SI KWELI Ulaji wa Chips husababisha ugonjwa wa Macho

SI KWELI Ulaji wa Chips husababisha ugonjwa wa Macho

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
<div class="bbWrapper"></div>
 
Tunachokijua
Kwa mujibu wa takwimu za WHO, takriban watu bilioni 2.2 duniani ni waathirika wa magonjwa ya macho yanayohusisha upofu na uoni hafifu.

Kwa kiasi kikubwa, sababu zinazopelekea upofu, uoni hafifu pamoja na changamoto zingine za macho ni-
  • Uzee
  • Mtoto wa jicho
  • Kisukari
  • Glaucoma
  • Sababu zingine zinazoharibu neva za fahamu pamoja na mishipa ya damu ya macho
Pia, takriban watoto 250,000-500,000 kila mwaka hupatwa na upofu kutokana na upungufu wa virutubisho vya Vitamini A. Hii inatoa maana kuwa vyakula pia huchukua sehemu muhimu katika kuamua uimara wa afya ya macho.

Kwa mujibu wa USDA, viazi huwa na mjumuiko wa nishati, aina mbalimbali za madini muhimu kwa mwili, vitamini pamoja na sukari. Ni virutubisho muhimu katika kujenga mwili wa binadamu ambapo macho ni sehemu ya viungo vinavyo uunda.

Kwa kuzingatia mgawanyiko wa virutubisho hivyo pamoja na kazi zake mwilini, JamiiForums imebaini kuwa madai ya chips kusababisha changamoto za macho hayana mashiko, hivyo ni uzushi. Ukaangaji wa viazi kwenye mafuta hauwezi kuleta madhara hasi yanayoweza kunasibishwa na magonjwa ya macho.

Hata hivyo, kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, aina hii ya chakula huhusishwa na kuongeza uzito na mafuta mabaya mwilini, shinikizo kubwa la damu pamoja na magonjwa ya mfumo wa damu na moyo.
<div class="bbWrapper"></div>
 
Back
Top Bottom