Ulaji wa kitunguu baada ya kula chakula

Ulaji wa kitunguu baada ya kula chakula

dendaboy

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2016
Posts
1,085
Reaction score
742
Jana nilikaribishwa kuungana na familia ya rafiki yangu mmoja kwa ajili ya chakula cha mchana vitu vilivyo andaliwa mezani ni pamoja na sahani iliyokua na vitunguu maji vikiwa vimemenywa na kukatwa sikua nimeelewa dhumuni la kuwepo vitunguu vile.

Baada ya kumaliza kula sasa ndipo walianza kila mtu kutafuna vile vitunguu sasa kwangu ilikua swala geni nikashindwa nikihofu naweza kurudisha chenchi
naomba wajuzi mnijuze nini faida yake kaa mkubwa mzizi mkavu na wengine karibuni.
 
Ingekua vyema zaidi ungewauliza wangekupatia majibu ila ngoja waje wanaofahamu hii kitu
 
Sasa kama uliona aibu kuwailiza wenyeji wako ambao ni watumiaji wenyewe sisi tutajuaje? Labda tumwite Mzizi mkavu aje atuelemishe.
 
Ingekua vyema zaidi ungewauliza wangekupatia majibu ila ngoja waje wanaofahamu hii kitu
ilikua vigumu kwangu kuanza kuhoji baada ya kukaribishwa.
nilihisi si jambo zuri
 
ilikuwa ni vyema kuwauliza walaji baada ya majibu unge kuja ku share nasi kuhusu majibu kuliko kutuuliza sisi badara ya walaji
 
Sasa kama uliona aibu kuwailiza wenyeji wako ambao ni watumiaji wenyewe sisi tutajuaje? Labda tumwite Mzizi mkavu aje atuelemishe.
ndio maana nimemuomba apite hapa.
 
Kitunguu maji kinafaida nyingi mwilini hasa pale unapokila bila kukiosha,si lazima ukile peke yake lakini hata ukitengeneza kachumbari we katia tu kula hivyo hivyo usiogope kunuka mdomo we hali afya yako,au kwa mfano unakula ubwabwa kata vitunguu vyako kwa mviringo mzuri kisha vipambie kwa kuvizungushia juu ya ubwabwa kisha mkaribishe mgeni lazima akasimulie
 
tupe faida yake
 
jana nilikaribishwa kuungana na familia ya rafiki yangu mmoja kwa ajili ya chakula cha mchana vitu vilivyo andaliwa mezani ni pamoja na sahani iliyokua na vitunguu maji vikiwa vimemenywa na kukatwa sikua nimeelewa dhumuni la kuwepo vitunguu vile.baada ya kumaliza kula sasa ndipo walianza kila mtu kutafuna vile vitunguu sasa kwangu ilikua swala geni nikashindwa nikihofu naweza kurudisha chenchi.
naomba wajuzi mnijuze nini faida yake kaa mkubwa mzizi mkavu na wengine karibuni.
Hebu mpigie simu huyo aliyekualika,na muulize kwamba ilikuwaje siku ile baada ya kumaliza kula,mkala vitunguu peke yake na si kachumbali?.Halafu njoo utujuze
 
Licha ya faida za vitunguu maji, nadhani hao rafiki zako wamejifunza utamaduni huo kutoka kwa wahindi. Kwa sehemu kubwa ya India, kila mlo lazima uambatane na vitunguu maji vilivyomenywa na kukatwa. Tena hata nyanya nazo huwa sehemu ya mlo. Nyanya hukatwa vipande vinne au zaidi na hazichanganywi na vitunguu kama tufanyavyo kwa kachumbali. Ni utamaduni wa kihindi zaid.
 
Back
Top Bottom