Uwepo wa sayari nyingine nyingi inje ya mfumo wa jua letu na zilizotengeneza mfumo kama wa solar system yetu ambako inadhaniwa kuna uhai mwingine kwa sababu angani sayari na nyota ni nyingi.
Jua letu ni nyota iliyopo karibu ina mfumo wa sayari zake zinazolizunguka.
Nyota nyingi angani zina mfumo kama wa jua letu na zina sayari zinazo jizungusha kama ilivyo ktk jua letu.
Miaka billion 12 iliyopita kulitokea mlipuko (big bang) chembechembe zilijikusanya na kutengeneza sayari na nyota na vyote vilivyomo ulimwenguni.
Utata kuhusu kupatwa kwa mwezi ni utata uliomalizwa na science watu waliamini mwezi unanaswa na jua wakati mwezi upo mbali sana na jua 92million umbali.
Halafu sisi wengine na umri wetu huu mdogo kiasi utata huo umetupitia mbali mno,yaani hatujawahi kutatizika hata kwa bahati mbaya yaani tunapata elimu sahihi kuhusu vitu hivyo na sisi tunavifanyia kazi.
Sasa ngoja nikupe faida nyingine,kutokana na kile ulichokigusia yaani kupatwa kwa mwezi.
Waislamu tuna kalenda yetu,yaani ina tarehe na miezi,kwa wote hakuna shaka ya kuwa idadi ya miezi ipo kumi na mbili tangu ilipoumbwa hii dunia.Kwa waislamu miezi huwa ina siku 29,na mara chache sana huenda mpaka siku ya 30,ndipo mwezi huandama.
Kawaida jua hupatwa pindi mwezi unapopotea katika uso wa dunia yaani ardhini,na jua halipatwi isipokuwa katika tarehe ya 28 au 29,hii ni kwa mujibu wa kalenda ya hijiriya.Kwahiyo ni juu yako kama utakuwa ni mtu wa kupenda kujua ukweli.Kwa mfano kwa Tanzania juzi lilipopatwa jua ilikuwa ni tarehe 1.9.2016 sawa na yarehe 29.11.2016.Huo ndio muujiza wa Mola kutuonyesha sisi kwamba yeye upo.Katika kupatwa kwa jua tarehe hizo hazibadiliki.Kama Mola akikupa uhai,ukisikia tena jua limepatwa wewe ulizia ni tarehe ngapi katika kalenda ya hijiriya.
Tukirudi katika suala la kupatwa kwa mwezi,inajulikana ya kuwa mwezi una njia zake na vituo vyake,nidhamu hiyo ameiweka yule mjuzi wa kupangalia mambo hasa.Jua na Mwezi haviingiliani katika njia zao wali kimoja hakimtangulii mwenzie wala havidirikiani.
Mwezi haupatwi isipokuwa katika siku ya 13 au 14 au 15 tangu unapoandama.Hii ni kwa mujibu wa kalenda ya hijiriya kwahiyo utatafuta muwafaka wake na kalenda ya miladiya.
Tofauti yetu sisi na wayakinifu sisi vitu hivi kamwe havitupi utata na tunajua kwanini kuna kupatwa kwa jua na kwanini kuna kupatwa kwa mwezi.Mpaka kesho kiyama hakuna mwanasayansi atakayekwambia kwanini kuna kupata kwa jua au mwezi,sio kwanini mwezi umepatwa au jua.
Sisi tumeitangulia sayansi mbali sana,sababu tunaujua ukweli ambao wao hawaujui tena kwao wao mpaka wafanye majaribio na dhana zao.Mimi najua ni tarehe gani jua au mwezi utapatwa tena.Hatukuoteshwa bali tumesomeshwa ukweli.