- Source #1
- View Source #1
Baadhi ya jamii huamini kuwa ulaji wa limao na ndimu husababisha upungufu wa damu mwilini.
Uvumi huu uliosambaa kwenye maeneo mengi hutoa maonyo makali hasa kwa watoto na wanawake wenye ujauzito wanaojaribu kutumia matunda haya.
Je, ni kweli kuwa matunda haya hukausha damu mwilini?
Uvumi huu uliosambaa kwenye maeneo mengi hutoa maonyo makali hasa kwa watoto na wanawake wenye ujauzito wanaojaribu kutumia matunda haya.
Je, ni kweli kuwa matunda haya hukausha damu mwilini?
- Tunachokijua
- Kwa mujibu wa Idara ya Kilimo ya Marekani (USDA, ) limao (ndimu) huwa na mjumuiko wa nishati, protini, wanga, nyuzilishe, madini ya calcium, magnesium, phosphorus, potassium, sodium, zinc, copper, selenium na kiasi kidogo cha sukari.
Huwa na vitamini C, citric acid, vitamini B12, folate pamoja na viondoa sumu vya carotene, vitamini E, lutein na zeaxanthin.
Madini ya chuma, folate na vitamini B12 hufanya kazi kwa pamoja katika kuwezesha utengenezwaji wa damu mwilini.
Aidha, vitamini C na citric acid huhitajika kwenye kuzuia tatizo la Anemia linaloweza kutokea baada ya mwili kushindwa kufyonza madini ya chuma yanayopatikana kwenye mlo kisha kusababisha upungufu wa damu.
Taasisi ya Chakula la Lishe Tanzania inazungumziaje suala hili?
JamiiCheck pia imefuatilia ukweli wa madai haya kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, TFNC, ambayo kwa mujibu wa Maelezo yanayopatikana kwenye tovuti yake rasmi, matunda haya hayasababishi upungufu wa Damu, bali huusaidia mwili kuongeza damu zaidi.
“Ndimu na limau ni matunda yenye vitamini C ambayo husaidia katika ufyonzwaji wa madini ya chuma yanayopatikana kwenye vyakula. Madini ya chuma ni muhimu katika kutengeneza chembechembe nyekundu za damu. Kwa mantiki hiyo matumizi ya ndimu na limau hutumika kama kichocheo kimajawapo cha kuongeza damu mwilini na wala si kupunguza damu mwilini.
Pia ifahamike kwamba ndimu na limau husaidia kuongeza hamu ya kula hasa kwa mtu anayepata kichefuchefu na kutapika” wanaandika TFNC
Taasisi hii inawataka watu kupuuza madai hayo kwani hayana ukweli.
Kwa kurejea vyanzo hivi, JamiiCheck imebaini sio kweli kuwa matunda haya hakausha damu, bali huusaidia mwili kutengeneza damu pamoja na kuzuia upungufu wake.