Ukweli wenye kusikitisha

Ukweli wenye kusikitisha

Lamzettttt

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2020
Posts
1,218
Reaction score
3,481
Wanawake wamefanya kila kitu ili kuvutia macho ya wanaume... Wengine kwa waume zao, wengine kwa kila mtu. Makeup, kuchonga mwili, nguo fupi na tumbo wazi, kifua nje nje, urembo na cosmetics, kujitongozesha na kujipendekeza.

KISHA NINI?
Jicho la mwanaume bado linatafuta zaidi! Na linatizama kulia na kushoto ... na linachukua kutoka hapa na pale!

Usaliti katika mahusiano unazidi kuongezeka.
Hakuna kinachokidhi silika, kinachoshibisha matamania ya manaume. Matangazo ya wanawake yameongezeka! Na bidhaa hiyo imepewa leseni ya uhalali. Wanawake wamekuwa ni bidhaa rahisi mno!

Matokeo
Hakuna mwanamke anayeweza kujaza macho ya mwanaume na kumtosha isipokuwa kufahamu thamani ya utu wake na uchamungu unamtosha. Kumcha Mungu ndiko kunakofanya macho kuinama chini na moyo kuacha matamanio kwa kumcha Mungu.

Zaidi ya hayo, ni bidhaa ambayo mwanamke huyo ndio mwenye kulipa thamani yake. Kupenda wala kusifiwa hakufai kitu isipokuwa ni kwa kulinda sheria za Mwenyezi Mungu.

Nimeipata >>Hadi Tv Swahili

FB_IMG_16964254028050315.jpg
 
Imekaa vizuri

Hapa chini nifafanulie kidogo lugha imenipiga chenga
Zaidi ya hayo, ni bidhaa ambayo mwanamke huyo ndio mwenye kulipa thamani yake. Kupenda wala kusifiwa hakufai kitu isipokuwa ni kwa kulinda sheria za Mwenyezi Mungu.
 
Kuna nguo naiona huko mitandaoni manzi akivaa anakuwa kama Niki minaji ila hutakiwi ukae,uheme,au ujisaidie,Sawa ila manzi yangu akivaa hivi napiga chini siku hiyo hiyo,Bora niweke ndani kiazi mviringo ntachemsha.
 
Back
Top Bottom