Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Kuna hii stori ambayo nimekuwa nikiisikia sana mtaani tangu nikiwa mdogo, eti "Ukipenda sana kula mayai, moyo wako utatanuka."
Zamani tulikuwa tunaogopeshwa sana na hii kauli ya "moyo kutanuka," na wengi wetu tukajikuta tunaogopa kula mayai kwa kuhofia afya zetu. Wengine wanasema shida ni kile kiini cha njano, wengine wanasema ugonjwa unakuja ukila mayai ya kisasa tu. Bibi alitunyima kabisa kula mayai kwa hofu hiyo.
Lakini nikikaa na kufikiria kwa kina, najiuliza maswali haya:

- Je, ni kweli yai lina uwezo wa kutanua misuli ya moyo moja kwa moja kimwili?
- Au labda wazee wetu walikuwa wanachanganya ishu ya mafuta au lehemu (Cholesterol) inayoweza kuziba mishipa ya damu na dhana nzima ya moyo kutanuka?
- Sayansi ya sasa inasemaje kuhusu ulaji wa mayai na afya ya moyo wako kwa ujumla?