Chips ni chakula maarufu sana kinachotumiwa na watu wengi, hasa vijana. Baadhi ya watu huamini kuwa chakula hiki husababisha ugonjwa wa macho hasa kutoa machozi, maumivu ya mishipa ya macho pamoja na upofu.
Je, kuna ukweli wowote kuhusu madai haya?
Je, kuna ukweli wowote kuhusu madai haya?
- Tunachokijua
- Kwa mujibu wa takwimu za WHO, takriban watu bilioni 2.2 duniani ni waathirika wa magonjwa ya macho yanayohusisha upofu na uoni hafifu.
Kwa kiasi kikubwa, sababu zinazopelekea upofu, uoni hafifu pamoja na changamoto zingine za macho ni-
- Uzee
- Mtoto wa jicho
- Kisukari
- Glaucoma
- Sababu zingine zinazoharibu neva za fahamu pamoja na mishipa ya damu ya macho
Kwa mujibu wa USDA, viazi huwa na mjumuiko wa nishati, aina mbalimbali za madini muhimu kwa mwili, vitamini pamoja na sukari. Ni virutubisho muhimu katika kujenga mwili wa binadamu ambapo macho ni sehemu ya viungo vinavyo uunda.
Kwa kuzingatia mgawanyiko wa virutubisho hivyo pamoja na kazi zake mwilini, JamiiForums imebaini kuwa madai ya chips kusababisha changamoto za macho hayana mashiko, hivyo ni uzushi. Ukaangaji wa viazi kwenye mafuta hauwezi kuleta madhara hasi yanayoweza kunasibishwa na magonjwa ya macho.
Hata hivyo, kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, aina hii ya chakula huhusishwa na kuongeza uzito na mafuta mabaya mwilini, shinikizo kubwa la damu pamoja na magonjwa ya mfumo wa damu na moyo.