Ukweli wa uwepo wa Mungu na Makazi yake upo hapa

Sayansi inatanuka Roho ya mwanadamu ni Mungu tosha na inatosha kabisa kuleta majibu ya kila jambo huko unakosema hakufikiki patafikika tu kama pameshagundulika ni swala la muda tu
Mda utaongea
 
Pole kwa banned
 
Mungu ndie mpangaji wa yote tumezaliwa tutakufa sioni maajabu kufa ni lazima haijarishi tetemeko ,njaa, vita ,n.k kufa ni kufa tu
Kama mungu ndiyo mpangaji kwahiyo moja kwa moja mungu wako ni muuaji sasa.

Pia kwanini atuletee haya mabalaa yote mfano njaa, tetemeko n.k?

Yeye si anadai kuwa una upendo, mwingi wa rehema.

Kwanini asiyazuie hayo mambo mabaya yanayowatesa watu wake anaowapenda?

Kulingana na unavyomuelezea atakuwa ni mnafiki mkubwa sana Mkuu!

Chukulia huu mfano wa kawaida-- hakuna mzazi wa kumuua mtoto wake kisa kamkosea mbali na kumuonesha njia sahihi anavyotakiwa aishi!
 
Mkuu, Kifo ni sehemu ya maisha kufa Si dhambi labda kujiua ni dhambi ila kama mda wako ukifika ni mipango ya Mungu kwa kuwa kuna maisha inje ya mwili.

Mungu ni mwenye upendo na hakuna kifo kisicho umiza kwa jinsi yoyote.

Siku ukifahamu ukweli wa maisha inje ya mwili utatubu na Mungu atakusamehe
 
Aisee Asante sana
 
Ulimwengu umejaa mambo mengi ya kustaajabisha
 
Mungu Si mwanadamu na kila jambo amelipanga kama alivyoona inafaa kwa utaratibu wake.
 
Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jibu na la Bwana Libarikiwe
Mnaongozwa vibaya kutumia mstari wa Biblia. Kumbuka kwamba maneno hayo yalitamkwa na Ayubu kwenye Ayubu 1:21 baada ya kupatwa na majanga makubwa likiwemo la kufiwa na watoto wake wote. Alikuwa akimlaumu Mungu kuwa ndiye alimletea mabalaa yote hayo kama wewe na wengine mnavyomtuhumu Mungu kuwa muuaji. Ukiendelea kusoma sura zinazofuata za Ayubu, aliendelea kumlaumu na kuilaani siku aliyozaliwa. Baada ya kuongea mambo mengi ya shutuma dhidi ya Mungu, Mungu anaanza kumjibu Ayubu kuanzia Sura ya 38 ya kitabu cha Ayubu, anamuuliza maswali mazito ambayo Ayubu anashindwa kujibu.
Kwenye Sura ya 40:4 Ayubu anasema;"Tazama! Nimekuwa kitu kisicho na maana. Nitakujibu nini? Nimeuweka mkono wangu juu ya kinywa changu. 5. Nimesema mara moja nami sitajibu; Na mara mbili, nami sitaongeza lolote. - NW.
Baada ya Ayubu kujibu hivyo, Mungu aliendelea kumuuliza maswali ambayo Ayubu alishindwa kuyajibu. Ndipo sasa kwenye Ayubu 42:1-5 Ayubu anaujua ukweli kumhusu Mungu na mambo makubwa aliyoyafanya na kukiri hivi.. "Nimesikia habari zako kwa fununu, lakini sasa jicho langu mwenyewe linakuona wewe. 6. Ndiyo sababu NINAYATANGUA NILIYOSEMA NAMI NINATUBU KATIKA MAVUMBI NA MAJIVU". - NW.
Ayubu aliyatangua yote aliyomshutumu Mungu likiwemo lile alilosema "Bwana anatwaa" , na akatubu makosa hayo, inakuwaje leo mnafanya makosa hayo hayo na hamtubu? Na mnaendelea kufundisha watu kwamba Mungu ni muuaji?
 
Mkuu nadhani umeni quote vibaya hakuna nilikosema Mungu ni muuaji.
Mungu ameumba kila kitu ni vyovyote atakavyo kufanya kama anavyoona inafaa
 
Samahani ndugu yangu, ulimaanisha nini kwenye hizi nyuzi zako?
Mkuu, Hizo nyuzi nilikuwa nikijibu anayepinga uwepo wa Mungu ili afahamu Mungu amefanya kila kitu kwa mpangilio wake kama alivyo ona inafaa.
Naamini uwepo wa Mungu kwani kuishi kwangu ni Kristo.
 
Nibiru ni tishio lingine katika Dunia yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…