Ukweli wa Kustaajabisha Kuhusu Nyota za Angani

Ukweli wa Kustaajabisha Kuhusu Nyota za Angani

Status
Not open for further replies.
Ama kweli Mungu yupo na anapaswa kuogopwa kuliko kawaidaaa!! mtoa maana asante sana
 
mmh! sayansi zingine hizi unahitaji muda wa ziada kumezs
 
Kwangu hili darasa, halina saaaana mapya, mengi aliyoyasema hapa nimeyajuanikiwa shuleni. Lakini kama hukuwahi yapitia, ni mwanzo mzuri wa kujifunza na kujua kitu.

Mtoa mada ni mwandishi mzuri sababu anaelewa anachoongelea, kama unapenda kujifunza na hukuwa unafahamu haya ni mwanzo mzuri. Changamoto iko kwenye mahesabu na kujua assumptions zilizotumika kufikia conclusion fulani. Haya yote kama unataka kujua inabidi usiwe mvivu.

Imagine mie niliprint na kumpelekea kijana wangu wa darasa na nne, alisoma yote, alifurahi akawa na maswali milioni kidogo. Mengine nikamjibu mengine nikamwambia with time ataelewa, anahitaji kujua vitu vingine kabla hajaelewa kila kitu katika mada hii. Kiukweli alikuwa over excited, nilimpelekea sababu najua yuko interested.

So hata wewe kama unapenda, with time ukiwa unasoma soma utaelewa tu.

sisi pia tupo angani...hayo manyota na magalaxi yapa anga za mbali. We unaonaji hili darasa?
 
how do you know vilipangwa?!!

Kwa jinsi vilivyopangiliwa" ni ishara tosha kwamba kuna mtu aliyepanga.. wewe kama huelewi chochote utawezaje kusema muumba wa hivyo vyote hayupo! au uliumba wewe hizo galaxy na nyota?
 
Kwa jinsi vilivyopangiliwa" ni ishara tosha kwamba kuna mtu aliyepanga.. wewe kama huelewi chochote utawezaje kusema muumba wa hivyo vyote hayupo! au uliumba wewe hizo galaxy na nyota?

If complexity and order must have someone to create it, surely that someone must need a creator, and that creator another creator, ad infinitum, ad absurdum.
 
If complexity and order must have someone to create it, surely that someone must need a creator, and that creator another creator, ad infinitum, ad absurdum.

Rafiki Mungu yupo...
 
naona mnataka kuanza kuleta zile siasa zenu tulizo zizoea ktk mabandiko mengine.
tafadhali msije mka divert maudhui yote ya hii thread na kuleta ya kwenu.muacheni mleta mada atupe ilm hii adhimu.
acha niwaombe hawa wakuu watuthibitishie hicho ulicho gusia ktk post yako. Ishmael kahtaan & Eiyer .

Mwambie kaa anakubali kuwa kimantiki hakuna kinachoweza kuwepo tu bila kuwekwa ni kitu gani kinamfanya asikubaliane na kuwepo muumba wa aliyeviumba vilivyoumbwa?
 
ahsante kwa uzi mzuri..mimi nahitaji kujua jinsi ya kuzisoma hizo nyota zikiwa angani.kuna maumbo ambayo hujipanga na yana maana yake.

Download Google sky map utafaidi na kujifunza mengi
 
Mkuu kwani huwezi kukomenti bila ku-quote uzi mzima...???
Unatupa shida tunaotumia simu mkuu

mbona mimi natumia simu na sioni tatizo?anyway jaribu kununua simu yenye uwezo zaidi.
 
Mkuu 072, Haina tabu ngoja tuwasome tu labda tutajifunza kitu.

What is the ultimate origin of stars mkuu, according to your cosmogony.

Umeleta mada nzuri sana, labda tukuchimbe zaidi kupata elimu zaidi.
 
Halafu huwa unaniudhi na kiingereza chako hicho! Mwenzako Mgalanjuka ameleta ilmu kwa kiswahili we unakuja kujambajamba hapa hoo sijui yu now vis is tangs just a dream my color bak its so cold no air, alaah! We si mmakonde wewe?
Mnajifanyaga wajanja mnatuzuga na inglish kwa kutupakulia kidogo sasa leo mkuu Mgalanjuka amemwaga pilau hadharani kila mtu ajilie anvyotaka na ninyi ndio mnakuja hoo sijui pilau lina mawe, hoo I no very very about this, kwa nini hukutuletea kwa lugha nyepesi kama yu know?
 
What is the ultimate origin of stars mkuu, according to your cosmogony.

Umeleta mada nzuri sana, labda tukuchimbe zaidi kupata elimu zaidi.

Mkuu Kiranga, according to astronomy and science idea yenye uzito ni Big-bang theory as origin of matter space and time including stars as source of planets which accommodate us. You know that very well. I could see you guys debating on whether God is there or not. My side is we absorb the available knowledge, think by our brains and from what we got and understood we decide for ourselves.
 
Nashukuru sana Mr. Mgalanjuka kwa kuonyesha dhahiri umuhimu wa elimu ya astronomia katika kuleta udadisi, kutengeneza fikra mpya na hali ya kupenda sayansi. Kama ulivyo wewe nami naipenda elimu hii kwani kila siku siachi kujifunza jambo jipya. Kutokana na kuipenda kwangu huwa natumia muda wangu wa ziada kuwafundisha watoto na jamii kuhusu mambo haya. Suala la kuchanganya elimu hii na astrology halina budi kufanyiwa kazi ili watu waweze kuielewa elimu hii na kunufaika nayo, vivyo hivyo katika suala la uwepo wa Mungu na Imani zetu. Nimependa ulivyoacha kila mtu aamue mwenyewe kutoka na imani yake na uelewa wake. Naomba uendelee kutujuza mengi zaidi
 
Mkuu HKBW, shukrani. Nakubaliana nawe katika hili la kuheshimu misingi au taratibu fulani za watu ili tupate nafasi ya kuelewa zaidi mambo mengi yanayotuzunguka. Katika mambo yanayotutofautisha na viumbe karibu vyote ni jinsi ubongo wetu ulivyo na nafasi kubwa ya kufikiri na kuamua hivyo ni wazi mambo mengi sana itategemea mtu ataamuaje kwa nafasi yake mwenyewe. Ndio maana tukiwa wazi na kujifunza zaidi kuhusu kila kitu basi kuna wale watakaoona uwepo wa Mungu na wengine wataona hayupo na hivi na vile kila mtu kwa utashi wake.

Miaka ishirini iliyopita binadamu wote hatukujua habari yoyote ya sayari nyingine tofauti na zile zinazolizunguka Jua. Leo hii kuna sayari karibu 1900 ambazo tunazijua kwa hakika nje ya mfumo wa sayari yetu ya Jua na nyingine takribani 3500 ziko njiani kuthibitishwa uwepo wake. Hii si kwa kuhisi bali kwa chombo kinachozunguka anga za mbali (Kepler) kikiwa na telescope na vifaa vingine vya hali ya juu kikileta maarifa mazito ambayo ni ya thamani kubwa kwetu. Kwangu naona ni muhimu tuki-share na kujadili mambo kama haya na mengineyo mengi kuliko vinginevyo.

Si kwamba sio vizuri kujadili kila kitu kwa uwazi lakini tayari inajulikana mijadala kama hiyo ya kuwepo na kutokuwepo Mungu kwa hapa JF inasababisha uzi kutupwa kule jukwaa la dini ambapo si wengi wana-access au interest mimi nikiwa mmoja wao.
 
Nakuheshimu sana mkuu Mgalanjuka sio tu kwa kuleta hii mada, Bali kwa Uvumilivu wako kwa kujibu maswali hata ya kuudhi. Wewe ni Mwalimu mzuri sana, ni vema tukakutumia vizuri kwa faida ya kizazi hiki. Asante sana.
Ova.
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom