Peter Mwaihola
JF-Expert Member
- Jun 23, 2022
- 289
- 489
Kumekuwa na vuguvugu na dalili za mgawanyiko kuhusu msimamo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA kupitia kaulimbiu No Reforms No Election iliyoasisiwa na chama hicho chini ya mwenyekiti wake Tundu Lisu.
Mgawanyiko huo wa kimtazamo unatokana na kampeni ya kutoshiriki uchaguzi pasipo mabadiliko hivyo kushinikiza mabadiliko yafanyike katika mifumo ya kusimamia uchaguzi kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025.
Hivi karibuni umoja wa waliowahi kuwa wabunge wa chama hicho unaojiita G-55 umetuma walaka kwa katibu mkuu wa chama hicho kueleza umuhimu wa chama hicho kuachana na mpango wa kutoshiriki uchaguzi pamoja na kutahadharisha kuwa kitendo cha chama hicho kutaka kuzuia uchaguzi usifanyike kinaweza kuwa na viashiria vya uhaini.
Hata hivyo msimamo wa mwenyekiti na Viongozi wakuu wa chama umebaki vilevile huku wakiendelea na ziara nchi nzima kuelimisha wananchi na wanachama wao juu ya kampeni yao ya mabadiliko.
Lakini kuna swali watu huulizana kuwa Tundu Lisu anaipeleka wapi CHADEMA na wengine hujiuliza mgawanyiko wa kifikra uliopo hauwezi kukiua chama? Na msimamo wa chama kutoshiriki uchaguzi pasipo mabadiliko katika mfumo wa uchaguzi hauwezi kukiathiri chama iwapo hakitoshiriki uchaguzi?
Tundu Lisu mwenyewe anasema hakuna haja ya kushiriki uchaguzi ambao chama tawala kimeandaa ushindi wake kabla ya kufika kwenye sanduku la kura na anasisitiza kuwa kama kuna mwanachadema anataka kuwa na haki ya kushinda uchaguzi na atangazwe kuwa mshindi basi ajitoe kwa moyo wake kushinikiza mabadiliko yafanyike.
Tukirejea nyuma kipindi cha uongozi wa Freeman Mbowe akiwa mwenyekiti wa CHADEMA wanachadema wengi walikuwa wanalalamika juu ya upole wa mwenyekiti katika harakati za chama kwakua muumini mkubwa wa maridhiano na serikali pamoja na chama tawala.
Wengi waliamini kuwa chama tawala hakiwezi kukubali kufanya mabadiliko ya kikatiba kuruhusu tume ya uchaguzi itende haki hivyo maridhiano hayakuwa na maana.
Kuelekea uchaguzi wa ndani ya chama wanachama wengi waliweka imani kwa Lisu kuwa angebadilisha siasa ya chama hicho na kuwa chama cha kiharakati chenye kuchochea mabadiliko ya haraka na kurejesha imani kwa wafuasi wake ambao walikuwa wamekata tamaa.
Ujio wa Tundu Lisu unaakisi mabadiliko makubwa ya tabia ya siasa ya chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania kwa kuleta taswira ya harakati na msimamo mkali wenye Itikadi ya mabadiliko kama ilivyo kwa vyama vingine vinara vya upinzani katika nchi mbalimbali kama vile Movement for Democratic Change nchini Zimbabwe chini ya Nelson Chamisa, Economic Freedom Fighter cha nchini Afrika kusini na vyama vingine ambavyo vimekuwa mwiba mkali kwa serikali katika nchi husika.
Peter Mwaihola ni Mwandishi wa maudhui na mchambuzi wa masuala ya siasa na jamii.