Ulaji huu wa mafuta ni kawaida?

Ulaji huu wa mafuta ni kawaida?

Banned

Member
Joined
Apr 7, 2013
Posts
47
Reaction score
13
Salaam wadau!

Nina toyota Vitz 2000 1300cc ambayo haina hata miezi mitatu tokea iingie Tanzania!
Nilihakikisha fuel tank mafuta yameisha nkatia mafuta 27Lts na kwenye fuel gauge ilionesha 5 bars na tokea niweke mafuta nimetembea 205Kms na naona bar ya mwisho ina Blink(Naweza ifananisha na Nearly Empty 'E" kwenye magari mengine) na kwa experience yangu haitozidi 20Kms mafuta yataisha.Hivo on average itakua inatumia 8Kms/lt.
Pengine utakua unajiuliza kwa nini nisisubiri mafuta yakaribie kuisha kabisa ila inshort ni kwamba hii gari imewai nizimikia bila kuleta kwenye dashboard.

Hii gari naitumia kwenda kazini sehemu nakopita ni rami tupu isipokua sehemu kama ya 700ms ndo barabara ya vumbi na vishimo vya hapa na pale,njiani hakuna foleni ni moja kwa moja.
Kutoka Nyumbani mpaka kazini ni around 7Kms kwenda na kurudi na mara zote vioo nakua nimefunga na imekua nimewasha A/C isipokua mara chache kama kuna ubaridi.
Nimeifanyia service mara moja so far na vitu vilivyofanyiwa service ni Engine Oil,Gearbox Oil,Oil filter na Air cleaner pekee.
Plugs na Brakepads mafundi walisema hazina shida.

GearBox Oil ilotumika ni zile za Lubex
Wakati Engine Oil ilotumika ni ya FUCHS TITAN Super Formula na viscosity values zake ni 20W-50 japo Ukisoma Manual online inaonesha recommended viscossity ni SAE 5W−30 na wamesisitiza for Good fuel economy iwe hiyo viscosity.
Sasa hii fuel consumption kwa gari kama hii ni kinyume na matarajio yangu ya 12-14Kms/lt ambayo nimeyasoma mitandaoni humu.

Je shida inaweza kuwa hiyo Oil ilotumika au ni kitu gani?
Naombeni uzoefu wenu maana mimi ni mgeni kwenye haya mambo.

Natanguliza shukrani!
 
Ipeleke kwa fundi ikakaguliwe, kuna gari ina 1500cc ilikuwa inatumia 9km/l. Ilikutwa na tatizo la Oxygen sensor mass air and flow sensor na nozzle moja ilikuwa inamwaga mafuta zilipobadilisha ikaanza kutumia 15-16km/l.
Inawezekana na gari yako ikawa na tatizo kati ya hayo.
 
Kinachokumaliza ni hiyo 20w-50 ndio mana consumption iko juu... ukitaka kuamini weka castro 5w-30 utaona tofauti mimi nilifanya makosa hayohayo nilimwaga oil iliokuja na gari nikajichanganya nikaweka 20w-50 lita sita engine ya V6 ndani ya siku moja tu nilianza kuona gari imekuwa nzito na mafuta yanakwenda haswa nikaingia hasara nikaimwaga na kubadili hadi filter nikaweka castro 5w-30 recommended aisee raha sana gari nyepesi sana mafuta kiduchu nasafiri mkoani safi na ni km 10000 ila kwasasa nimeshafagia km 6000 nataka next week nitoe niweke mpya
 
nimekuwa interested hapo,
cjaelewa vizur hzo code, tofauti ya 20w-50 na 5w -30 ni ipi,
ipi ni nzur kwa gari ndogo kama starlet..
shukran
 
Hukupaswa kubadili gearbox oil...engine oil weka recommended oil not otherwise.
Gari ya CC1300 consumption rate yapaswa kuwa 1lt kwa 10km to 15km....city and highway respectively

Baadhi ya mafundi si unajua tena mkuu!
Nilishapitia mjadala hapa chini nkawa najua haina haja kubadili nkawambia wakasema watacheki kama inafaa so mwisho walibadili na ndo ishatokea.
Muda Gani Baada ya kununua gari kutoka Japan unatakiwa kumwaga Oil ya Gearbox?

Ila nilisoma hapa hapa jukwaani kwamba with time hiyo gearbox oil mpya inaji redistribute vizuri na consumption ina normalize
 
Kuna fundi nimempelekea leo anasema zitakua Plugs inabidi zibadirishwe hili nalo vipi wadau/
hayo maswala mengine hajaongelea kabisa
 
Kuna fundi nimempelekea leo anasema zitakua Plugs inabidi zibadirishwe hili nalo vipi wadau/
hayo maswala mengine hajaongelea kabisa
Kama mdau alivyosema hapo juu, hiyo specification ya oil ndio inakumaliza. Ishanikuta pia kwenye gari la 1.8cc. Niliweka oil ya 20w-50, niliishia kuimwaga kabla ya wakati. Weka recommended oil. Hiyo ya 20w-50 nilitembea 200km tank likaisha, baada ya kubadili, nikaenda 400km na gari kuwa nyepesi.
 
Kinachokumaliza ni hiyo 20w-50 ndio mana consumption iko juu... ukitaka kuamini weka castro 5w-30 utaona tofauti mimi nilifanya makosa hayohayo nilimwaga oil iliokuja na gari nikajichanganya nikaweka 20w-50 lita sita engine ya V6 ndani ya siku moja tu nilianza kuona gari imekuwa nzito na mafuta yanakwenda haswa nikaingia hasara nikaimwaga na kubadili hadi filter nikaweka castro 5w-30 recommended aisee raha sana gari nyepesi sana mafuta kiduchu nasafiri mkoani safi na ni km 10000 ila kwasasa nimeshafagia km 6000 nataka next week nitoe niweke mpya
nimekuwa interested hapo,
cjaelewa vizur hzo code, tofauti ya 20w-50 na 5w -30 ni ipi,
ipi ni nzur kwa gari ndogo kama starlet..
shukran

this statement is very true, faced the same issue nlibadili oil na kuweka ile ambayo haikuwa recommended kwenye gari, nikachange na kuweka inayotakiwa (Catrol 5W-30) and the changes were amazing, japo castrol yenye hiyo viscosity rating ni bei ndefu
 
nimekuwa interested hapo,
cjaelewa vizur hzo code, tofauti ya 20w-50 na 5w -30 ni ipi,
ipi ni nzur kwa gari ndogo kama starlet..
shukran
5w30 ni nyepesi kuliko 20w50..
Hivyo inashauri wa kwa nchi zenye baridi sana nywkati za asubuhi na joto kali mchana utumie 5w 30..
Wepesi wa oil hii unafanya kufika sehemu za engine kwa urahisi zaidi pale unapowasha gari wakati engine imepoa..
Pia 5w30 ina viscosity nzuri zaidi na inahimili joto kali zaidi la engne na inahimili baridi kali..
20w 50 ni oil maalum kwa mazingira ya nchi zenye joto kali kuliko joto la Dar..
nchi kama huko Uarabuni nk.

Hivyo wepesi wa 5w30 unafanya engine yako ifanye kazi kwa wepesi zaidi ndiyo maana inasaidia kwenye fuel economy.

Wengine wataongezea
 
THIS KIND OF INFORMATION wengi hawana. na hili ni jambo ambalo wengi linawapa shida sana.so ni vizuri watu wapewe hii elimu waelewe umuhimu wa matumizi haya ya oil na viwango vyake. mimi mwaka flani nilikuwa na gari ndogo ambayo imeandikwa kabisa kuwa engine oli yake ni 5W 40 But nikawa nmeenda kwa muuzaji flani POSTA akanishauri ninunue 20W 50 akisema kwa kuwa engine imetembea kms zaiodi ya 150,000 then nibadilishe oil. kuwa itakuwa engine nayo inaelekea kuchoka. but nilijaribu sana kuangalia views za watu wengine kwenye mitandao kama zitasema kitu kama hicho kwa wenzetu sikuwah pata.
so i bought the recommended one 5W 40.

5w30 ni nyepesi kuliko 20w50..
Hivyo inashauri wa kwa nchi zenye baridi sana nywkati za asubuhi na joto kali mchana utumie 5w 30..
Wepesi wa oil hii unafanya kufika sehemu za engine kwa urahisi zaidi pale unapowasha gari wakati engine imepoa..
Pia 5w30 ina viscosity nzuri zaidi na inahimili joto kali zaidi la engne na inahimili baridi kali..
20w 50 ni oil maalum kwa mazingira ya nchi zenye joto kali kuliko joto la Dar..
nchi kama huko Uarabuni nk.

Hivyo wepesi wa 5w30 unafanya engine yako ifanye kazi kwa wepesi zaidi ndiyo maana inasaidia kwenye fuel economy.

Wengine wataongezea
 
this statement is very true, faced the same issue nlibadili oil na kuweka ile ambayo haikuwa recommended kwenye gari, nikachange na kuweka inayotakiwa (Catrol 5W-30) and the changes were amazing, japo castrol yenye hiyo viscosity rating ni bei ndefu
Nimepata somo zuri,naenda kumwaga oil 20w50,nakubadili oil filter.
Hiyo 5w30 inapatikana kwenye ujazo gani?na ni bei gani?
 
Nimepata somo zuri,naenda kumwaga oil 20w50,nakubadili oil filter.
Hiyo 5w30 inapatikana kwenye ujazo gani?na ni bei gani?
Mkuu nami nimejifunza hapa, jf ni shule tosha, nimekuwa nikijiuliza sana kwa nini huu ulaji wa mafuta umeongezeka, kumbe engine oil inachangia. Nitahamia Castrol oil maana hata oil ya gear box natumia Castrol kwa sasa, sikuwahi kujua tofauti ya 5w30 na 20w50 kwa kweli.
 
Nimepata somo zuri,naenda kumwaga oil 20w50,nakubadili oil filter.
Hiyo 5w30 inapatikana kwenye ujazo gani?na ni bei gani?
Binafsi huwa natumia Total quartz 9000 5w 30..kuna ujazo wa lita 1 na lita 4.
Hapa nilipo lita 1 nanunua 15000/- lita4 55000/-

Castrol sina uzoefu na bei zake lakini ni oil bora pia kama ilivyo total.
 
THIS KIND OF INFORMATION wengi hawana. na hili ni jambo ambalo wengi linawapa shida sana.so ni vizuri watu wapewe hii elimu waelewe umuhimu wa matumizi haya ya oil na viwango vyake. mimi mwaka flani nilikuwa na gari ndogo ambayo imeandikwa kabisa kuwa engine oli yake ni 5W 40 But nikawa nmeenda kwa muuzaji flani POSTA akanishauri ninunue 20W 50 akisema kwa kuwa engine imetembea kms zaiodi ya 150,000 then nibadilishe oil. kuwa itakuwa engine nayo inaelekea kuchoka. but nilijaribu sana kuangalia views za watu wengine kwenye mitandao kama zitasema kitu kama hicho kwa wenzetu sikuwah pata.
so i bought the recommended one 5W 40.
Tanzania tuna tatizo kubwa la mafundi....Mafundi wetu hawapendi kusoma au hata kugoogle info ambazo zitasaidia kukuza ujuzi wao..

Unakuta gari ndogo chini ya cc 1500 injini teknolojia ya kisasa fundi anakuambia weka oil namba 50... hapo lazima ukione kwenye fuel consumption.

5w 30 ni viscosity recommended kwa gari nyingi sana za teknolojia ya kisasa..

5w 30 ina uwezo wa kuhimili baridi kali sana na joto kali sana...pia inamudu masafa marefu.

Kuna hili suala la mafundi kusema gari ikishatembea 150k km, eti tumia 20w 50....hii elimu sijui wameipata wapi.

Binafsi nina nissani kwenye user manual yake wamerecommend 5w30 na hakuna mahali wameandika mileage ikifika 150k nitumie 20w50.

Mafundi wajisomee wasije wakafanya watanzania wayachukue magari yao.
Wakumbuke engine zinebadilika sana...siku hizi hakuna tena carburator...kuna VVTi, EFI n.k
 
Kama unaishi Dsm, 5w40 au 10w40 inakuhusu. 5w30 inaweza isiwe ideal saana kwa Dsm na mikoa mingine yenye joto kali, maana kuna vipindi joto linazidi nyuzi 35, japo ni vigumu saana kushuka zaidi ya nyuzi 10
 
Back
Top Bottom