Ukweli wa Kustaajabisha Kuhusu Nyota za Angani

Ukweli wa Kustaajabisha Kuhusu Nyota za Angani

Status
Not open for further replies.
Mkuu Mgalanjuka, nimesoma bandiko lako hapo juu na nimerudia na kurudia kitu nilichooma hapo ni vigumu kuamini kwa akili ya kawaida. Mimi nachojua sayansi inaprove fact. Mpaka hapo mimi sijaona ukweli wowote.

Kwa mfano unasema ...katika picha hii kuna galax 10000 na kila 1 ina nyota bilion 100. Na hiki ni kaeneo kadogo tu katika anga! haya manyota yote na ukubwa ulisema pamoja na umbali uliosema wa karibu km 1600 yanakaeje huko angani?

Ukaendelea tena, chuo kikuu cha Hawaii kilifanya utafiti wa kutosha kukokotoa kila punje ya mchanga hapa duniani wakagundua kuna 7.5 quintillion za mchanga na kila punje inawakilisha nyota 10000 katika universe! Ajabu uwiiiiii! Hii ni nini jamani? Mm nitakuwa wa mwisho kuamini. Yaani hawa jamaa wanajua idadi ya punje za mchanga?

Hapa ndio ulinimaliza kabisa uliposema kijiko (nerton) cha chai kina uzito sawa na mapiramidi 900 yaliyoko pale misri! hawa jamaa huwa wanaandika wakia wamelewaeh! Heeh! Hii kali.

Mkuu Mgalanjuka haya makitu uliondika ni fikra za watu na ni ubabaishaji wa kiwango cha juu. Naomba nitofautiane na wewe.
 
Last edited by a moderator:

Hapa ndio ulinimaliza kabisa uliposema kijiko cha chai kina uzito sawa na mapiramidi 19000 yaliyoko pale misri! hawa jamaa huwa wanaandika wakia wamelewaeh! Heeh! Hii kali.

Mkuu Mgalanjuka haya makitu uliondika ni fikra za watu na ni ubabaishaji wa kiwango cha juu. Naomba nitofautiane na wewe.

Mwanafunzi makini huwa ni mdadisi, safi kijana
 
Last edited by a moderator:
Hahahah! Makamba tena? Haya twende taratibu usikurupuke. Elezea vizuri fix ni wapi na wewe unachojua ambayo ndio ukweli kiandike vizuri ni kipi. Nina uhakika hujasoma vizuri na huna uelewa wa kutosha kujua hiyo comparison ya distance na kwa nini miaka elfu sabini imewekwa hapo. Wengi wanaelewa nazungumzia nini na sijui kama naweza kubishana na wewe kama huna mbadala wa "nyororo na kamba ngumu"

Hilo jina la namba unayo-refer unakosea siyo "six trillion" inaitwa Sextillion. Kuchanganya kitu kilichoandikwa wazi namna hiyo it is a sign of your incompetence. Usiwe mvivu jiridhishe hapa what is sextillion:

Sextillion | Define Sextillion at Dictionary.com

noun, plural sex·til·lions ( as after a numeral ) sex·til·lion.1.a cardinal number represented in the U.S. by 1 followed by 21 zeros, and in Great Britain by 1 followed by 36 zeros.

adjective2.amounting to one sextillion in number.

Origin:
1680–90; < French < Latin sext ( us ) sixth + -illion, as in million

Related formssex·til·lionth, adjective, noun

!
!
haya kaka mkubwa mie ni inkompetensi nimekubali ila kwa kamba hujambo.......yaani kama mtoto akizaliwa leo kwenda hadi huko atafika akiwa na miaka elfu sabini au, hebu fafanua vizuri mkuu nielewe. Tena kwa chombo cha mwendo mkali
 
mkuu "316 pekeako" kumbe na wewe umeshtukia? Kwani links ndio ukweli? Tufike mahali tusikubali kila kitu, kuna watu humu washaanza eti jamaa apewe tuzo ya mwanajukwa bora.!

Naapa kwa mbingu na ardhi hata wingi wa nywele zangu hawa jamaa hawajui seuse mchanga! Eti dunia ina zaidi ya miaka milioni 65! Wakati huo watu walikuwa hawazaani? Mbona dunia ingeshajaa miaka kibao iliyopita.

Hii maanake ni kuwa kama kuna uwiano wa kuzaa na kufa ni kwamba kama miaka hiyo 65ml ilyopita na watu walikuwa nanazaliwa 2000 kwa kila mwaka na 1000 wanakufa kila mwaka , leo dunia ingekuwa na watu 65 billion. Kumbuka dunia ina watu takribani 6 bln kwa sasa.

Mgalanjuka njoo huku bwana.
 
sie wengine ambao ni wabishi kumeza ni mainkompetensi bana................yaani miaka elfu sabini na mtu anakubaki tu hahahahahahahahaha duh. Hapana hata kama bwana, hapana bana hii ngumu kumesa
 
Ulivo-quote post ya jamaa hapo juu ina maandishi mengi kitendo cha wewe kuiquote tena ina maana inaongezeka urefu mara mbili, kwa watu wanaotumia simu kuscrow mpaka kufika chini kwenye hizi post zingine inawawia vigumu.

vilaza kama huyo wako wengi sana humu,unataka kuniambia haelewi? mi mwenyewe natumia simu ya kizamani sana ambayo haina hata touch ila napenda jf
 
Mkuu Mgalanjuka, nimesoma bandiko lako hapo juu na nimerudia na kurudia kitu nilichooma hapo ni vigumu kuamini kwa akili ya kawaida. Mimi nachojua sayansi inaprove fact. Mpaka hapo mimi sijaona ukweli wowote.

Mkuu, Asante kwa maswali yako, Sayansi ni mfumo wa kupata elimu. Mfumo huu unatumia mbinu za kuangalia, kupima na kufanya majaribio ili kuelezea na kufafanua jambo au mambo fulani katika ulimwengu halisi. Katika arguments zako sioni sayansi inapovurugwa ila zaidi sana naona hujaielewa vizuri concept na mifano iliyowekwa na pia ume-quote kwa ufupi na ukaacha context nzima ambayo ingekusaidia kuelewa vizuri. Sio mbaya nitakuelewesha ila kwanza open your mind fully. Nitapitia concerns zako na kujibu kwa ufupi ila uwe tayari at least kugoogle na kufuata link nitakazokupa.

Kwa mfano unasema ...katika picha hii kuna galax 10000 na kila 1 ina nyota bilion 100. Na hiki ni kaeneo kadogo tu katika anga! haya manyota yote na ukubwa ulisema pamoja na umbali uliosema wa karibu km 1600 yanakaeje huko angani?

Umeielewa vibaya. Kumbuka hapa nilikuwa sizungumzii universe nzima bali eneo dogo sana katika anga za mbali zaidi ambazo hazikuwa kuchunguzwa kabla ya mwaka 1995. Hebu nisome nanukuu:

"Mwaka 1995, wanasayansi walichagua kajisehemu kadogo sana katika anga ambako kwa macho ya kawaida kalikuwa kanaonekana hakana nyota yoyote wala mwanga wowote. pia kwa telescope ya kawaida kaeneo haka bado kalionesha hakana kitu chochote yani ni giza tu. Eneo hili dogo ambalo lilionekana tupu ni kama vile eneo linaloweza kuzibwa na mpira wa tenis ukiwa juu yako kwa mita mia. Kwamuda wa siku kumi wanasayansi wakitumia Hubble telescope, walichunguza eneo hili ambalo lilidhaniwa halina kitu na picha nii chini ndicho walichovumbua:"(picha) Ajabu!

Kila kinachoonekana katika picha hiyo si nyota tena, hata kidoti kidogo kabisa cha mwanga ni galaxi nzima. Katika picha hii tu kuna zaidi ya galaxi 10,000 na kila moja ikiwa na zaidi ya nyota billioni 100. Lakini kumbuka hiki ni kisehemu kidogo sana cha anga tunayoiona kama vile saizi ya kichwa cha pini.

Hivyo picha hii ilisaidia makadirio ya ulimwengu uonekanao (observable universe) kwamba una zaidi ya galaxi bilioni 100, ambayo inafanya jumla ya nyota katika ulimwengu tunaoweza kuuona kuwa kwenye kati ya 100 sextillion stars."
Mwisho wa kunukuu.

Hebu google Hubble Ultra Deep Field then ukishasoma urudi uniambie wapi hujaelewa ili twende sawa.

Ukaendelea tena, chuo kikuu cha Hawaii kilifanya utafiti wa kutosha kukokotoa kila punje ya mchanga hapa duniani wakagundua kuna 7.5 quintillion za mchanga na kila punje inawakilisha nyota 10000 katika universe! Ajabu uwiiiiii! Hii ni nini jamani? Mm nitakuwa wa mwisho kuamini. Yaani hawa jamaa wanajua idadi ya punje za mchanga?

Ndio, wenzetu wanafanya tafiti za kila aina. Nimetumia mfano huu wa mchanga ili kukupa picha rahisi ya number kubwa zinazotajwa ili ujenge mental picture unapofikiria wingi wa nyota. Kuhesabu mchanga ndio ni hesabu ngumu lakini kisayansi inawezekana ndio maana tuna kitu inaitwa Approximation. Hii inakuwa applied frequently kwenye mathematical functions, shapes, physical laws etc. and its valid and popular in science. Kwa mfano katika physics baadhi ya complex problems ambazo huwezi ukazifanya kwa ku-analyse directly bali unatumia njia hii na unapata accurate solution. Tunaweza hata tukahesabu miti yote duniani katika sayansi. Na hii ya mchanga isikutishe sana maana zipo zile nzito haswaa, ningetaja hesabu na equations zinazotumia katika SUSY ama Super symmetry theory ndio ungenipiga mawe kabisa.

Sasa nenda kachungulie formula ya kuhesabu mchanga wa bahari iko hapa:
Grains of Sand on the World's Beaches

Hapa ndio ulinimaliza kabisa uliposema kijiko (nerton) cha chai kina uzito sawa na mapiramidi 900 yaliyoko pale misri! hawa jamaa huwa wanaandika wakia wamelewaeh! Heeh! Hii kali.

Hii ni pia naona umeiquote vibaya. Hapo ina maana uzito wa kijiko kimoja cha chai labda gram 2, katika Netron star ujazo sawa na huo (wa steel ya kijiko cha chai) una uzito mkubwa sana ( 5.5×10[SUP]12[/SUP] kg) (that is 1100 tonnes per 1 nanolitre) unaoweza kulinganisha na mapiramidi 900 ya Giza Egypt. Ni katika kukujengea picha ya namba kubwa zinazotajwa ndipo mifano hii inakuja kwa maana zaidi ya trillion namba nyinginezo hatuna matumizi nazo na hivyo hatujua hata tofauti yake. Kuna mifano mingi ya uzito(solar mass) wa Neutron Star, mwingine unasema material ya Neutron start inayojaza kibox kimoja cha kiberiti ina uzito wa tani bilioni tano sawa na jiwe kubwa lenye upana wa kilomita moja.

Hebu kachungulie hapa Neutron Star Crust Is Stronger than Steel

Mkuu Mgalanjuka haya makitu uliondika ni fikra za watu na ni ubabaishaji wa kiwango cha juu. Naomba nitofautiane na wewe.

Mpaka leo hii sijawahi kusoma kitu ambacho si fikra za mtu. Kila kitu hata hiyo device unayotumia kuleta post zako imetokana na fikra za mtu. Ni sawa kabisa, una uhuru wa kukubali au kukataa lakini at least kutokuelewa kwako kusiwe sababu ya kuona mambo usiyoyaelewa ni ubabaishaji. Karibu tena.
 
!
!
haya kaka mkubwa mie ni inkompetensi nimekubali ila kwa kamba hujambo.......yaani kama mtoto akizaliwa leo kwenda hadi huko atafika akiwa na miaka elfu sabini au, hebu fafanua vizuri mkuu nielewe. Tena kwa chombo cha mwendo mkali

Threesixteen Himself, hii ni topic serious. Ukiuliza swali nitajibu lakini ukisema tu ni kamba basi mi nakosa cha kukujibu zaidi ya kukuona mtu fulani. Miaka elfu sabini! Isome concept vizuri ukiwa umetulia. Kumbuka hiyo ni katika kukuonesha kwamba ni mbali sana na sisi binadamu kwa technolojia ya sasa hatuwezi kufika huko kirahisi. Hiyo ni nyota iliyokaribu kabisa. Umbali wake ni kama miaka 4.5 ya mwendo ambao mwanga unasafiri. Sasa wewe kama binadamu na chombo chako ambacho kwa hakika hakiwezi kusafiri kwa mwendo wa mwanga basi utasafiri au chombo chako kama kingekuwa na mafuta na uwezo wa kutoharibika na pia kuwa na akiba ya chakula na mazingira ya kukufanya wewe ukae ndani yake bila kuhitaji chochote kutoka nje basi miaka sabini ungekuwa uko njiani na labda ungekufa bila kufika. kama ni ni mtoto ndio angefika akiwa na miaka sabini.

Lugha hii au mifano hii inatumika kukupa makadirio halisi ambayo ni ukweli na yamefanyiwa utafiti na kupitishwa. Ili wewe ulewe miaka 4.5 ya kusafiri kwa mwanga ni nini na umbali uliopo kati yetu na nyota nyingine iliyo karibu ni upi, basi mifano kama hii ni lazima lakini usidhani kwamba ni mimi nimetunga au ni watu fulani wametunga. Ni matokeo ya hisabati na research zinazohusisha wataalam wa hali ya juu. Unapobisha lazima pia utoe hoja nzito na kuonesha kwa nini unabisha na wewe utafiti wako unasemaje au fikra zako zinapinga kutokana na nini. Mi nipo nakusubiri.
 
Mleta mada una moyo ndugu, yaani vitu basics kabisa hivi inawawia ngumu watu kuelewa wanatoapovu tu, kaazi kweli!
 
Mtoa maada haya mambo uliyoeleza hapa yanahitaji sana.. akili inayoweza kufanya imagnation kichwani.. Kama uelewavyo watanzania wengi hesabu walikimbia. Watu wa HGL watakuuliza maswali mpka utakiona cha moto mkuu... Hawajui hata atom ni kitu gani kwanza..
 
Kijana it seems you know that field very well, but usikrem kila kitu kwa technologia yetu ya kibongo hiyo elimu sio muhimu sana kwamba inahitadi attention katika masomo yetu, hizo information ndeefu unazoleta hapa kila mtu anaweza kuziacces 'Google it' ulichofanya hapo ni kutafsiri tuu nayo pia kwa kutumia google translator, hakuna jipya hapo, watu ni wavivu tuu wa kutafuta mambo ulivyoandika hapa kuna watu wanakuona genius na wengine wanatamani upewe tuzo Nobel

vipi hizi hating tena zinatoka wapi, kati ya aliyoandika kweli hakuna jipya, hata wewe uliyojifunza chuoni hakuna jipya yote yanapatikana google, kushare na wanajamii chochote unachokijua bila kujali ulikokitoa ni jambo jema, au mwenzetu haujawahi kusoma jambo sehemu ukaja kulileta jf?!! Btw, mleta mada anaelewa anachokiandika, ni tofauti na kucopy na kupaste bila kuwa na uelewa sahihi wa mada husika, na karahisisha kwa kuandika kiswahili, hajatumia translator kama unavyodai wewe, hakuna kiswahili cha google translator hapo!! Tuache kukatishana tamaa jamani, elimu tuliyonayo ni ndogo sana kulinganisha na elimu ya dunia hii, tunavyosoma na kujadiliana katika mada mbalimbali ndiyo tunapanua uelewa, kama wewe unaelewa kila kitu ni nzuri pia ukapita kimyakimya kwani thread ngapi umepita humu jf!!!
 
Mleta mada una moyo ndugu, yaani vitu basics kabisa hivi inawawia ngumu watu kuelewa wanatoapovu tu, kaazi kweli!

Aisee Qyberteq, ndio tabu yenyewe hii. Nilitaka nione ni upeo gani hawa watu wanao lakini naona nimepata jibu baada ya kuona post zao zilizofuata. Lakini inashangaza pale mtu asipoelewa yeye that makes everything false. Na wale wote wanaoelewa basi kwake wamepotoka. So how can we move forward? Ndio sababu ya kuwaelezea kwa njia rahisi kabisa lakini labda ni kwa faida ya watu wengine wanaopenda kufahamu lakini sio wao.
 
Pale ambapo akili yetu inaishia,ndipo Mungu huanzia.
Kuwaza Mungu atakuwaje,ni sawa na kuchota maji baharini na kuyamwaga Kisimani,Hupunguzi hata theluthi ya Bahari.Mungu atabaki kuwa Mungu.

nadhani hiyo ni topic nyingine, hapa tunajifunza mambo ya anga tu!
 
Mtoa maada haya mambo uliyoeleza hapa yanahitaji sana.. akili inayoweza kufanya imagnation kichwani.. Kama uelewavyo watanzania wengi hesabu walikimbia. Watu wa HGL watakuuliza maswali mpka utakiona cha moto mkuu... Hawajui hata atom ni kitu gani kwanza..

duh! vilaza walikimbia hesabu lakini wanajiita namba namba ..mara ziroseventytwo mara threesixteen heheheh kaazi kwei kwei.
 
Mkuu Mgalanjuka haya makitu yanachanganya sana. Labda mimi sielewi, lakini mbona umeandika kwa lugha nyepesi sana.? Kwa hiyo mkuu hizi link unazotuwekea ndio ushahidi wa kuwa kuna manyota kibao huko angani kuzidi mchanga wa pwani!?

Naomba niendelee kufuatilia bila kuamini.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mgalanjuka, nimesoma bandiko lako hapo juu na nimerudia na kurudia kitu nilichooma hapo ni vigumu kuamini kwa akili ya kawaida. Mimi nachojua sayansi inaprove fact. Mpaka hapo mimi sijaona ukweli wowote.

Kwa mfano unasema ...katika picha hii kuna galax 10000 na kila 1 ina nyota bilion 100. Na hiki ni kaeneo kadogo tu katika anga! haya manyota yote na ukubwa ulisema pamoja na umbali uliosema wa karibu km 1600 yanakaeje huko angani?

Ukaendelea tena, chuo kikuu cha Hawaii kilifanya utafiti wa kutosha kukokotoa kila punje ya mchanga hapa duniani wakagundua kuna 7.5 quintillion za mchanga na kila punje inawakilisha nyota 10000 katika universe! Ajabu uwiiiiii! Hii ni nini jamani? Mm nitakuwa wa mwisho kuamini. Yaani hawa jamaa wanajua idadi ya punje za mchanga?

Hapa ndio ulinimaliza kabisa uliposema kijiko (nerton) cha chai kina uzito sawa na mapiramidi 900 yaliyoko pale misri! hawa jamaa huwa wanaandika wakia wamelewaeh! Heeh! Hii kali.

Mkuu Mgalanjuka haya makitu uliondika ni fikra za watu na ni ubabaishaji wa kiwango cha juu. Naomba nitofautiane na wewe.

Atakuja anahema kwa ukali huyo, hapendi kabisa ubishe anachoandika
 
Last edited by a moderator:
Aisee Qyberteq, ndio tabu yenyewe hii. Nilitaka nione ni upeo gani hawa watu wanao lakini naona nimepata jibu baada ya kuona post zao zilizofuata. Lakini inashangaza pale mtu asipoelewa yeye that makes everything false. Na wale wote wanaoelewa basi kwake wamepotoka. So how can we move forward? Ndio sababu ya kuwaelezea kwa njia rahisi kabisa lakini labda ni kwa faida ya watu wengine wanaopenda kufahamu lakini sio wao.

Mbona haya mambo unayoandika ni ya kawaida sana ila wewe unatulazimisha tuone ni mambo makuuuuubwa!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom