Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
Nadhani wote tunaelewa Wanasiasa na Ulaghai / Kulaumu wengine ni pete na Kidole....; Mdau mmoja alisema.... To err is human. To blame someone else is politics.
Nashangaa pale Chama tawala wanapolaumu wapinzani ni kama dereva kulaumu abiria wakati yeye ndio anaendesha (lakini naelewa wanajilinda waendelee kutawala).
Na Wapinzani wanapopinga ndio kazi yao wala sishangai; lakini productively badala ya Watawala kupoteza muda labda wangejipima kwa kipi wamefanya kutokana na walichosema watafanya. Na wapinzani wangejikita kwenye kuonyesha nini hakijafanyika na wao wangefanya nini tofauti.
Tatizo imekuja hii Kasumba ya hawa Wanasiasa (Wapinzani) kuanza kulaumu maboss wao...; yaani sisi tunaowalipa Ruzuku na wabangaizaji ambao tumewaweka pale ili wafanye hilo wanalofanya na sisi tufanye mengine... Unasikia jamaa anasema Watanzania wanajua kuongelea tu Mpira (Sasa wanataka nini, labda hatuongelei Siasa hawajaifanya iweze kuongeleka) yaani wanasema kama vile wana-magic wand kwamba wao wakipewa uskani mambo yote yatakuwa Kosher.
Mwingine anasema hata taarifa hamuangalii ni miziki tu. Sasa kwa kinachoendelea Vijembe na Ulaghai si bora mtu ajiridhishe kwa kupunguza maumivu kwa hivi viburudisho? Najiuliza hivi bila hawa wadau (Mipira na Wasanii) kufanya kazi yao ipasavyo jambo ambalo wanasiasa hawafanyi si maisha yangekuwa magumu maradufu?
Angalizo; Endeleeni kunyosheana vidole lakini tusivunjiane heshima kwa kutaka kuingia kwenye starehe zetu chache zilizobaki na kutulaumu sisi wakati nyie ndio mna-under-perform. Sisi huku kitaa tumefanya yetu kwa kuwalipa na kuwaweka hapo mlipo, na mkizingatia Ulaghai wenu huenda hatuna Imani ya kwamba mtafanya mnachosema. Sasa it's up to you to convince us; na kama bado hatuwaelewi ongezeni bidii.