Mkuu
Mgalanjuka, swali langu lina sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo.
umetuambia kuhusu idadi ya galaxy kwamba ni nyingi sana na sisi tupo kwenye kagalax kamoja tu kanakoitwa milky way, sasa je,
(a) Hakuna uwezekano wa kuwepo sayari kama hii katika galaxy nyingine yenye binadamu wazuri wazuri kama hii na wenye akili kama/zaidi ya sisi?
(b) Katika maafa yanayoweza kuikumba dunia, je, kitu kinachoitwa nibru (sijui kama nimepatia kuandika) kinachozungumzwa sana miaka ya karibuni unakizingumziake?
SWALI LA NYONGEZA:
Kuna utafiti wowote wa kisayansi uliowahi kufanywa kuhusu sehemu (a) hapo juu na majibu yalikuwaje?
Mkuu Capitalist, nitaelezea kwa kifupi na kwa lugha nyepesi.
Tuanze na kipengele (a)Uwezekano wa kuwepo sayari kama hii katika galaxy nyingine yenye binadamu wazuri wazuri kama hii na wenye akili kama/zaidi ya sisi.
Ni ukweli usio na shaka kwamba kuna nyota nyingi sana zinazofanana na jua letu katika maeneo mengine ya mbali sana katika universe. Wanasayansi wanasema nyota zinazofanana na Jua letu ni kati ya asilimia 5 hadi 20 ya nyota zote katika universe tunayoweza kuiona (observable universe). Hili neno la universe tunayoweza kuiona lina maana kwamba pale tusipoona basi kuna uwezekano universe inaendelea au kunavitu vingine tusivyovijua lakini makadirio yanayofanyika ni ya ulimwengu tunaoweza kuuona. Sasa ukumbuke katika mada nilisema nyota zinakadiriwa kuwa sextillion 100 au zaidi katika ulimwengu tunaoweza kuuona sasa tukisema mfano tuchukue tu asilimia 5 yake, basi tutakuwa tunaongelea nyota bilioni-bilioni 500 zinafanana kimazingira (joto, ukubwa, umri, aina, uwepo wa sayari) na jua letu.
Sasa kwa number hizi basi ina maana uwezekano wa kuwepo sayari zenye maisha ni mkubwa ingawa maisha yanaweza yasiwe haya tunayoyajua sisi. Hapo kabla niligusia tafiti iliyofanywa na PNAS (
Proceedings of the National Academy of Sciences) ambayo inapendekeza kwamba kuna angalau asilimia moja (1%) ya sayari zinazofanana sana na dunia yetu katika hizi nyota zinazofanana na jua.
Kuwa na binadamu wanaofanana na sisi hilo linawezekana lakini kumbuka kisanyansi mazingira yanachangia sana mwonekano au matokeo ya viumbe. Kama mazingira yakiwa tofauti kidogo basi matokeo ya maisha au viumbe yatafuata mkondo. Hili tunaliona hata katika viumbe wa kawaida wa duniani jinsi wanavyokuwa na vigezo vinavyoendana na wao kumudu mazingira yao. Kwa kuwa hata hizi sayari zinazofanana na dunia haziwezi kuwa na mfanano pacha yani circumstance zile zile basi tusitegemee kukutana na viumbe "wanaofanana asilimia mia na sisi". Jinsi kila kitu kinavyoonekana leo hii ni matokeo ya jinsi mazingira yalivyokuwa miaka milioni iliyopita na vivyo hivyo kadri muda unavyoenda.
Kuwa na akili zaidi yetu au kuwa na maendeleo na technology kubwa sana zaidi yetu hili ni wazi na lina sababu zake. Kwanza kuna uwezekano wa utofauti wa maisha kuanza hivyo kufanya viumbe wengine kama wapo basi wendine wanaweza kuwa wame-evolve zaidi yetu kwa kuwa na muda mrefu zaidi katika ulimwengu. Kama tukichukua mfano wa dunia yetu (Earth), maisha yanakadiriwa kuevolve kutoka katika simple form kati ya miaka bilioni 3.5 iliyopita hii ni kutoka kwa evolutionists. Kuna sayari zilizo na muda mrefu zaidi ya dunia na hapa lazima utaona katika hali ya kawaida sisi ndo tunaanza na kuna wengine waliokwisha piga hatua kubwa sana. Na hata tukisema katika sayari nyingine kuna viumbe waliumbwa kabla yetu (Creationists) alafu sasa tujilinganishe nao lazima watakuwa wametuzidi mbali.
Pili, kama kuna kiumbe kikifika katika sayari yetu basi hii ina maana technology inayowezesha kusafiri umbali huo si ya kawaida. Katika mada nimeongelea huge distances kutoka eneo moja hadi jingine. Hata nyota iliyo jirani yetu si rahisi kuifikia kwa technolojia ya usafiri tuliyonayo sasa. Miaka elfu sabini njiani kwa speed kali kabisa ambayo space shuttle inaweza kwenda.
(b)Kuhusu Nibiru. Hii ya Nibiru au planet X haina ukweli wowote na wala haipo. Astronomers na wanasayansi (sio wote) wala hawahangaiki na habari hii kwa kuwa haina uthibitisho wa kisayansi zaidi ya tafsiri flani za symbols za jamii za zamani. Ila kama kuna mwenye uthibitisho au misingi iliyosimama vizuri kuhusu hili atuwekee tujadili.