cha Glasgow. Anadai madini fulani na udongo yanaweza kuwa chanzo cha kujipanga kwa organic molecules kuwa aina Fulani ya sehemu ya kiumbe na baadae molecules hizi kuanza kujipanga zenyewe.
Life might have Evolved in Clay, Researchers Find : Biology : Nature World News
Ulimwengu wa asidi zenye protini (RNA world)
Deoxyribonucleic acid (DNA) zinahitaji protein ili ziform na protein zinahitaji DNA ili ziform. Hapo sasa ndio inakuja hii theory ya Ribonucleic acid (RNA) World ambayo inapendekeza kwamba kwa sababu RNA inatunza informations kama DNA na inafanya kazi ya catalyst kama protein yani inaweza kuapply pande zote basi ndio chanzo. Lakini ugumu unakuja sasa hizo RNA zilitokea wapi kwa mara ya kwanza. Ni ngumu sana kwamba ziliibukia tu alafu zikaanza kuji-replicate.
The RNA World and the Origins of Life - Molecular Biology of the Cell - NCBI Bookshelf
Kutoka kwenye anga za mbali (Panspermia)
Hii ambayo inashikiliwa na wengi inasema maisha hayakuanzia hapa dunia bali yaliletwa na kimwondo kutoka anga za mbali. kwa mfano tunaweza kujionea vipande vya miamba na mawe vilivyotoka sehemu nyingine ambayo si duniani. hivyo theory hii inapendekeza vimwondo au kimwondo Fulani kilikuja na vijidudu(microbes) vilivyo sababisha maisha kuanza hivyo sisi wote asili yetu ni huko mbali angani. Sasa hapa ugumu unarudi kule kule kwamba sasa kama maisha hayakuanzia hapa duniani na huko angani yalikotokea yalianzaje?
PANSPERMIA THEORY origin of life on Earth directed panspermia lithopanspermia meteorites - Panspermia Theory
Zipo na nyingine ila hii inatoa mwanga baadhi wanasayansi waonaje katika swala hili la mwanzo wa maisha.