Nilipokuwa mtoto mdogo nilikuwa nasikia ukila maharage sana unapata uoni hafifu na mpaka sasa kuna watu wanaamini hivyo.
Mimi ni daktari lakini mpaka sasa sijafundishwa hicho kitu.
Mimi ni daktari lakini mpaka sasa sijafundishwa hicho kitu.
- Tunachokijua
- Maharage ni mbegu zinazozalishwa na mimea jamii ya mikunde inayopatikana kwenye familia ya Fabaceae.
Watu wengi huchukulia maharage kama chakula duni kisicho na faida kubwa kwa afya, lakini ukweli haupo hivyo. Hiki ni chakula muhimu kinachoweza kuimarisha afya ya mwili na kutoa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali hasa yale yasiyo ya kuambukiza.
Faida za kula Maharage
Pamoja na uwepo wa aina nyingi za maharage, yote husifika kwa kuwa na kiwango cha kikubwa cha protini kinachosaidia mwili kuponya majeraha yake na kutengeneza tishu mpya za mifupa, misuli, nywele, ngozi na damu.
Kwa upekee kabisa, maharage ya soya huwa na amino asidi zote 9 zinazotumika kuunda protini.
Virutubisho vya folate ambavyo ni muhimu kwa kutengeneza damu na afya ya mama mjamzito katika kumkinga mtoto dhidi ya mapungufu ya utengenezwaji wa viungo vya mwili hupatikana pia kwenye maharage.
Faida zingine ni kuondoa sumu mwilini, kuimarisha afya ya moyo na mishipa ya damu, kupunguza hatari ya kuuugua saratani, kudhibiti sukari na kulinda ini.
Madai ya kusababisha uoni hafifu
Tafiti za afya zinataja maharage kama chakula bora kinachoweza kuimarisha afya ya macho ikiwemo kuzuia tatizo la mtoto wa jicho na kupunguza athari za mionzi mikali ya mwanga.
Maharage huwa na kiwango kidogo cha mafuta, wingi wa nyuzi nyuzi pamoja na madini ya zinc. Vyote hivi ni vizuri kwa macho.
JamiiForums imepitia pia tafiti mbalimbali za afya pamoja na kuzungumza na wataalamu wa lishe pamoja na madaktari wa Binadamu waliothibitisha kuwa madai ya maharage kusababisha uoni hafifu ni uzushi usio na uthibitisho wowote kisayansi.
Maharage ni chakula bora kwa makundi yote ya binadamu. Hakuna ushahidi wa wazi unaoonesha kuwa husababisha tatizo la uoni hafifu.